Symbion Power acquires DOWANS Power plant

Symbion Power acquires DOWANS Power plant

duuh, kudadadeki hiki ni kichwa bwana!! ndio maana kina Nape hawalali!!
 
Alieumwa na nyoka akiona unyasi anakimbia.

Si rahisi mimi kwaamini hawa watu.
- nahisi kuwa beli hii ni kutuhadaa ili tutamani kufanya nao kazi.
- Misimamo huwa ni rahisi kutunga lakini migumu kutekeleza, je tutakuwa tunabadili misimamo yetu kwa kuonyeshwa karoti kila mara??
 
Dr Slaa, ni kweli kabisa wananchi tulio wengi tunasoma katiba kma kusoma gazeti la SANI au MCHESHI.
Katiba iko wazi Tafsiri imefinyangwa na Mafisadi wa Serikali ya CCM kwa woga wa kutiwa JambaJamba na wananchi.

Nakushukuru sana mimi binafsi nimefumbuliwa macho kwa hilo.

Mzee mwenzangu Mwanakijiji mtafute tena Dr Slaa ili aendelee kutupa SHULE zaidi. Pia ni vema ukimtafuta Mkongwe mwingine wa CCM ili ajibu maswali kuhusu malalamiko ya wananchi pia mwelekeo wa CCM na serikali yao.

Serikali na watu
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6



8.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata
misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo -


(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali
itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa
wananchi kwa mujibu wa Katiba hii; (
Maana yake sisi wananchi tukisema basi mamalaka ya serikali inakoma pale pale, kuna haja ya msingi ya kubainisha namna wananchi tuwezavyo kutumia sheria hii kivitendo.Pia kuna haja ya kuiparaphrase sheria hii ili ieleweke vyema katika lugha nyepesi ,ya kawaid na isiyo na tungo Tata. Hapo kwenye kifungu "a" ndipo pamalizapo Mzizi wote wa Fitna kati yetu na Mabaradhuri walafi viwavi wa CCM. Wananchi tunatiwa hofu kwa sababu tumefumbia macho maarifa na zaidi Haki zetu za msingi za kuisoma na kuitafiri sheria ya nchi. Seikali haina nguvu mbele ya wananchi pia serikali haiwezi kuwatishia wananchi, na hakuna mtu au kundi la watu ndani ya serikali wenye mamlaka zaidi ya wananchi) Serikali imekuwa ikiwageuzia kibao wananchi ili waendelee kuumia kwa gharama ya jasho na damu yao wenyewe.

(b) Lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;

(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;

(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao
kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

(2) Muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar, au wa chochote kati ya vyombo
vyake na uendeshaji wa shughuli zake, utatekelezwa kwa
kuzingatia umoja wa Jamhuri ya Muungano na haja ya
kukuza umoja wa kitaifa na kudumisha heshima ya Taifa.
 
Angalia nyuma ya AVATA yako kasimama Ninja kuhakikisha kwamba unatumika ipasavyo na unasema kileuamriwacho kusema.
Ni maneno ya kusindiliwa bila hiana na walio nyuma ya ujumbe.

Hivi ataongea kipi cha maana zaidi ya ufataani?,
 
@Mwanakijiji nasikia tu majibu ya Dr ila maswali yako siyasikii. please check on it any resolve acoordingly
 
Naomba kujuzwa!!hawa symbion watakuwa wanasambaza wenyewe au wanauza kwa tanesco tu?sasa wale mafundi woote wale zaidi 200 wa nini??naomba kujulishwa hilo!
 
Hivi hao Symbion ndo kazi wanazotufundisha watanzania??

Yaani badala ya kuwafundisha watu jinsi ya kuendesha na ku-configure mamitambo yao, wao wanawafundisha kukwea mistimu(nguzo)..

Tunajua kazi ni kazi, lakini kwa hii, hata ukikusanya vijana pale Ubungo wanafanya tena haraka kabisa..
 
