Kuna tofauti kubwa kama mwanga ulivyo na tofauti na giza. Maswali yaliyopo yanahitaji kujibiwa katika majadiliano. Hadi hivi sasa hili ni suala la Symbion na Dowans.. nasubiri litakapokuwa Symbion na Tanesco..
Kampuni ya umeme nchini Tanesco imesema mazungumzo na kampuni ya kuzalisha umeme ya Symbion Power yamefikia hatua nzuri na wanatarajia kusaini mkataba wa kuuziana umeme na kampuni hiyo muda wowote ndani ya wiki mbili.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO wakati wa kikao cha kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.
Kampuni ya Symbion Power ndiyo iliyoinunua kampuni ya Dowans/Richmond ambayo iliingia kwenye utata wa kisheria na Serikali/Tanesco kutokana na kasoro nyingi za kisheria katika mkataba wa kuzalisha umeme kati yake na Tanesco/serikali.
May take: Mkataaba wa Dowans haukuwa halali kutokana na kuwa na kasoro zilizorithiwa kutoka Richmond. Je iweje uwe halali kwa Symbion Power?
Wakuu Salaam,
Kampuni ya Umeme nchini (TANESCO) imesema kuwa zaidi ya 70% ya mapato yake inatumika kuilipa kampuni ya kufua umeme ya Songas na bado umeme unaozalishwa na kampuni hiyo hautoshelezi mahitaji ya nchi.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Bw. William Mhando wakati akihojiwa na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.
Mhando alisema Serikali haitoa ruzuku kwa ajili ya kuendeshea kampuni hiyo na vilevile ni vigumu kwa kampuni hiyo kukopesheka kwa kuwa haiwezi kujiendesha kibiashara kutokana na mzigo huo mkubwa wa kuilipa kampuni ya Songas.
My take: Kama mambo haya ni kweli basi kazi tunayo.
Source: Mtanzania 25.02.2011
Inaonyeesha hapa kwenye Symbion pana maswali mengi kidogo!
Hata mimi nisichoelewa kuhusiana na kampuni hii ni: je baada ya kununua hii mitambo ya Dowans wataihamisha au itabaki palepale ilipo?
Lakini pia nadhani walishahakikishiwa soko la umeme na mtu fulani, vinginevyo wasingenunua mitambo mizito hivyo, ndio waanze kutafuta soko!
Halafu ni juniors sana hawa watu...kama wameanza mwaka 2005 yaonyesha wanaendelea kujifunzia vichwani mwetu!...anyway!
Bado kuna harufu fulani unpleasant hapa kwa symbion!
Kuna tofauti kubwa kama mwanga ulivyo na tofauti na giza. Maswali yaliyopo yanahitaji kujibiwa katika majadiliano. Hadi hivi sasa hili ni suala la Symbion na Dowans.. nasubiri litakapokuwa Symbion na Tanesco..
Of course kwenye biashara kuna kila mbinu, kila mtaji unapokuwa mkiubwa na ndio mbinu za kibiashara zinakuwa kubwa. Wafanya biashara wakubwa na waliofaulu vyema kwenye biashara zao, hutegemea sana intelijensia za kibiashara, mahusiano na watu aina na kada mbalimbali, kunusa harufu ya faida na hasara mapema, uwezo wa kufanya maamuzi ya haraka.
Hivi katika vigezo hivyo vyote, ni mfanya biashara yupi atatumbukiza kiwango kikubwa cha fedha bila kuwa na intelijensia zilizomfanya aamue kutumbukiza fedha yake? Leo hii hata ukitaka kwenda machungwa toka muheza, kama hujatazama bei ya soko, kama hujatazama usafiri wa uhakika, kama hujatazama ni nani au wapi ukiyafikisha yatanunuliwa kwa haraka na kwa faida nzuri, basi utakuwa unacheza mchezo wa pata potea na hufanyi biashara.
Kwa mantiki hiyo, Symbion, wameyafanya yote kabla na ndio maana wanaingia katika hii biashara. Na kama hawajafanya hivyo watakuwa si wafanya biashara.
Dah! wakifanya hivyo watakua wameua kabisa!Naona hii ndio siri ya Mgawo mkali wa sasa hivi. Tena wanasema wataiwasha Jumatatu ijayo!
Of course kwenye biashara kuna kila mbinu, kila mtaji unapokuwa mkiubwa na ndio mbinu za kibiashara zinakuwa kubwa. Wafanya biashara wakubwa na waliofaulu vyema kwenye biashara zao, hutegemea sana intelijensia za kibiashara, mahusiano na watu aina na kada mbalimbali, kunusa harufu ya faida na hasara mapema, uwezo wa kufanya maamuzi ya haraka.
