Star tv yasimamisha baadhi ya vipindi

Kichuchunge

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
335
885
Uongozi wa kituo cha televisheni cha Star Tv.chenye maskani yake jijini Mwanza,kimetangaza kusitisha uzalishaji wa vipindi vyote vya ndani kuanzia leo Januari 18,isipokuwa taarifa za Habari,BBC Swahili,na vipindi vingine vilivyolipiwa na uandaaji wake hufanyika nje.

Taarifa iliyotolewa kwa wafanyakazi wote wa kituo hicho leo Januari 18,katika kikao cha dharura,imesema uongozi wa kampuni umefikia uamuzi huo ili kupisha maboresho ya vipindi vilivyopo,na vingine vipya vilivyo mbioni kuanzishwa,na muda wote wa maboresho (Haujatajwa) wafanyakazi na wahusika wa uzalishaji vipindi watapaswa kukaa makwao kwani hakuna kazi tena.

Kitendo cha Kampuni kusitisha matangazo kimekuja katikati ya vuguvugu kali la wafanyakazi kudai madeni yao ya muda mrefu ambayo kampuni mara zote imedai kuwa haina pesa na haiingizi pesa,vuguvugu lililopelekea mgomo takribani juma zima kuanzia Januari 2.

Hatua ya kusitishwa kwa vipindi itawaathiri waandaji wa vipindi mbalimbali pamoja na wasanii wa vichekesho ambao wote watatakiwa kupumzika nyumbani hadi pale taarifa zaidi zitakapotolewa na uongozi wa kampuni hiyo.

Hata hivyo taarifa kutoka kwa wafanyakazi wa Star Tv zinasema kuwa,licha ya tangazo la kusitisha,uongozi haukugusia kabisa suala la malipo ya wafanyakazi ambalo ndio agenda kuu kwa sasa,na hata alipoulizwa katia kikao,Mharirir wa Star Tv Dotto Shashi kuhusu kusitishwa kwa vipindi na hatima ya madeni ya wafanyakazi,alikosa majibu ya kuridhisha na kusema kuwa mtu anaeweweza kujibu suala hilo ni mtu wa utawala,na si yeye,hatua ambayo iliwalazimu wafanyakazi kuomba kukutana na mkurugenzi wa kampuni hiyo kwa sasa (Maana wanabadilika kila muda) Samwel Nyalla ili awaeleze hatima yao.

Wafuatiliaji wa mambo wamedai huenda hatua hiyo imefikiwa na kampuni kama mbinu ya kunyong’onyeza vuguvugu la madai ya wafanyakazi,na kwamba huenda vipindi vitaanza kurudi kimoja kimoja kwa masharti kuwa mzalisha/mtayalishaji atakaetaka kurejea kwenye kipindi chake,akubali kufanya kazi kwa mkopo bila kuisumbua kampuni kuhusu malipo,jambo ambalo limekuwa mwiba kwa kampuni muda mrefu sasa, na ndio sababu vipindi vyote vinavyoingiza pesa ikiwemo Habari,BBC na vipindi vya dini havitoathirika kwa sababu ya mikataba ya wateja na kwamba kampuni haiwezi kukubali kurudisha fedha kwa mteja.

Nchini Tanzania,wandishi wa habari na hasa watayarishaji wa vipindi mbalimbali wamekuwa wakijapatia pesa za kujikimu kutoka kwa adau wa masuala mbalimbali ambao wanataka kutumia vyombo vya habari kutangaza shughuli zao bila malipo ya kununua muda wa hewani na kupitia njia hiyo ya mkato,hali inayotajwa kuwa huenda watayarishaji engi wa vipindi watasalimu amri ya kurejea kazini na kufanya kazi bila kudai.
madeni yao kwa kutafuta namna ya kujilipa.
 
Kuna kamanda namuona anatangaza habari hapo kila siku nakumbuka jamaa anafanya kazi bila kulipwa halafu yupo serius kweli. anyways futuhi watubakishie.
 
Back
Top Bottom