Sumu ya Saanene - swali kwa MASALIA a.k.a PM-7

Sumu ya Saanene - swali kwa MASALIA a.k.a PM-7

ha ha ha leftovers --aka mabaki -- sasa mabaki ya nani mi sijui waulize wenyewe.

haaa haaa

mkuu FUSO

ben saanane alivyo smart hili neno 'masalia' litakuwa lina maana pana na limeficha mambo mengi sana
 
Last edited by a moderator:
Sumu ni sumu,tayari taarifa hizi police wanazo na si Saa nane tu,kuna viongozi watatu wa chadema watahojiwa na njama zao za kumtoa uhai Zitto.Hii insu itaondoka na watu ambao hamujawai tarajia na hapo ndipo tutakapojuwa nan mnafiki na muuaji chadema.

Ushirikina utawatesa sana nyie!! Kawaambie na wenzako!!
 
Unajua mwizi akikosa pa kuiba anaweza kuiba hata mboga aliyopika mkewe

kaka.wahuni sio watu.anaweza akampa mkewe chapaa ya matumizi halafu anamuibia then anakuja kumuuliza mke wangu mbona hupiki huku povu linamtoka na mikwala mingine mingiiii.
 
hizi accusations zisichukuliwe kimzaamzaa! Inabidi anayedaiwa kutaka kumnywesha sumu Zitto aende mahakamani kwa kuchafuliwa mbele ya jamii ukweli ujulikane upo wap!? haya madai mazito aisee....
 
Zitto amepata mapigo mawili kwa mpigo
1: Usaliti wake umejulikani
2: Mh Lema ambaye alikuwa anamhujumu (rejea maelezo ya Ben) amerudishiwa ubunge wake
 
Wana jamvi,
Ben Saanane and E. Mamuya wametoa maelezo yao (allegations) kuhusu jinsi Zitto Kabwe (mb) na wengine (Juliana Shonza, H. Mchange, M. Mwampamba, Gwakisa, E. Sanga, Dr. Kitila Mkumbo) wamekuwa wakidhoofisha CDM. Katika utetezi wa baadhi yao [Zitto Kabwe (ZZK), J. Shonza, na H. Mchange) wamekuwa wakikwepa kujibu hoja au tuhuma zilizoelekezwa kwao, nadhani kwa makusudi au kutokana na uelewa mdogo. Hoja (issues) ni kama ifuatavyo.

  1. ZZK ni amekuwa akifadhili kikundi cha waasi, ‘Masalia’, kwa kueneza kwa makusudi propaganda za udini, ukanda, na ukabila. Lengo kuu ni kudhoofisha CDM, ili ZZK aweze kujijenga na kupata nguvu katika CDM (na baadae kuwa kugombea urais?) au kuhakikisha CDM inaipa CCM nafuu. (Angalia, Mamuya, Ben, DEC 18-20, 2012).


  1. Ben na Mamuya wanadai wanafahamiana na ZZK na wameshiriki nae kwenye hujuma za kudhoofisha CDM, kabla ya wao (Ben na Mamuya) kurudi kwenye mstari (Mamuya, Ben).


  1. ZZK alishiriki kuchochea mgogoro wa madiwani wa Arusha wa CDM. Hujuma hizi pia zilimhusisha Dr. Kitila Mkumbo (Mamuya, Ben).
    1. ZZK aliwapa moyo (encourage) madiwani waliofukuzwa CDM kwa kuwaamba wakomae tu watashinda na kuwasihi wasiombe msamaha.
    2. ZZK alikuwa akiwasaliana na madiwani wa CDM-Arusha waliofukuzwa kwa njia ya sma wakati wa kikao cha Kamati Kuu-CDM kilichikuwa kikiwajadili. Wadiwani hao wali-forward sms hizo kwa Mamuya wakati kikao kikiendelea


  1. Mara nyingi Mamuya alipokuwa Dar ZZK alimkutanisha yeye Mamuya, Mchange, Mwampamba, Shonza, Gwakisa, F. Sanga kwa nyakati tofauti kwa ajili ya kupanga mikakati ya kudhoofisha viongozi wakuu wa CDM, hasa F. Mbowe (mb) na Dr. Slaa. Lengo lilikuwa kuwagombanisha ili ZZK aweze kung’ara (Mamuya, Ben).


