Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Kilo ya sukari Tz imefika Tshs.5,000/, nadhani serikali inatakiwa itoe tamko kutupatia walaji mwongozo wa kufuata kutoka kwenye anguko hili.

Sababu tunayopewa ni dhaifu kwamba mashamba ya miwa yamefurika maji wakati TMA ilitoa tahadhari miezi 2 kabla ya mvua kushuka. Nadhani ni Tz pekee ambako mvua na jua ni laana isiyokoma kwa kilimo, umeme, maji, mifugo, uvuvi nikitaja kwa uchache.

Aidha, viwanda vya sukari vya Magereza vilivyojengwa kwa kasi ya mwanga hatujui vimefikia wapi baada ya kutumia fedha za umma kwenye ujenzi huo kama machinjio ya kisasa ya Vingunguti, Kibaha, Simiyu na Manyara vilivyobaki kuwa makumbusho ndani ya nchi ambayo ni ya pili kwa idadi kubwa ya mifugo barani Afrika?

Tz sukari haijawahi kushuka kwa miaka 23 mfululizo tangu Julai 2001 licha ya mashamba ya miwa kuongezeka na viwanda vipya kujengwa Morogoro na Bagamoyo pamoja na uingizaji wa sukari ya nje ya nchi.

Tz sukari ni miongoni mwa bidhaa na huduma ambavyo vimekuwa vya kidemokrasia vikiwemo Korosho, Mafuta ya mitambo, Mafuta ya kula, Katani, Umeme na Maji.

Nchi kubwa, hali ya hewa ya kitropiki, mitambo ipo, rasilimaliwatu rahisi wapo, soko la ndani lipo lakini tumeshindwa hata kwenda kujifunza Uganda tu hapo namna ya kuendesha sekta ya sukari.

Ni kama vifuatavyo vyote 4 vimefeli jumla kwenye sekta ya sukari:-

1. Sheria ya Taifa ya Sukari 2001 (National Sugar Act 2001).

2. Taasisi ya Sukari Tz (National Sugar Institute).

3. Shirika la Maendeleo ya Sukari (Sugar Development Corporation SUDECO).

4. Makampuni ya Sukari (Sugar Factories).

NB.
1. Tz ina makampuni 5 ya sukari kwenye mikoa 4.

2. Kenya ina makampuni 16 ya sukari.

3. Uganda ina makampuni 14 ya sukari.

4. Zambia ina kiwanda cha sukari kikubwa kuliko vyote barani Afrika tangu 1964.

Uganda ina sukari kuzidi mahitaji ya ndani na hawajui wapeleke wapi ziada hadi waliwahi kuiomba Tz ichukuwe sukari yao hata kwa mkopo ili maghala yao yawe wazi kupokea uzalishaji mpya maana hawawezi kumwaga ziada ziwani.

Sasa mapapa wa biashara ya sukari wanapiga jaramba ili serikali iruhusu uagizaji toka nje ya jamhuri. Nadhani kwa spirit ya EAC serikali ichukuwe sukari ya Uganda ambayo nayo pia itapunguza bei kwa sababu ni jirani nasi kuliko kutoa sukari ng'ambo ya bahari. Let us think over and handle this matter strategically, progressively and proactively.

Bei ya sukari ikipanda vifuatavyo navyo vinapanda kwa sababu kuna aina nyingi za sukari zinazotengeneza bidhaa mbalimbali:-

1. Bei ya Soda kufuatia kupanda bei ya sukari.

2. Bei ya vitafunwa (mikate, maandazi, vitumbua, keki nk) kufuatia kupanda bei ya sukari.

3. Bei za madawa ya syrups kufuatia kupanda bei ya sukari.

4. Bei za sharubati kufuatia kupanda bei ya sukari.

5. Bei za sweets kufuatia kupanda bei ya sukari.

6. Bei ya wanzuki (inayotumia sukariguru) kufuatia kupanda bei ya sukari. Whatnot?

NB.
Miili yetu inapokea sukari kwa 99% ya vitu tunavyokula na kunywa hivyo sukari ni maisha (Sugar is Life)

Sir Richard Gordon Turnbull GCMG hakukosea kutumia viboko kutawala Tanganyika.
 
As of jana Mwanza sukari bei ya jumla kwa wale big suppliers ni 163,000 for 50kg na hapo inaemdelea kupanda wana estimate itafika 180k.
Hapo hapo kuna wandewa wanachukua sukar burundi, wanairebag kwa mifuko ya kagera sugar inauzwa tena
Tutafrahi!
 
Ndiyo shida ya kuachia Kila jambo secta binafsi.
Kweli mkuu, wanaweza hata kuhonga viwanda visizalishe ili wasipate ushindani wa bei kwa shehena zao za kutoka nje ya nchi.

Dunia inakoelekea kuna dalili zote kuwa Marxism inarudi. Tayari BRICS (wafuasi wa Marxism) pekee imeishateka 17.% ya eneo la sayari ambapo wanachama waanzilishi pekee wana soko la walaji lenye ukubwa wa watu 3.27 bl sawa na 41.13% ya watu wa dunia. BRICS inatarajia kumiliki uchumi wa dunia ifikapo 2050 miaka 26 tu ijayo.
 