Inaonyeesha hapa kwenye Symbion pana maswali mengi kidogo!
Hata mimi nisichoelewa kuhusiana na kampuni hii ni: je baada ya kununua hii mitambo ya Dowans wataihamisha au itabaki palepale ilipo?
Lakini pia nadhani walishahakikishiwa soko la umeme na mtu fulani, vinginevyo wasingenunua mitambo mizito hivyo, ndio waanze kutafuta soko!
Halafu ni juniors sana hawa watu...kama wameanza mwaka 2005 yaonyesha wanaendelea kujifunzia vichwani mwetu!...anyway!
Bado kuna harufu fulani unpleasant hapa kwa symbion!
 
Nakubaliana na katibu mkuu nishati alivyosema majuzi kwamba tunataka umeme, sio siasa alipokuwa anazungumzia suala la Symbion, lakini kisheria tupo wapi katika hili ili tusije pata vikwazo tena huko mbeleni yaifanye Symbion ibadilike tena and become Chameleon. Tumechoka na mgao ambao umekaa kisiasa zaidi kuliko kitaalam in my view.

Wanasheria, uelewa wangu kuhusu Symbion kisheria ni mdogo sana, ndio maana uwepo wenu ni muhimu sana. Nawaomba msaada katika hili. Ni nini tofauti kubwa kati ya Symbion na Dowans? Ile kesi ya kupinga dowans kulipwa fidia, imeishia wapi? Kama bado ipo, ikipatiwa hukumu, itaathiri vipi suala la Symbion? Inachanganya kwa kweli. Kwa uelewa wangu finyu sana, suala la Dowans lilishamalizika bungeni mwaka jana; Suala la fidia nalo nahisi limesimama; Na leo katika vyombo vya habari, Tanesco, kamati ya bunge nishati na madini na wizara ya nishati wameridhia biashara na Symbion na according to Tanesco, wapo katika mchakato wa kuingia mkataba na symbion kununua umeme; Baraza la mawaziri kazi kubwa ni kutunga na kutekeleza sera mbali mbali, au sio? Bunge nalo kazi yake ni kutunga sheria, among other things au sio? Suala la Symbion limepitishwa kisera zaidi au kisheria or both? Kama ni kisheria, uamuzi wa chombo cha kutunga sheria yaani bunge wa mwaka jana juu ya Dowans umekaa vipi katika symbion? Kama kisera, suala la symbion kama limepata Baraka ya baraza la mawaziri, kuna synergy gani kisheria na kisera katika suala hili?

Kunapochanganya zaidi, juzi afisa mawasiliano wa tanesco alipoulizwa TBC kwenye taarifa ya habari saa mbili usiku je wananchi waelewe nani mwenye kauli ya mwisho, kamati ya bunge nishati na madini? Tanesco? Au wizara nishati na madini? Akajibu kwamba tanesco na wizara wana msimamo mmoja, akakwepa suala la kamati ya bunge nishati na madini; Sasa katika suala la symbion, tuelewe kwamba uamuzi wa kuiridhia symbion kibunge umefanywa kwa niaba ya chombo cha kutunga sheria (bunge) na kamati ya nishati na madini kwa niaba ya bunge au bado kuna hatua ya suala hili suala kwenda pata Baraka bungeni? Na je, Bunge mwaka jana lilimaliza suala la Dowans kama kampuni? Dowans kama mitambo? Dowans kama mrithi wa richmon? Au dowans kama mchakato mzima wa kupata tender?kama lililomalizwa lilikuwa ni suala la kampuni, hali ya leo ipo vipi under symbion? Kama lililomalizwa ni suala la mitambo, hali ipo vipi? Kama lililomalizwa ni mchakato mzima wa tender, hilo nalo lipo vipi katika mazingira mapya ya symbion? Na pia je, nini tofauti kubwa kati ya mabadiliko from Zain to Airtel na Dowans to Symbion katika sheria zetu Tanzania? Na je, hapa pia kuna kodi tumezikosa kutokana na ubovu wa sheria zetu?
 