  1. Dr. Kitila Mkumbo alishiriki kutoa mikakati ya kumdhoofisha G. Lema (mb) ili madiwani wa Arusha (hasa Estomih Milah) aweze kuwa na nguvu kisiasa kumzidi Lema (Mamuya, Ben).


  1. Dr. Kitila Mkumbo alivijisha repoti ya ‘Kamati ya Marando (Mamuya).


  1. Tarehe 18-12-2012 Dr. Kitila Mkumbo alikutana na ZZK, na baadae Dr. Mkumbo alikutana na Ben. Dr. Mkumbo alimwomba Ben akanushe thread ya Mamuya. Ben alikataa. Hii ilipekea ZZK kuanzisha thread ambapo alikana kumfahamu Ben (Ben).


  1. Kundi la Masalia linalodhaliwa na ZZK lilifanya propaganda chafu dhidi ya CDM. Ben anakiri kushiriki katika kundi hili kabla ya kurudi kwenye mstari (kuungama?). Ben.


  1. Kundi la Masalia wamekuwa wakitoa tuhuma za ‘kuchinjana’ dhidi ya Ben. Ben anasema mbinu wamekuwa wakiitumia kama ngao wakati akiwa bado yuko nao (masalia), kwa hiyo anajua watumia mbinu hii ili kubadili hoja. Ben


  1. ZZK na kundi lake la Masalia wamekula kiapo kwa mganga wa kienyeji (mchawi??) ili wasisalitiane katika juhudi za kudhoofisha CDM. Ben, Shonza walikataa kula kiapo. Ben.

Majibu (responses) ya ZZK, Shonza, na Mchange yasioridhisha au kujibu hoja za Mamuya na Ben


  1. Majibu ya ZZK

  • Anadai hamjui Ben, japo hajamkana kumjua Mamuya. Anadai amekuwa akiwasiliana na Ben kwa simu kama mara mbili au tatu kwa mambo ya kitaaluma au pale Ben alipokuwa akionewa kwenye chama (wakati wa uchaguzi wa Bavicha?)
    • Swali. ZZK ni mwana taaluma?
    • Uki-connect dots, kwa nini ZZK awe so much concerned na issue za Ben za kitaaluma na kisiasa kwa muda mrefu bila hata kuwahi kuonana nae hata mara moja?
      • Hapa ZZK anaonekana kukwepa hoja namba 2 ili tuhuma za Ben/Mamuya zionekane ni za uongo. Implication. ZZK ni mwongo na/au anajaribu kukwepa hoja (ameona aibu baada kushikwa pabaya?)
  • Anajaribu kukwepa hoja kwa kuzungumzia (kwa majivuno) mchango wake katika CDM. Pamoja na kukwepa hoja za Ben na Mamuya, tujiulize.
    • CDM alianzishwa lini na ZZK alijiunga na CDM lini kiasi cha kujivuna kiasi hiki?
    • Je, ni kweli siku zote mtu akiwa na mchango mkubwa kwenye chama hawezi kusaliti chama kama? Mbona waswahili wanasema ‘mvunja nchi ni mwananchi’? Hii si ndio ngao yake ya kuficha maovu yake?


  • Badala ya kujibu hoja, anasema hajawahi kuwa mwanachama wa chama chochote.
    • Hii sio sehemu ya hoja za Ben/Mamuya. Ameulizwa na nani? Nafikiri hii ilikuwa ni mwendelezo wa propaganda za kumiliki kadi (ametoa kijembe indirectly) ili ku water down tuhuma dhidi yake.
    • Japo sio sehemu ya hoja, kwani kama hajawahi kuwa mwanachama chochote cha siasa zaidi ya CDM ndio inahalalisha kutokisaliti chama?
  • Anahimiza watu wajenge chama badala ya kueneza majungu. Sawa kabisa!!!. Lakini akumbuke kuwa wakati wa kujenga chama ni vema pia kuwa makini kwani wakati wa vita kuna kuwa na wasaliti pia. Hakuna kazi yoyote isiyokuwa na usaliti. Hivyo, hoja za Ben na Mamuya kuwa ZZk anaendesha kundi la masalia (wasaliti0 alipaswi kupuuzwa kijumla jumla.
  • Badala ya kujibu hoja, ZZK amekimbilia kutoa dharau, vitisho (uchawi), majivuno, na tuhumu ambazo, ukiangalia kwa undani zinalenda kubadili mwelekeo (focus).
  • Ili kuzima mjadala au kuji defend, au kuwatisha watoa hoja (Ben na Mamuya), ZZK amekimbilia kutoa vitisho vya uchawi.
    • Hii analenga’ kutishia nyau’?
    • Kwani kutoka Kigoma ndio ‘dili’ ya kufanya maovu huku watu wakikuogopa?
    • Mbona hakutumia ‘uchawi’ ili asisimamishwe ubunge wakati wa sakata la Buzwagi?
    • Kwani Kigoma ndio nini? Wachawi????? Mbona ‘kwetu pia wapo’?—Sam wa Ukweli.


