Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,867
Kuna taarifa ya ajali barabara ya Msata-Bagamoyo daladala Coaster imegongana na lori imeua watu wote. Tungoje taarifa zaidi.
Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu panapostahili.
======
Watu tisa wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya barabarani baada ya basi dogo la abiria aina ya coster lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekwa Bagamoyo, kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa limebeba mawe, eneo la Kiromo Bagamoyo.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Pius Lutumo amesema ajali hiyo imetokea Machi 10, 2024 majira ya saa 11 jioni na kwamba chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori, aliyekuwa akiyapita magari mengine eneo ambalo haliruhusiwi kufanya hivyo.
Ameongeza kuwa miili ya waliofariki katika ajali hiyo imehifadhiwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo.
View: https://youtu.be/kU4ClnU4epI?si=rH9gWLwo1odNIwH8