Serikali yatangaza Amri ya Bei Elekezi za Sukari Tanzania Bara

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
1706072885886.png

1706072942386.png

Kufuatia malalamiko ya Wananchi juu ya kupanda kwa gharama za Sukari, Serikali imetangaza Amri ya Bei Elekezi iliyoanza kutumika Januari 23, 2024 katika Mikoa yote ya Tanzania Bara kwa lengo la kudhibiti Bei holela za Bidhaa hiyo

Kwa mujibu wa Tangazo la Serikali, Amri hiyo imesema Mtu yeyote anayeuza Sukari kinyume na Bei Elekezi zilizoainishwa atakuwa ametenda Kosa na akitiwa hatiani atawajibika kwa adhabu iliyoainishwa katika masharti ya Sheria ya Tasnia ya Sukari

Bei Elekezi za Rejareja kwa Kilo 1 Sukari ziko kama ifuatavyo: Dar, Morogoro, Pwani Tsh. 2,700 - 3,000, Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe Tsh. 2,700 -3000, Dodoma, Singida, Tabora Tsh. 2,800 - 3,000, Lindi Mtwara, Ruvuma Tsh. 2,900 - 3,200

Mikoa ya Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara Tsh. 2,800 - 3,000, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara Tsh. 2,700 - 3,000 na Kagera, Kigoma, Katavi, Rukwa Tsh. 2,800 - 3,200

===========For English Audience Only=============​

The Tanzanian government has announced a directive on Sugar Price Controls for Mainland Tanzania in response to public complaints about the rising costs of sugar. The price control directive came into effect on January 23, 2024, across all regions of Mainland Tanzania with the aim of regulating the arbitrary pricing of this commodity.

According to the government announcement, anyone selling sugar above the specified price controls will be committing an offense. If found guilty, they will be liable for penalties as stipulated in the Sugar Industry Act.

The retail price controls for 1 kilogram of sugar are as follows: In Dar es Salaam, Morogoro, and Pwani regions, the price ranges from Tsh. 2,700 to 3,000. In Iringa, Mbeya, Songwe, and Njombe regions, the price is between Tsh. 2,700 and 3,000. In Dodoma, Singida, and Tabora regions, the price is between Tsh. 2,800 and 3,000. In Lindi, Mtwara, and Ruvuma regions, the price is between Tsh. 2,900 and 3,200.

For the regions of Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, and Mara, the price ranges from Tsh. 2,800 to 3,000. In Tanga, Kilimanjaro, Arusha, and Manyara regions, the price is between Tsh. 2,700 and 3,000. Lastly, in Kagera, Kigoma, Katavi, and Rukwa regions, the price ranges from Tsh. 2,800 to 3,200.
 

Attachments

  • 1706072824921.png
    1706072824921.png
    66.4 KB · Views: 12
  • 1706072834530.png
    1706072834530.png
    120.5 KB · Views: 13
Kama umesoma hili tangazo na akili yako ikakuambia ni jambo linawezekana basi ujue una kamtindio ka ubongo
Bei za soko katika dunia ya kibepari zinaamuliwa automatically na demand and supply.
Hili tangazo litaifanya sukari isionekane kabisa na ukiipata bei itakuwa juu kuliko sasa
 
Ikiadimika serikali inatakiwa iwachukulie hatua wanaoficha sukari.
Hawa watu sio wakuwachekea hata kidogo. Ukiona hadi awamu hii inafikia hatua hii ujue uhuni umezidi.

Nakuelewa sana Mkuu, mtu aliyekua anaziweza hizi mambo ni huyo kwenye avatar Yako.

Unakumbuka sakata la mafuta ya kula, na sukari enzi zake?

Hapa hii amri inaweza kupuuzwa na kisitokee chochote.

Binafsi naona hili ni kama tangazo la watu kulinda nafasi zao tu za ajira. Waonekane wamechukua hatua. Sidhani litakua na nguvu.

Litapelekea sukari kupotea kabisa mtaani.
 
Waende kiwandani wawaambie wauze sukari kwa bei elekezi na iwe toshelezi, kwann sukari inapanda bei, mawakala wameweka oda kiwandani lkn bidhaa hakuna, ikipatikana anapigiwa cm wakala mmoja sukali ipo lkn kwa shilingi kadhaa bei sio ile halisi anaongezewa kidogo hata hivyo anapata pungufu ya idadi aliotaka mfano amehitaji tani 60 analetewa tani 40 wakati huo huyu wakala ana wateja zaid ya 20 wanataka sukali, ikifika anaiweka ndani anawapigia wateja sukari imefika lkn kwa bei fulania wale wanaenda kununua hapo inauzwa kwa jumla mtu anachukua mifuko 100 nk huyu nae anakwenda kuwauzi wale wa mfuko moja mwenye kuitaji mifuko kumi kwa kuongoza zaid mpka ikufikie ww , kaa kwa kutulia waende kiwandani wakatatue tatizo kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa watu wanatuona mazuzu ebu jiulize kwanini wafanyabiashara wasipandishe bei siku za nyuma waje kupandisha leo! Ni dhahiri kuna tatizo katika upatikanaji wa bidhaa ndiyo maana bei imepanda sasa katika hali ya kawaida mfanyabiashara hawezi kununua bidhaa kwa bei ya juu halafu auze kwa bei ya chini.
Wao badala ya kuonea watu ili kujiosha waruhusu wafanyabiashara walete sukari kutoka nje ya nchi kufidia upungufu uliopo, hii ya kuwapa wenye viwanda pekee vibali vya kuagiza sukari toka nje ni kuongeza urasimu na bei inaweza isishuke.
 
Back
Top Bottom