  1. Majibu ya Mwampamba

  • Anaonekana kukana kundi ya ‘Masali’ wakati huo huo akijichanganya kwa kukiri kufahamu members wa Masalia.
  • Anakiri kuwafahamu Ben na Mamuya, tofauti na ZZK, tangu uchaguzi wa Bavicha.
    • Kwa kukiri kuwafahamu Ben na Mamuya, kihesabu, ZZK anamfahamu Ben, japo anakana, kwani Mwampamba anasema ni mfuasi wa ZZK. Hii inatthibitisha uwepo wa kundi la masalia.


  • Amekwepa hoja kwa kutoa hadithi za uchaguzi wa Bavicha. Hata hivyo, katika kukwepa hoja, inapekelea kutoa mwanga kuwa kundi la Masalia lilianzishwa au kushamiri tangu uchaguzi wa Bavicha. Na hapa inaonekana ndio mikakati ya ZZK kuanza juhudi za kudhoofisha chama au kugonganisha viongozi ili yeye ashamiri. Pia huu ulikuwa mwanzo wa mikakati ya ‘wabaya’ wa CDM, nje na ndani ya chama.
    • Inaonekana uongozi wa CDM uligundua mbinu ya kuweka mamluki kuvuruga chama wakati wa uchaguzi wa Bavicha. ZZK alitumia udhaifu wa vijana waliokosa uongozi kuweza kuanzisha kundi la Masalia. Hata hivyo, mmoja wao (Shonza) alipenya na kuwa kiongozi.
    • Ukwepaji wa hoja wa Mwampamba pia unaonyesha jinsi walioanza mbinu za kuwagonganisha Mbowe (mb) na Dr. Slaa.


  • Badala ya kujibu hoja Ben and Mamuya, Mwampamba anaongelea utiifu wake kwa ZZK (nadhani kutokana na kiapo kwa mganga/mchawi???).
    • Para 14 ya maelezo ya Mwampamba anaongelea propaganda zile zile zinazotumiwa na ‘upande wa pili’.
      • Ni kama vile maneno haya wamekaririshwa (kwa mganga/mchawi??) kwani ni word-to-word ya yale ambayo Shonza na ‘wale wa upande wa pili’ wamekuwa wakiyatumia.


  • Mwampamba, katika para 15-17, anazungumzia propaganda zile zile za ‘upande wa pili’ au waumini wa kundi la ‘Masalia’.
    • Lengo ni ku-tarnish image ya viongozi wa juu wa CDM, hasa Dr. Slaa.