Hivi katika vigezo hivyo vyote, ni mfanya biashara yupi atatumbukiza kiwango kikubwa cha fedha bila kuwa na intelijensia zilizomfanya aamue kutumbukiza fedha yake? Leo hii hata ukitaka kwenda machungwa toka muheza, kama hujatazama bei ya soko, kama hujatazama usafiri wa uhakika, kama hujatazama ni nani au wapi ukiyafikisha yatanunuliwa kwa haraka na kwa faida nzuri, basi utakuwa unacheza mchezo wa pata potea na hufanyi biashara.
Kwa mantiki hiyo, Symbion, wameyafanya yote kabla na ndio maana wanaingia katika hii biashara. Na kama hawajafanya hivyo watakuwa si wafanya biashara.
Mashirika ya uma yako chini ya nani Fauzia??? sio serikali?? serikali ni mwajiriwa wa nani Fauzia??? sio wa wananchi???? wananchi ni akina nani sasa?? sio mimi na wewe na yule?? sasa lawama abebe nani kama sio sisi wenyewe tunaokaa kimya pamoja na kuona maovu yote haya?Tanesco wizi mtupu, au huyajui mashirika ya umma? kwani yote yamekufa kwa nini? si ufisadi wa wafanyakazi wa hayo mashirika.
Nakubaliana na katibu mkuu nishati alivyosema majuzi kwamba tunataka umeme, sio siasa alipokuwa anazungumzia suala la Symbion, lakini kisheria tupo wapi katika hili ili tusije pata vikwazo tena huko mbeleni yaifanye Symbion ibadilike tena and become Chameleon. Tumechoka na mgao ambao umekaa kisiasa zaidi kuliko kitaalam in my view.
Wanasheria, uelewa wangu kuhusu Symbion kisheria ni mdogo sana, ndio maana uwepo wenu ni muhimu sana. Nawaomba msaada katika hili. Ni nini tofauti kubwa kati ya Symbion na Dowans? Ile kesi ya kupinga dowans kulipwa fidia, imeishia wapi? Kama bado ipo, ikipatiwa hukumu, itaathiri vipi suala la Symbion? Inachanganya kwa kweli. Kwa uelewa wangu finyu sana, suala la Dowans lilishamalizika bungeni mwaka jana; Suala la fidia nalo nahisi limesimama; Na leo katika vyombo vya habari, Tanesco, kamati ya bunge nishati na madini na wizara ya nishati wameridhia biashara na Symbion na according to Tanesco, wapo katika mchakato wa kuingia mkataba na symbion kununua umeme; Baraza la mawaziri kazi kubwa ni kutunga na kutekeleza sera mbali mbali, au sio? Bunge nalo kazi yake ni kutunga sheria, among other things au sio? Suala la Symbion limepitishwa kisera zaidi au kisheria or both? Kama ni kisheria, uamuzi wa chombo cha kutunga sheria yaani bunge wa mwaka jana juu ya Dowans umekaa vipi katika symbion? Kama kisera, suala la symbion kama limepata Baraka ya baraza la mawaziri, kuna synergy gani kisheria na kisera katika suala hili?
Kunapochanganya zaidi, juzi afisa mawasiliano wa tanesco alipoulizwa TBC kwenye taarifa ya habari saa mbili usiku je wananchi waelewe nani mwenye kauli ya mwisho, kamati ya bunge nishati na madini? Tanesco? Au wizara nishati na madini? Akajibu kwamba tanesco na wizara wana msimamo mmoja, akakwepa suala la kamati ya bunge nishati na madini; Sasa katika suala la symbion, tuelewe kwamba uamuzi wa kuiridhia symbion kibunge umefanywa kwa niaba ya chombo cha kutunga sheria (bunge) na kamati ya nishati na madini kwa niaba ya bunge au bado kuna hatua ya suala hili suala kwenda pata Baraka bungeni? Na je, Bunge mwaka jana lilimaliza suala la Dowans kama kampuni? Dowans kama mitambo? Dowans kama mrithi wa richmon? Au dowans kama mchakato mzima wa kupata tender?kama lililomalizwa lilikuwa ni suala la kampuni, hali ya leo ipo vipi under symbion? Kama lililomalizwa ni suala la mitambo, hali ipo vipi? Kama lililomalizwa ni mchakato mzima wa tender, hilo nalo lipo vipi katika mazingira mapya ya symbion? Na pia je, nini tofauti kubwa kati ya mabadiliko from Zain to Airtel na Dowans to Symbion katika sheria zetu Tanzania? Na je, hapa pia kuna kodi tumezikosa kutokana na ubovu wa sheria zetu?