USSR
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 9,896
- 22,666
Spika wa bunge la Tanzania Mh Tulia Aksoni amepiga marufuku wabunge kuvua nguo Bungeni akisema ni kosa kubwa na kuonya tukio kama hilo lisijirudie tena
Tulia Aksoni alikuwa akizungumzia suala la mbunge Mwita waitara kuvua koti na tai alipokuwa anaondoka Bungeni kupinga majibu aliyoyaita sio ya kuridhisha kutoka kwa waziri.
Kuvua tai,koti,mtandio,shati au kitu chochote ulichoingia umevaa bungeni ni kosa la kikanuni na adhabu yake ipo .
USSR
===
Wabunge wa Tanzania wameonywa kutovua nguo zozote wanapokuwa bungeni.
Spika Tulia Ackson alitoa onyo hilo baada ya Mbunge Mwita Waitara kuvua koti na tai wakati wa mjadala.
Alikuwa akionyesha kutoridhishwa na na majibu ya serikali - kuhusu fidia kwa wapiga kura wake walioko kwenye maeneo va uchimbai madini.
Alivua mavazi hayo huku akitoka nje ya ukumbi.
Kwa mujibu wa Spika, hakukerwa na namna ya kuondoka kwake, bali alikiuka kanuni za mavazi ya ubunge, ambayo yanahitaji uvaaji rasmi ndani ya ukumbi wa Bunge.
Alielezea kitendo chake ni kilikuwa ni "utovu wa nidhamu".
"Tabia hii hairuhusiwi ndani ya bunge na isijirudie tena," alisema Bi Ackson.
BBC
Sent using Jamii Forums mobile app