  1. Majibu ya Juliana Shonza

  • Japo hajibu hoja moja kwa moja, Para ya 2 anaonyesha kuwajua watu walioko kundi la ‘Masalia’ (bila yeye kujua kuwa ana expose hilo kundi na kuthibitisha hoja namba 1-2 za Ben na Mamuya).
    • Pia anaonesha utiifu wake kwa ZZK/Masalia, pengine kutokana na kiapo kwa mganga (mchawi), pajo Ben anasema yeye Shonza alikataa (labda baadae alikwenda???)
  • Anadhamilia kujibu hoja (para 4-5) lakini anaishia kutokuzijibu (kwa kutozijua, kukurupuka, au uwezo mdogo wa kuelewa na kupangilia hoja)
  • Ana describe Ben na Mamuya badala ya kujibu hoja zao. Hapa inaonekana ama kuandaliwa majibu au kujibu akiwa na hasira!!!.
  • Badala ya kujibu hoja za Ben na Mamuya, Shonza anakwepa kwa kutoa maneno ambayo ama amekaririshwa au yamehaririwa na mtu au kikundi cha watu waliokuwa wamepanga jinsi ya kukwepa hoja au tuhuma za Ben na Mamuya.
    • Ukiangalia kwa undani na umakini, utagundua kuwa maneno au maelezo ya Shonza ni yale yale ya Mwapamba, ZZK, na ‘upande wa pili’ ambayo ni character assassination kwa viongozi wa juu wa CDM, hasa Dr. Slaa. Ama yaliandaliwa na kuhaririwa na mtu mmoja au kikundi (masalia) au ni ku-copy na ku-paste.
    • Majibu yake yanaonyesha uwezo mdogo wa kupambanua mambo au kukaririshwa maneno ya kusema.
  • Anakwepa hoja kwa kulalama kuwa amekuwa akionewa na Dr. Slaa.
    • Nadhani amekuwa (pia na Masalia wengine) akinyimwa forum za kujenga chama kwa sababu uongozi ulikwishajua mbinu zao za kujipanga kudhoofisha chama kama Ben na Mamuya wanavyoonesha.
Nawasilisha.
 
Wawasilishe mawazo yao ila bila kutoa maneno machafu
 
Tumesikia maneno mengi ya kashfa, dharau, na matusi kutoka kwa Mchange Juliana shoza, TUNTEMEKE na Mtela Mwampamba, wamefanya hivyo mara kadhaa kwenye fb wall zao.

Tumekerwa na mengi na tukavumilia mengi maana wengine tuliona kuna utoto na vurugu za maono kwenye mbongo zao.

Hili la SUMU sio swala la kuacha lipite hivihivi,hapa lazima wote walio singizia kuwa Zitto alitaka kuuwawa na sumu na kinara wa hilo akiwa Ben Saanane basi lazima wadhibitishe bila chembe ya shaka kuwa ni kweli mpango huo ulikwepo ili hatua stahiki zichuliwe, mahali pekee pa wao kudhibitisha madai yao si pengine ni mahakamani.

Kuwawa kwa Zitto ni serious allegation ambazo ni lazima zifanyiwe kazi ili kukitakasa chama na walio tuhumiwa kuwa walitaka kuuwa mwanachama mwenzao.

Kwa maono yangu.
Katika mambo ambayo lazima kuonyesha u-serious ni pamoja na hili. Tena bila ya kumuuonea mtu aibu. Ben Saanane anaweza kuanza mchakato wa mashtaka hayo kwa kuwasilisha malalamiko kwenye baraza la wazee la chama. Wahusika wakiitwa na kushindwa kuweka ushahidi suala hilo liende mahakamani kwa uamuzi zaidi, hivyohivyo kama Ben nae itadhihirika bila chembe ya shaka kuwa alikuwa na mpango wa kuuwa kwa sumu naye sheria ichukue mkondo wake.

Lazima tulazimishe kuhama kutoka kwenye siasa za kutungiana uwongo na kuviziana tuje kwenye siasa safi zenye mashiko.
 
Last edited by a moderator:
Lini Dr Slaa kafunga ndoa...katika dalili za unafiki ni kusema uongo.
 
ha ha ha leftovers --aka mabaki -- sasa mabaki ya nani mi sijui waulize wenyewe.

Eti mabaki ya watakatifu baada ya wale wateule wengine kupotoka!

Wapuuzi kweli hawa watoto, nimewadharau sana.........
 
naona mnatishiaana nyau.WEnzake wametangulia mahakamani

Hivi, pamoja na yote yaliyosemwa humu, hata aibu hamwoni? what's wrong with your brains? au ndio hiyo watu wanasema mmeshatekwa akili na mmegeuzwa misukule??
Mnataka tuamini kwamba mpaka sasa , kwa mfano wewe hujajua what is right and what is wrong na ufanye amends?

Kwa nini uendelee ku support a failed project? Aisee watu wengine wagumu!
 
Tumesikia maneno mengi ya kashfa, dharau, na matusi kutoka kwa Mchange Juliana shoza, TUNTEMEKE na Mtela Mwampamba, wamefanya hivyo mara kadhaa kwenye fb wall zao.

