Special thread: Vikaragosi vya Masoud Kipanya

Special thread: Vikaragosi vya Masoud Kipanya

TWAWEZA walikuwa sahihi
sawa. napiga vigeregere makusudi ili wapinzani wachukue hatua na kama wasipochukua watakinywea.
kwa mujibu wa akili yangu mbovu.
ukweli utaaki kuwa ukweli bila kujali unatolewa kwa mzaha, utani, ucheshi vigeregere na nderemo
 
Wanadamu ukiwaelewa wala hupati tabu....ni kusoma tu alama za nyakati na kuenda Sawa na mdundo...!!!!
 
KP yupo makini sana, chama kina nguvu kubwa sana wangeweza itumia ,tatizo wanafiki na wachumia tumbo. CCM inahistoria kubwa kwa nchi yetu mbali ya mapungufu yaliyopo.Amkeni Tumieni nguvu ya chama mwekeeni break kwa mambo ya msingi mfano umoja wa taifa letu.
 
Nakubalianan na wewe CCM ni chama kikubwa sana na kinaweza kufanya mambo mazuri kikiamua.

Mfano tu Rais magufuli anashindwa nini kufata utawala wa katiba na sheria za nvhi yetu. Je anashindwa nini kupambana na rushwa na wiI uliokithiri sasa. CCM kama chama kikubwa kinashindwa nini kusimamia mali asili, watu na fedha za walipa kodi?

Magufuli ana fursa kubwa tu ya kujijemgea heshima, sijui kuna tatizo gani?
 
Asante mkuu kwa kutulisha neno takatifu
Katika Biblia takatifu, Joka linawakilisha kiongozi/ utawala wenye mamlaka ya kishetani, utawala wa kimabavu wa kuwaonea watu wa Mungu kwakuwa hauna baraka za Mungu.
 
Huyu bwana amekuwa mtunzi mzuri Sana wa katuni zenye kubeba ujumbe,au maana fulani,ikiwa Kama njia ya kuikosoa serikali,kufikisha ujumbe kwa wananchi,au kuponda au kusifia matendo au matukio ya baadhi ya Viongozi,lakini hapa sijamuelewa vizuri.wadau naomba tusaidiane kutafasiri hii katuni.
kp09102018.jpeg
 
Nchi ilikuwa imejaa mafisadi na matapeli sasa amemaliza kusafisha inakuwa kwa sera zake
 
Back
Top Bottom