bless on
JF-Expert Member
- May 22, 2026
- 743
- 1,733
Sumu ya nyoka haikuumbwa kwa ajili ya kuwaumiza watu. Ni kimiminika cha thamani kubwa kwa nyoka ambacho hutumika kwa ajili ya kuishi. Nyoka hutegemea sumu hiyo kuwinda mawindo yao, na kwa kuwa kuitengeneza kunahitaji muda na nguvu nyingi, hawaitumii hovyo.
Nyoka anapomng'ata binadamu, mara nyingi huwa anajilinda, si kwa sababu anafurahia kufanya hivyo au anatamani kumdhuru mtu. Wakati mwingine anaweza hata kujizuia kabisa kuachia sumu yake na kutoa kile kinachoitwa kung'atwa bila sumu (dry bite). Hiyo huwa ni kama onyo tu.
Kwa mtazamo wa nyoka, kumng'ata binadamu mara nyingi ni hatua ya mwisho kabisa baada ya kuona hakuna njia nyingine ya kujilinda. Hata katika hali hiyo, wakati mwingine huamua kutopoteza sumu yake ya thamani na kuihifadhi kwa mambo muhimu zaidi, kama vile kukamata na kuua mawindo yake kwa ajili ya chakula.
Kwa nini unawachukia nyoka, ukweli ni kwamba nyoka hawakuchukii wewe ila wanakuogopa sana.
Kiroho nyoka maana yake ni akili kwenye biblia nyoka anatambulika kama shetani huu ni uongo biblia ni kitabu Cha mafumbo wanaitafsiri nyoka ni shetani wanasema hivyo kwa maslahi yao shetani sio kiumbe.
Je umewai kujiuliza kwenye logo za hospitali kwanini inawekwa mchoro wa nyoka??