Tumekerwa na mengi na tukavumilia mengi maana wengine tuliona kuna utoto na vurugu za maono kwenye mbongo zao.

Hili la SUMU sio swala la kuacha lipite hivihivi,hapa lazima wote walio singizia kuwa Zitto alitaka kuuwawa na sumu na kinara wa hilo akiwa Ben Saanane basi lazima wadhibitishe bila chembe ya shaka kuwa ni kweli mpango huo ulikwepo ili hatua stahiki zichuliwe, mahali pekee pa wao kudhibitisha madai yao si pengine ni mahakamani.

Kuwawa kwa Zitto ni serious allegation ambazo ni lazima zifanyiwe kazi ili kukitakasa chama na walio tuhumiwa kuwa walitaka kuuwa mwanachama mwenzao.

Kwa maono yangu.
Katika mambo ambayo lazima kuonyesha u-serious ni pamoja na hili. Tena bila ya kumuuonea mtu aibu. Ben Saanane anaweza kuanza mchakato wa mashtaka hayo kwa kuwasilisha malalamiko kwenye baraza la wazee la chama. Wahusika wakiitwa na kushindwa kuweka ushahidi suala hilo liende mahakamani kwa uamuzi zaidi, hivyohivyo kama Ben nae itadhihirika bila chembe ya shaka kuwa alikuwa na mpango wa kuuwa kwa sumu naye sheria ichukue mkondo wake.

Lazima tulazimishe kuhama kutoka kwenye siasa za kutungiana uwongo na kuviziana tuje kwenye siasa safi zenye mashiko.
Ben Saanane lazima awe makini. Kwa jinsi Zitto alivyo lazima amtupie JUGNA JUHI
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hili kundi ni machokoraa na hawana adabu kabisa!!! Cha pili wote ni kundi la zitto na wanaweza kujipanga tu kusema kuwa Ben Saanane alikuwa na sumu. Ukiangalia maelezo yao ni kama vile wameandikiana ili yawe na ufanano fulani hivi. At the same time Zitto ni mjanja sana!!! Anatumia muda huu na watu hawa kuendeleza siasa zake za kukibomoa chama!!! Cha msingi wakienda mahakamani ni lazima wawe na evidence ya sumu!!! Walimrekodi Saanane akisema hayo na the so called sumu yake!!! Machokoraaa hawa wanatumika tu. Bora Ben Saanane ameungama!!

Hawa machokoraa ni waongo, tangu lini SUMU ya Panya ikatumika kuua binadamu, tena kwa kumuwekea kwenye chakula au kinywaji?? Kama ni kweli huyo Ben Saanane alijaribu kumuua Zitto kwa sumu ya panya basi ni kilaza wa milenia. kama alikosa Polonium si angetumia hata nyongo ya mamba tu...
 
Well said, hawa wanalo la kujibu, hata kama hawwatajibu hapa watajibu mbele ya Uongozi.
 
Du kaka uchambuzi wako nimeukubali. Inaonyeaha umepitia maelezo ya mmoja baada ya mwngine. Babako hajapata hasara katika kukusomesha. Hongera.
 
Lini Dr Slaa kafunga ndoa...katika dalili za unafiki ni kusema uongo.

Hivi Ritz and co. Haujui kuwa kwa Tanzania ukikaa na mwanamke kinyumba zaidi ya miezi sita tayari amekuwa ni mke wako! Mbona akili zenu ni kama za masalia. Nimetumia wingi kwa sababu sijui sasahivi nani yupo zamu kutoka lumumba
 
Hawa machokoraa ni waongo, tangu lini SUMU ya Panya ikatumika kuua binadamu, tena kwa kumuwekea kwenye chakula au kinywaji?? Kama ni kweli huyo Ben Saanane alijaribu kumuua Zitto kwa sumu ya panya basi ni kilaza wa milenia. kama alikosa Polonium si angetumia hata nyongo ya mamba tu...

Mkuu huu upuuzi wa hawa panya usiutilie maanani.
Kimsingi Ben ni mhuni tu na msaliti, ila amewazidi akili hawa panya wengine. Inawezekana na yeye ameaga kwao kama Zitto. Hahahhahaaa.
 
Back
Top Bottom