Spika Ndugai ameitaka Serikali iache kutoa visingizio kuwa malori ya Dangote yanaharibu barabara ya Mtwara

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai ameitaka Serikali iache kutoa visingizio ambavyo havina msingi kuwa malori ya kampuni ya Dangote yanaharibu barabara za mikoa ya Lindi na Mtwara.

Amesema kinachotokea ni barabara hizo kujengwa chini ya kiwango, kwani ni jambo linalofahamika kwamba malori hayo yanapimwa uzito, hivyo kampuni ya Dangote haistahili lawama.

Kabla ya kauli hiyo ya Spika, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Sera na Watu Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama alisema Serikali itapitia upya ujenzi wa barabara hizo ambazo zimekuwa zikiigharimu fedha nyingi.

Awali wabunge wa kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara walilalamikia jinsi Serikali inavyotumia fedha nyingi katika kuikarabati wa barabara hiyo ukarabati ambao hauna tija kwa kuwa imekuwa ikiharibika.

ITV
 
Dangote amekutana na Rais juzi ikulu iweje mpaka leo waendelee kuleta hivyo visingizio, anatakiwa kuwaondoa wasaidizi wake wanaoshindwa kwenda na spidi yake.
kwani mkuu wamewekewa vikwazo gani vya visingizio gani? h ivi si kila gari barabarani linatakiwa kupima uzito na kuwa na uzito unaotakiwa barabarani? mbona wakina mo, bakhera na matajiri wengine , twiga cement, Tanga cement wanapima uzito? kwanini Dangote wasipime?
 
Ni kweli Huyu ni ndugai wa awamu ya 6. Yule wa awamu ya tano sijui aliendaga wapi. Labda ile barabara ya Dar lindi Mtwara haikijengwa kwa sababu ya malori.
Mwenda zake aliwahi kusikika akisema ikikamilika mtu ataweza kusafiri kwa saloon car toka Mtwara mpaka Bukoba, nadhani alikuwa ana maanisha jambo alipotolea mfano wa saloon car badala ya bus au roli
 
Mbona wakati wa Mwendazake hakuwahi kuitaka serikali kwa jambl lolote!! Akae atulie tuli
Timewazoea mwenyewe anasema walikuwa wamelala

20210515_172214.jpg
 
kwani mkuu wamewekewa vikwazo gani vya visingizio gani? h ivi si kila gari barabarani linatakiwa kupima uzito na kuwa na uzito unaotakiwa barabarani? mbona wakina mo, bakhera na matajiri wengine , twiga cement, Tanga cement wanapima uzito? kwanini Dangote wasipime?
Dangote anaambiwa malori yake yanaharibu barabara, kama ni kupima uzito mizani hakuna lori lisilopima uzito, tatizo ni huko kwa hao wapimaji wanaona malori ya Dangote ndio yanafaa "kupiga"
 
Ndugai endelea kuwanyoosha hivyohivyo angalau ustaafu kwa heshima japo kiduchu. Otherwise huna jema la kukumbukwa nalo
 
Back
Top Bottom