Lori laparamia nyumba na kuua mtu mkoani Songwe

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Mtu mmoja amefariki na wengine wawili wamejeruhiwa baada ya lori lililokuwa limebeba sukari kutoka Tunduma Mkoani Songwe kuelekea Mkoa wa Mbeya kuparamia nyumba eneo la Senjele Wilaya ya Mbozi.

Inasemekana ajali hiyo imeua Mtu mmoja aliyekuwa eneo hilo, imejeruhi wawili ambao ni Dereva na Kondakta, imeua ng'ombe wawili pamoja na kuiharibu nyumba hiyo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe, Theopista Mallya amethibitisha kutokea kwa tukio leo Jumatatu July 17, 2023 huku akisema kuwa aliyefariki dunia ametambulika kwa majina ya Zawad Kyusa (29).

"Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari hilo aina ya Scania T-887 DTJ lililokuwa limebeba sukari kutoka Tunduma kuelekea Mkoa jirani wa Mbeya, alikuwa amebeba mzigo mkubwa wa sukari huku akiwa kwenye spidi kali, alikuwa akijaribu kuyapita magari mengine yaliyokuwa mbele, baada ya kuona atakutana na gari lingine aliamua kukatisha pembeni na kwenda kuparamia nyumba iliyopo karibu na barabara kuu ya Dar -Tunduma" ——— amesema RPC Theopista.
 
Back
Top Bottom