Suala la Simba kuzindua jezi katika kilele cha Mlima Kilimanjaro sio suala la kimichezo ila ni la kiroho litakaloathiri sana siasa za Taifa letu

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,894
155,913
Wasalaam.
Wanasema kila jambo fulani liwe zuri au liwe baya basi hutanguliza alama, dalili, viasharia na taarifa fulani za kimafumbo ambazo ni lazima watu wazima wakae chini, wapasue vichwa vyao kuweza kuzi uncode hizo secret codes.

Mwaka 1961 Nyirenda alipandisha bendera ya Tanganyika na mwenge wa Uhuru kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro na kupelekea kilele hicho kuitwa Uhuru Peak.

Lile lilikuwa na sura ya kusherehesha sherehe za uhuru. Tulipandisha mwenge ili umulike mpaka nje ya mipaka yetu. Tulipandisha mwenge Mlima Kilimanjaro ili ulete amani palipo na chuki, ulete tumaini pasipo na tumaini. Jiulize mwenge unawezaje kuleta amani na tumaini?

Kumbe kwenye ulimwengu wa kiroho mwenge ulikuwa na lengo la kupumbaza na kufubaza fiķra za wengi.

Wakikandamizwa waone sawa tu, wakiburuzwa na kuonewa waone sawa tu, yaani wayapuuzie matatizo yao. Kwa njia hiyo tu ndio amani na utulivu vitapatikana.

Mwaka 1964 tulipoungana na Zanzibar hatukupandisha mwenge wala bendera, Tanganyika ikafa kimyakimya.

Tumepita kwenye misukosuko ya kila namna, furaha na vicheko hatimaye umefika mwaka 2023.

Simba ambaye ni mfalme wa nyika kapanda kwenye kilele. Kaenda kuweka bendera yake nyekundu kule kileleni.

Nyirenda mwaka 1961 aliweka bendera yenye rangi ya kijani, njano na nyeusi, utawala wa twiga mnyama mrembo lakini goigoi akatawala kuanzia hapo. Wote tumesguhudia jinsi taifa letu lilivyo na watu wavivu na goigoi, hadi wawekezaji wanasema hawataki kufanya kazi na Watanzania kwani hawataki kufànya kazi kwa bidii ila wanataka wakuibie.

Kwa ujio huu mpya kiroho, uelekeo wa kitaifa unabadilika. Spirit ya mapàmbano imetamalaki.

Sasa pale kileleni ni pekundu na pana Simba mfalme wa nyika. Tutaziona rangi zote.

Mabadiliko makubwa sana yanakuja kwenye siasa zetu na uongozi kwa ujumla, mabadiliko haya mtaanza kuyaona siku sio nyingi.

Wenye macho ya rohoni tumeona.
Gwappo Mwakatobe , Mshana Jr, Pascal Mayalla , Rakims
 
La Simba SC sijui ila la Mwenge huwa naamini hivo! Huwa nashangazwa sana eti VIONGOZI wanakula kiapo mbele ya torch ... 😁😁😁
Na ukishaingia anga hizo unakuwa ..kama mashabiki wa Yañga ukimwondoa Mzee Manara na Kikwete!
Umesikia huko kuna mzungu kapewa heka million sita, hivi Usalama wa Taifa ndio wasaidizi wa mama chausiku katika kuuza ardhi ya Tanganyika?
 
Umesikia huko kuna mzungu kapewa heka million sita, hivi Usalama wa Taifa ndio wasaidizi wa mama chausiku katika kuuza ardhi ya Tanganyika?
Mwaka 2015, Friedkin Conversation Trust iliipa Tanzania Tsh Bilioni 231.55 ili kulinda mazingira na kukuza utalii.

Kazi zao nchini Tanzania
zinatajwa kuanza miaka ya 1989 na Thomas Friedkin, Baba mzazi wa Dan Friedkin aliyefariki Machi 14, 2017 akiwa na umri wa miaka 81.
 
Maka Samia huyo, The Mother of Modern Tanzania, anawageuza watu kuwa waganga wa kienyeji kwa kasi yake ya kimaendeleo, kwa kasi yake ya maono ya kiuchumi, kwa mbinu zake murua za kuwapiga 'bani' wezi.

Go Mama Samia, gooooooo!!!
 
Nimesoma nimeelewa ila tusubiri yajayo yatakuwwa mazuri kwa taifa letu.
Mama anaona mbali na anatupenda na kutulinda kama Simba anavyolinda ufalme wake msituni.
YAJAYO NI MAZURI TUSUBIRI MATOKEO.
 
Nimesoma nimeelewa ila tusubiri yajayo yatakuwwa mazuri kwa taifa letu.
Mama anaona mbali na anatupenda na kutulinda kama Simba anavyolinda ufalme wake msituni.
YAJAYO NI MAZURI TUSUBIRI MATOKEO.
Hayatakuja kwa njia rahisi, lazima tuparuzane na kukwaruzana sana, huenda na bi mdashi akavurushwa
 
Back
Top Bottom