Tutafute chanzo mbadala cha sukari ya miwa

mpasta

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
917
1,997
Sukari mitaani Hali mbaya imefika mpaka bei ya TZS 5,000/= kwa kilo moja.

Mwanzoni tulidhani kupanuliwa kwa kiwanda Cha Kilombero, kuanzishwa kwa viwanda vipya vya BAGAMOYO SUGAR, NSSF-MKULAZI na LAKE AGRO-Rufiji kuyamaliza tatizo la sukari nchini, lakini mabadiliko ya hali ya hewa Duniani yatupe SoMo kama nchi.

Ni wakati Sasa muafaka wa kutafuta vyanzo vingine vya sukari, na tuache utegemezi wa chanzo kimoja tu Cha sukari kutoka kwenye zao la MIWA.

MAREKANI inakisiwa 55-60% ya sukari yake inatokana na zao la "SUGAR BEET" na sio MIWA.

Faida za "SUGAR BEET" unaweza kuvuna mara mbili kwa mwaka, linakomaa ndani ya miezi 5-6 tofauti na MIWA inayokaa shambani miezi 12-14. Lakini pia "SUGAR BEET" inatumiwa maji na mbolea chache kwa chini ya 30% ya gharama za MIWA.

Wizara ya Kilimo ianze Sasa kufanya tafiti za zao la SUGAR BEET, nchi nyingine za Kiafrika kama SUDANI, KENYA, SOUTH AFRICA, na hata bara la Asia kama INDIA wameanza kufanya tafiti za mbegu za SUGAR BEET zinazofaa kwa mazingira ya joto la KITROPIKI.

Nawasilisha wazo langu.
 
Wazo zuri,
Je hiyo Sugar Beet inafaa kulimwa mazingira gani?
Zamani ilikuwa inajulikana inastawi kwenye Temperate Zones lakini Sasa kuna mbegu zimefanyiwa Utafiti zinastawi maeneo ya KITROPIKI, ukienda KENYA maeneo ya Nyandarua County wameanza kulima na kiwanda cha kuchakata sukari ya SUGAR BEET kinajengwa maeneo ya KIPIPIRI Constituency...
Hivyo ZIPO mbegu Special kwa nchi za KITROPIKI
 
Yaani mpaka haitumiki bas ukute returns yake compared to cost of production ni lower.
 
soma uzi wangu kuhusu
Ahsante ngoja nijisomee niongezs maarifa
 
Yaani mpaka haitumiki bas ukute returns yake compared to cost of production ni lower.
Nadhani Exposure yetu na mawazo mgando, INDIA na BRAZIL ni wazalishaji wakubwa wa Sukari ya Miwa lakini nao sasa wameanza kilimo cha SUGAR BEET ..., mabadiliko ya hali ya hewa yata tuumbua sana ..sasa na siku zijazo
 
Tuna mabonde kibao ya kufaa kulima miwa. Magufuli alithubutu kumpa Bakhresa bonde alime miwa. Ni kazi ndogo tu kwa hawa wa sasa kuiga kwa kuwapa wengine mabonde ili tuzidi kuzalisha sukari.
 
Back
Top Bottom