Spika Tulia Ackson ampa Onyo kali Mwita Waitara kutorudia kudharau madaraka ya Spika

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,495
7,993
Leo Juni 14, 2022 amesema Mwita Waitara ameshindwa kuthibitisha watu kuuawa jimboni kwake pia alibeza maamuzi ya Spika alipoipa Serikali siku 90 kuchunguza.

Waitara amekiuka kanuni ya 5 ya Bunge inayomtaka kukata rufaa kwa maandishi endapo hataridhika na maamuzi ya Spika badala yake akaenda kwenye vyombo vya habari.

Spika amesema kwa Mwita kusema Spika alikuwa Naibu Mwanasheria mkuu wa Serikali hawezi kujua sheria kuliko yeye.

Spika amesema adhabu iko wazi kanuni ya 84 imezungumzia utovu mkubwa lakini ameamua kumpa Onyo kali na Asirudie tena.

WAITARA.jpg

Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara​
 
Mbunge wa Tarime Mwita Waitara amepewa Onyo kali na Spika Tulia kwa kosa la kukidharau kiti cha Spika

Source Star tv bungeni
 
Mbunge wa Tarime Mwita Waitara amepewa Onyo kali na Spika Tulia kwa kosa la kukidharau kiti cha Spika

Source Star tv bungeni
Dikteita kutoka kwa Magufuli, sijui alimuibua wapi na kwa mausiano yapi katika wanawake wote intelligent Tanzania.
 
wabungepiic.jpg

Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara amepewa onyo na Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson na kutakiwa kutodharau maamuzi ya Spika baada ya kuvunja Kanuni ya 84 ya Bunge.

Spika Tulia amechukua hatua hiyo leo Juni 14, 2022 baada ya Waitara kutofuata utaratibu wa kuwasilisha maoni yake ya kutoridhishwa na maamuzi ya Spika wa Bunge, badala yake akaenda katika vyombo vya habari na kutoa kauli za kudhalilisha mwenendo wa Bunge.

Waitara alitakiwa kupeleka ushahidi wa tuhuma za wananchi kuuawa kwa risasi alizozitoa ndani ya Bunge, baadaye Spika aliagiza Serikali ichunguze suala hilo kwa miezi mitatu.
 
Spika amechemsha kwa hili huyu mvimba macho alikuwa sahihi,serengeti ya derikali then serikali ichunguze serengeti.
 
Amesema Spika, kwa alichofanya Waitara anahitaji afya ya akili yaani..!
 
Mh Lema aliwahi kuwatahadharisha wana CCM.

Alisema kuwa utawala wa ccm ukimaliza kuwabagua wapinzani basi wataanza kubaguana wao kwa wao wana CCM.

Leo hii Waitara ameanza kuyakumbuma maneno ya mh Lema pale mjengoni.

Hakika ccm itabakia kuwa ileile kama alivyo imba marehemu Komba.
 
Leo Juni 14, 2022 amesema Mwita Waitara ameshindwa kuthibitisha watu kuuawa jimboni kwake pia alibeza maamuzi ya Spika alipoipa Serikali siku 90 kuchunguza...
Laana ya chadema inamuandama huyu.

Waliingia chadema akiwa lofa kabisa Afu akanunuliwa na kuanza kutukana. Mpuuzi huyu.

Labda yule chizi afufuke vinginevyo chapati ubunge tena
 
Leo Juni 14, 2022 amesema Mwita Waitara ameshindwa kuthibitisha watu kuuawa jimboni kwake pia alibeza maamuzi ya Spika alipoipa Serikali siku 90 kuchunguza...
Walibebwa na mwenda zake sasa mambo maji ya shingo
 
Maandiko Matakatifu yameielezea laana ya Usaliti kwa ukubwa wake , unaweza kufanya Usaliti wa kijinga leo kwa sababu ya kufurahisha nafsi yako au kuwafurahisha waliokutuma lakini madhara yake yatawapata hadi vitukuu , laana ya Usaliti wako inakikumba hata kizazi chako cha nne .

Mwita Waitara aliyeondoka kwa mbwembwe Chadema hivi sasa amekalia kuti kavu ccm na huenda akatimuliwa wakati wowote kuanzia sasa kwa tuhuma za kukiaibisha chama chake baada ya kuweka wazi mauaji ya wapiga kura wa jimbo lake , Jambo ambalo ni kinyume cha utaratibu wa ccm , utaratibu wa ccm uliozoeleka siku zote ni ule anaoenda nao Waziri Mkuu wa kuficha ukweli .

Tayari Spika wa Bunge amempa onyo kali Waitara kwa kauli yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari , KWAMBA SERIKALI HAIWEZI KUJICHUNGUZA YENYEWE , baada ya Spika kuunda Tume ya kuchunguza Tuhuma za Malalamiko yake ya Raia kuuawa huko Tarime .
 
Leo Juni 14, 2022 amesema Mwita Waitara ameshindwa kuthibitisha watu kuuawa jimboni kwake pia alibeza maamuzi ya Spika alipoipa Serikali siku 90 kuchunguza.

Waitara amekiuka kanuni ya 5 ya Bunge inayomtaka kukata rufaa kwa maandishi endapo hataridhika na maamuzi ya Spika badala yake akaenda kwenye vyombo vya habari.

Spika amesema kwa Mwita kusema Spika alikuwa Naibu Mwanasheria mkuu wa Serikali hawezi kujua sheria kuliko yeye.

Spika amesema adhabu iko wazi kanuni ya 84 imezungumzia utovu mkubwa lakini ameamua kumpa Onyo kali na Asirudie tena.

View attachment 2260182
Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara​

Njia sahihi ya kushughulikia Kanuni za Kudumu za Bunge zisizofaa ni kwa wabunge kuzipinga na kuzibadilisha, sio kuzikiuka. Mbunge akiamua kuzikiuka badala ya kuzibadilisha, atashughulikiwa kwa Kanuni hizo hizo mbovu!
 
Back
Top Bottom