Star TV mbona mnakatisha matangazo ya BBC Dira ya Dunia?

Hivi wewe ndio wa kushangaa kwanini hivyo, mbona huku shangaa msimu wa uchaguzi unashangaa leo.
Taratibu tu, mwishowe wote tutaongea lugha moja. Hakuna binadamu anayefurahia kubanwa kwa mambo ya kawaida tu Kama kupata taarifa
 
Tatizo ni hiyo report ambayo JIWE na WACHUMIA tumbo hawataki kuisikia....Wakikata matangazo nenda youtube swahili utaipata live...Mimi walivyokata nikaenda youtube kuiona hiyo report ya haki za binadamu.
Report ya Uchaguzi mkuu wa Marekani wametoa?
 
Star tv hawaelewi kama matangazo ya BBC ndo yanawapa Sponsor we ngoja wanapata matangazo ya waganga tu
Yani Star tv kwa sasa wanatia huruma tangu walipoanza kuchagua habari za kutangaza imekuwa kama TBC tu pia usaliti walioufany kampeni za 2015
 
Report ya uchaguzi mkuu wa Marekani wametoa?
Sina uhakika kama imetoka ila taarifa zote za Shishi Trump na Joe Biden huwa BBC swahili wanaweka!! Trump kula za uso Pennsylvania niliona Star TV.

Startv huwa wanakata habari ambazo CCM na genge la wachumia tumbo ambazo hawataki kusikia.
 
Kama kuna habari mnataka isiwafikie Watanzania ni bora kipindi kizima mkaachana nacho badala ya kuonyesha zile mnazozipenda na kuzima tusione zile msizozipenda....
Hangaikeni na malalamiko yenu, anga ya Tanzania ipo salama, hakuna ndege vita, upuuzi, hata uzandiki utaopenyeza anga ya Tanzania.
 
Mabibi na mabwana bado mawazo ya kikoloni hayataki tusikie lolote kuhusiana na ghiliba za uchaguzi 2020.

Leo tena BBC Dira ya Dunia inayorushwa pia na star TV walikuwa na habari kuhusiana na Amnesty International ukiukwaji haki kwenye uchaguzi 2020.

Ilipofikiwa tu habari hiyo, Star TV kama ilivyo ada yao wakakata matangazo ya moja kwa moja tokea BBC na kuweka matangazo yao ya biashara.

Watu kama hawa ni wasaliti wa wazi kwa taifa. Taifa siyo viongozi bali taifa ni wananchi. Wamechagua kujikomba kwa watawala. Siku moja tutaulizana na kila mmoja atakuwapo ku account kuwa alichangia nini au alichangia vipi?

Si haba kupendekeza kwa BBC kuwazuia Star TV ku-relay matangazo yao kama huu ndiyo mwendelezo wao wa news sensor-ship wanaoendelea tangia kipindi kuelekea kampeni.

Vitendo vyao vyenye kutaka kutuchagulia sisi nini tuone au kusikia hatuviafiki. Uhuni huo hauna nafasi katika jamii yoyote iliyostaarabika.

Kama nia yao ni kupendekeza mapambio ya kusifu bora wawe wanajiunga na TBC kwani hao ndiyo size yao.

Waachane tu na BBC kwani hawa utu tunaojifanya sisi kuujua wao wanaujua zaidi.

Inashangaza sana!
 
Mabibi na mabwana bado mawazo ya kikoloni hayataki tusikie lolote kuhusiana na ghiliba za uchaguzi 2020...
Kwahiyo hao akina Amnesty International ndiyo Mungu Mtu wako, ambapo wakisema Kitu hata cha Uwongo kuihusu Tanzania yetu utawaamini tu?
 
Ulitaka hizo habari za uchochezi
Sikuwahi kufikiria kama Tanzania itafika kwenye mawazo ya watu kama hawa. Wewe huna kichwa cha kupima mwenyewe ndugu unataka serikali ikufanyie filter?

Mwisho watasema hamna CNN na BBC angalieni TBC!
 
Kama Star TV hawataki kuonyesha habari za BBC Swahili tutakuwa tunaziangalia kwenye yutub au tutakuwa tunasubiri KTN ya Kenya huwa inarusha saa 5
 
126146938_3402095063172765_1400351967337563643_n.jpg


Kwa sasa hatuhitaji kuwa na vyombo vya habari, tuwe na vyombo vya muziki na burudani tu.
 
Back
Top Bottom