wakikosi
JF-Expert Member
- Feb 28, 2015
- 1,354
- 1,483
Mita karibu 200 toka Mbagala rangi 3 kuelekea Mkuranga kuna mtelemko na kisha daraja la mto mzinga.
Eneo hili la mlima kokoto na daraja la mto mzinga njia ni nyembamba sana,na njia hii ni barabara ya kimataifa ina malori mengi sana.
Jambo baya ni kuwa mara kwa mara huwa kuna malori yanazimika hapo mlimani kokoto,na kufanya njia hiyo kutopitika hata masaa 4 mnakuwa mmeganda tu hapo mlimani na foleni huwa ndefu kufika hata kilometa 3.
Serikali ifanye wepesi wa kujenga njia 4 au 6 kati ya eneo la Mbagala rangi 3 hadi Kongowe pia kujenga daraja la kisasa eneo hilo la mzinga maana wakazi wa Kongowe, Toangoma, Mkuranga, Lindi na Mtwara tunateseka sana na changamoto za kufunga kwa barabara kunakotokana na ajari au kuharibika kwa magari hapo mlimani kokoto na kuharibu ratiba nzima ya wasafiri na wakazi wa huku Mkuranga ,Toangoma na mikoa ya Lindi na Mtwara