Nakubaliana na katibu mkuu nishati alivyosema majuzi kwamba tunataka umeme, sio siasa alipokuwa anazungumzia suala la Symbion, lakini kisheria tupo wapi katika hili ili tusije pata vikwazo tena huko mbeleni yaifanye Symbion ibadilike tena and become Chameleon. Tumechoka na mgao ambao umekaa kisiasa zaidi kuliko kitaalam in my view.

.... .... .... ......................................hapa pia kuna kodi tumezikosa kutokana na ubovu wa sheria zetu

Naona EL na RA wanakurudisha kwa gea nyingine waambie hatudanganyiki. Kiama chenu kimefika na hapo ndipo mtajua nini ni mbivu.

 
Kuna tofauti kubwa kama mwanga ulivyo na tofauti na giza. Maswali yaliyopo yanahitaji kujibiwa katika majadiliano. Hadi hivi sasa hili ni suala la Symbion na Dowans.. nasubiri litakapokuwa Symbion na Tanesco..
 
Naona EL na RA wanakurudisha kwa gea nyingine waambie hatudanganyiki. Kiama chenu kimefika na hapo ndipo mtajua nini ni mbivu.


Sina Ubia na na hawa watu na sina sababu ya kuwa na ubia wa aina yoyote nao. Vinginevyo mimi ni mtoto wa maskini, umaskini wangu utaniweka vipi karibu nao? Hawaniongezei wala kunipunguzia maisha yangu na wala sipo katika fikra zao kwani mimi kwao sio lolote. Nina waheshimu kama wakubwa wangu, na ninawasoma katika vyombo vya habari wakituhumiwa na ufisadi huku wakitakiwa wajiondoe wenyewe katika chama kabla ya kuondolewa kwa nguvu. Huo ni mzigo wao na hao wanaowatuhumu. Vinginevyo sijwahi kuwa na mkataba nao na wala sijawahi wahitaji na wala sitawahitaji katika maisha yangu yote yaliyobakia duniani.
 
Kuna tofauti kubwa kama mwanga ulivyo na tofauti na giza. Maswali yaliyopo yanahitaji kujibiwa katika majadiliano. Hadi hivi sasa hili ni suala la Symbion na Dowans.. nasubiri litakapokuwa Symbion na Tanesco..

Sawa sawa.
 
Watu wengine nanyi mlipata tatizo hilo?

hapana...inakata abruptly wakati anajibu maswali mawili ya mwisho. Lile la dowans na tarime! Anapokuwa anamalizia la dowans ghafla mziki unaanza. Kwa hiyo hatujasikia chochote juu ya tarime mkuu.
 
Wakuu Salaam,
Kampuni ya Umeme nchini (TANESCO) imesema kuwa zaidi ya 70% ya mapato yake inatumika kuilipa kampuni ya kufua umeme ya Songas na bado umeme unaozalishwa na kampuni hiyo hautoshelezi mahitaji ya nchi.

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Bw. William Mhando wakati akihojiwa na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.
Mhando alisema Serikali haitoa ruzuku kwa ajili ya kuendeshea kampuni hiyo na vilevile ni vigumu kwa kampuni hiyo kukopesheka kwa kuwa haiwezi kujiendesha kibiashara kutokana na mzigo huo mkubwa wa kuilipa kampuni ya Songas.

My take: Kama mambo haya ni kweli basi kazi tunayo.

Source: Mtanzania 25.02.2011
 
Kampuni ya umeme nchini Tanesco imesema mazungumzo na kampuni ya kuzalisha umeme ya Symbion Power yamefikia hatua nzuri na wanatarajia kusaini mkataba wa kuuziana umeme na kampuni hiyo muda wowote ndani ya wiki mbili.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO wakati wa kikao cha kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

Kampuni ya Symbion Power ndiyo iliyoinunua kampuni ya Dowans/Richmond ambayo iliingia kwenye utata wa kisheria na Serikali/Tanesco kutokana na kasoro nyingi za kisheria katika mkataba wa kuzalisha umeme kati yake na Tanesco/serikali.

May take: Mkataaba wa Dowans haukuwa halali kutokana na kuwa na kasoro zilizorithiwa kutoka Richmond. Je iweje uwe halali kwa Symbion Power?
 
Back
Top Bottom