Songwe: Ajali ya Malori 2, Bajaji na Bodaboda yaua Watu 5 Momba

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Watu watano wamefariki dunia na wengine 10 wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea katika eneo la Mpakani Wilaya ya Momba mkoani Songwe.

Akizungumza na Mwananchi Digital kwa njia ya simu leo Jumatano Juni 5, 2023; Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Theopista Mallya amethibitisha kutokea ajali hiyo.

Kamanda Mallya amesema kuwa ajali hiyo imehusisha malori mawili, bajaji na bodaboda. "Ni kweli ajali imetokea imesababisha vifo vya watu watano na watu wengine 10 wamejeruhiwa, imehusisha lori moja la IT, bajaji, bodaboda na lori lingine ambalo limefeli breki."

Kamanda huyu amesema kuwa majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya Mpakani - Tunduma na taarifa kamili itatolewa baadaye.

"Imetokea majira ya saa sita mchana, bado tunafuatilia kujua chanzo cha ajali hiyo" amesema Kamanda huyo.



 
Hizi ajali kama ZINA macho vilee maana serikali wakidhibiti sehemu moja inaenda kutokea sehemu nyingine....
Poleni wafiwa
 

Ajali yatokea eneo la Kichangani, Tunduma Mkoani Songwe na watu kadhaa wajeruhiwa.

Taarifa zaidi zitakujia
 
Mwanadamu aliezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi nazo hujaa taabu(Ayubu1:4)

Raha ya milele uwape ee Bwana na mwanga wa milele uwaangazie wapumzike kwa amani🙏🏻
 
Back
Top Bottom