BBC swahili, Dira ya Dunia imepoteza mvuto!

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
10,052
24,442
Kwa wafuatiliaji wa Bbc swahili dira ya dunia, kupitia matangazo yanayorushwa saa tatu usiku kuanzia jumatatu hadi ijumaa kupitia Star tv watakubaliana nami kuwa urushaji wa taarifa umekosa mvuto!

Tokea Charles Hilary aondoke, huku akifuata Zuhura Yunus na hatimae Salim Kikeke, Mariam Omary pamoja na Saluma Kassim utangazaji wa taarifa zake hauna mvuto kabisa!

Watangazaji wanaotangaza hivi sasa hawavutii kuwasikiliza na hata taarifa zinazotangazwa mara nyingi ni kutoka Kenya, na hata kwenye mijadala mara nyingi wakenya ndio wanakuwa wanashirikishwa zaidi, tofauti na hapo awali ambapo kulikuwa na balance!

Hivi sasa BBC haina tofauti na KBC ama Citizen Tv za Kenya!
 
Watangazaji wanaotangaza hivi sasa hawavutii kuwasikiliza na hata taarifa zinazotangazwa mara nyingi ni kutoka Kenya,
Head of BBC Swahili kwa sasa ni anatokea KENYA sio Tanzania kwa hio wamehamishia huko anaitwa Rachel Akidi Okwir, Head of East Africa Languages, is based in Nairobi, Kenya
✍️
 
Walikuja kuwekeza kwenu mkawatimua, wameenda kwa majirani zenu na wanapewa kipaumbele mnaanza nongwa!
 
Back
Top Bottom