Kuna umuhimu gani wa kuwa na CAG wakati ripoti zake hazifanyiwi kazi na Bunge wala Serikali?

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,283
2,043
Hii nchi ina viongozi wa ajabu sana. CAG yupo kwa mujibu wa Katiba kuwepo na kuondolewa kwake lazima kufuate Katiba japo kuna kiongozi tuliwahi kumpata kwa bahati mbaya kiongozi huyo alikuwa hatekelezi baadhi ya majukumu kwa mujibu wa Katiba na mwisho akatuondolea CAG bila kufuata utaratibu uliowekwa na Katiba.

Ripoti yake CAG ya mwaka uliopita ilipelekwa Bungeni lakini pamoja na Ubadhilifu wote uliotwaja kwenye ile ripoti hakuna aliyechukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufikishwa Mahakamani.

Juzi CAG katoa tena ripoti nayo imesheheni ubadhilifu wa Mali za Umma wahusika wametajwa ngoja tusubiri Bunge au Serikali kama itawashughulikia.

USHAURI
Kama Bunge na Serikali zinaona ripoti za CAG hazitekelezeki basi Cheo cha CAG na Ofisi yake VISIWEPO kuliko kuendelea kumtumia CAG huku ripoti yake hazifanyiwi kazi.

Cheo cha CAG kifutwe!
 
Amewekwatu kwa mujibu wa katiba kama bunge lilivyo na mahakama kwa mujibu wa katiba.
Nadhani imeeleweka.
 
*Serikali inasema imeweka mazingira mazuuuri ya uwekezaji LAKINI yenyewe inapata hasara kubwa za mabilioni kwenye huo uwekezaji wenyewe.
Watu hawaelewi Nini?
Shortly, Serikali hii ni dhaifu saana.
Wananchi watumie ripoti ya CAG lasivyo wao ni dhaifuaradufu hawapaswi kulaumu.
 
Back
Top Bottom