As of jana Mwanza sukari bei ya jumla kwa wale big suppliers ni 163,000 for 50kg na hapo inaemdelea kupanda wana estimate itafika 180k.
Hapo hapo kuna wandewa wanachukua sukar burundi, wanairebag kwa mifuko ya kagera sugar inauzwa tena
Tutafrahi!
Kama hali ndo hii kwisha kazi,,,mda mwingine nataka kujuta kwa nn nimezaliwa Tanzania Ila fresh maana unyonyaji na ukatili wa aina zote tunaongoza. Blah blah kibaooo.
 
As of jana Mwanza sukari bei ya jumla kwa wale big suppliers ni 163,000 for 50kg na hapo inaemdelea kupanda wana estimate itafika 180k.
Hapo hapo kuna wandewa wanachukua sukar burundi, wanairebag kwa mifuko ya kagera sugar inauzwa tena
Tutafrahi!
What is this in Lower Middle Income Economy!? Alafu eti wanataka tujadili dira mpya ya taifa 2050!?

Huo mchezo mchafu wa ku-rebag products wanaufanya kampuni ya maziwa ya Tanga Fresh wakitumia maziwa ya ASAS, nyumbani kwangu nimeweka ban kutumia Tanga Fresh until further notice.
 
Kilo ya sukari Tz imefika Tshs.5,000/, nadhani serikali inatakiwa itoe tamko kutupatia walaji mwongozo wa kipi kifanyike.

Sababu tunayopewa ni dhaifu kwamba mashamba ya miwa yamefurika maji wakati TMA ilitoa tahadhari miezi 2 kabla ya mvua kushuka. Nadhani ni Tz pekee ambako mvua na jua ni laana isiyokoma kwa kilimo, umeme, maji, mifugo, uvuvi nikitaja kwa uchache.

Aidha, viwanda vya sukari vya Magereza vilivyojengwa kwa kasi ya mwanga hatujui vimefikia wapi baada ya kutumia fedha za umma kwenye ujenzi huo kama machinjio ya kisasa ya Vingunguti, Kibaha, Simiyu na Manyara?

Tz sukari haijawahi kushuka kwa miaka 23 mfululizo tangu Julai 2001 licha ya mashamba ya miwa kuongezeka na viwanda vipya kujengwa Morogoro na Bagamoyo pamoja na uingizaji wa sukari ya nje ya nchi.

Tz sukari ni miongoni mwa bidhaa na huduma ambavyo vimekuwa vya kidemokrasia vikiwemo Korosho, Mafuta ya mitambo, Mafuta ya kula, Katani, Umeme na Maji.

Nchi kubwa, hali ya hewa ya kitropiki, mitambo ipo, rasilimaliwatu rahisi wapo, soko la ndani lipo lakini tumeshindwa hata kwenda kujifunza Uganda tu hapo namna ya kuendesha sekta ya sukari.

Uganda ina sukari kuzidi mahitaji ya ndani na hawajui wapeleke wapi ziada hadi waliwahi kuiomba Tz ichukuwe sukari yao hata kwa mkopo ili maghala yao yawe wazi kupokea uzalishaji mpya maana hawawezi kumwaga ziada ziwani.

Sasa mapapa wa biashara ya sukari wanapiga jaramba ili serikali iruhusu uagizaji toka nje ya jamhuri. Nadhani kwa spirit ya EAC serikali ichukuwe sukari ya Uganda ambayo nayo pia itapunguza bei kwa sababu ni jirani nasi kuliko kutoa sukari ng'ambo ya bahari. Let us think over and handle this matter strategically, progressively and proactively.

Sir Richard Gordon Turnbull GCMG hakukosea kutumia viboko kutawala Tanganyika.
Safi sana professor Janabi kwa kuishauri na kuishinikiza Serikali kuongeza bei ya sukari na mafuta ya kula. Usiishie hapo hakikisha nyama inapanda hadi elfu 30.

Haiwezekani watu kufa vifo vya kizembezembe tu kwa kula hovyohovyo unhealthy foods.

Janabi the national treasure.

Victoire
 
As of jana Mwanza sukari bei ya jumla kwa wale big suppliers ni 163,000 for 50kg na hapo inaemdelea kupanda wana estimate itafika 180k.
Hapo hapo kuna wandewa wanachukua sukar burundi, wanairebag kwa mifuko ya kagera sugar inauzwa tena
Tutafrahi!
Kwahiyo wanapata super profit ya 1740/ @kg
 
Safi sana professor Janabi kwa kuishauri na kuishinikiza Serikali kuongeza bei ya sukari na mafuta ya kula. Usiishie hapo hakikisha nyama inapanda hadi elfu 30.

Haiwezekani watu kufa vifo vya kizembezembe tu kwa kula hovyohovyo unhealthy foods.

Janabi the national treasure.

Victoire
Ila bia ishuke bei siyo? Madawa ya kulevya je Janabi anasemaje au haruhusiwi kugusa huko.
 
Back
Top Bottom