Swali kwa waliooa tu

Perry

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
10,043
2,000
Mnawezaje kudumisha ndoa zenu pamoja na vishawishi vyote hvi vnavowazunguka?
 
Au usitoe mahari, unajua mahari nayo huwa inakonfuse, unakuwa na uchungu sana kwa mkeo.
 
Kwani ulipoamua kuoa vishawishi havikuwepo???acha tamaa...tulia na mke au GF wako...Kwenye hiii dunia kila kitu kipo..uamuzi ni wako tuu
 
Vishawishi vipo saaana tu, Ukitingwa mara mojamoja ruksa ila usihamie
 
Mnawezaje kudumisha ndoa zenu pamoja na vishawishi vyote hvi vnavowazunguka?

Bado tumo ulimwenguni humu, ingawa aliyezaliwa mara ya pili yeye si wa ulimwengu huu (Yohana 17:16). Lakini kwa kuwa bado tumo katika ulimwengu uliojaa dhambi inayotutamani kila siku, na tusije tukajisahau. Inatupasa tuishinde.
Imeandikwa katika kitabu cha (Warumi 6:12-14)
“Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu, ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake; wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi, bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi, bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki. Kwa maana DHAMBI HAITA WATAWALA NINYI, kwa sababu hamuwi chini ya sheria, bali chini ya neema”.

​Tena imeandikwa;
“Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu HATENDI DHAMBI; bali yeye aliyezaliwa na Mungu HUJILINDA, wala yule mwovu HAMGUSI.” (1 Yohana 5:18)
Ee, mtu wa Mungu, jilinde basi kwa kuwa umezaliwa na Mungu, kwa nini tamaa ya uasherati ikusonge? Je?! umesahau ni uzao wa namna gani ulio ndani yako?
Ni kweli kwamba mtu akitenda dhambi na akatubu, Bwana atamsamehe, (1 Yohana 1:9). Lakini hatutakiwi kutenda dhambi. Ndiyo maana imeandika; “Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba MSITENDE DHAMBI”…. (1 Yohana 2:1)
 
Usiwe na shaka mkuu...Ukishaoa vishawishi vinakufa naturally...Join us and enjoy the dance!
 
Back
Top Bottom