Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

Sio kuwapigia magoti.
Ukweli ni kwamba, wana namba za kadi na majina yote ya wanachama wao mkoa wa Dar na jina la mengi halipo.

Kwa sababu yeye ni fisadi,inawezekana anakadi feki
 
Ahh!! Sio kundi la taarabu ni SEGERE maana Taarabu inachezwa ndani ya ukumbi mara nyingi lakini SEGERE popote yaani sisi ndio Wapiga kura SASA tunangoja nini jamani Si mmeona vituko vya viongozi? Haya Fikiria huyu Mh. Lion yaani amemwaga pwaaaa!! sasa wewe kazi kwako mimi kura yangu CHADEMA WEWE JE..................
 

Nani alikwambia tuna mpango wa kumuongezea miaka mingine mitano? Ili afanye nini?
 

Mods, Lunyungu is right!! huyu engineer hajafanya sawa...pls!!!!!!!
 

Mtoa habari,
Asante kwa makala. Mie nina maswali kidogo hapa kama utaweza kumwaga habari zaidi itakuwa mswano sana sana.

1. Alisema nini juu ya Membe, Rostam Azziz na Lowassa zaidi ya hayo maneno?

2. Hii story ya mama Kilango kukutwa na Madawa ya kulevya ni ya kweli hii? Kama ni kweli basi huyu mama kweli alitumwa na mtu mmoja mkubwa sana maana hizi habari zitafumua siri nyingi sana Tanzania.

3. Hii ya Mengi kupata pesa kutoka nje ya nchi imeshaongelewa hapa JF kama sikosei. Kuna mtu mwenye habari zaidi? Nafikiri kidogo kidogo nchi itarudi kwa Watanzania wenyewe.

Kama huyu mama ndiyo BOSS wa vyombo vya usalama, na ana uwezo wa kwenda hadi ndani ya hizo ofisi na kusoma habari za ndani, basi anaweza kuwa anasema kweli, Na kama anadanganya, basi inatakiwa ahukumiwe kama JASUSI na apigwe risasi.
 
 
Sio kuwapigia magoti.
Ukweli ni kwamba, wana namba za kadi na majina yote ya wanachama wao mkoa wa Dar na jina la mengi halipo.

Kwa sababu yeye ni fisadi,inawezekana anakadi feki



Hvi, mtu ukiwa na utajiri sasa hivi TZ maana yake wewe ni fisadi?

Halafu Samwel, kwa jinsi ninavyoijua hali ya TZ, ofisi za serikali tu zingine haziko "computerized", sasa niambie ofisi za CCM, tena tawi....watakuwa na mfumo mzuri wa kutunza kumbukumbu kweli? Mtindo wenyewe wa kuhifadhi kumbukumbu katika mafaili ya karatasi, hadi utafute jina la mwanachama ukalikosa na kuwa na uhakika kwamba kweli halipo ni kazi kubwa sana.

Simtetei Mengi, ila give the guy a break. Pia namshauri kama hawamtaki, si ahamie chama kingine? Au awe tu mwananchi asiyeambatana na chama chochote? Kwani lazima jamani?
 

- Mkuu Mtanzania, kwa kawaida huwa nina tabia ya kukataa upuuzi regardless unaelekezwa kwa nani, samahani sana kama nimekukwa za na huo mfano wangu nia haikuwa kutomtendea haki Mwakalinga, nia na madhumuni ilikuwa kuweka wazi kwamba pamoja na kushuka sana kwa maadili ya uongozi Tanzania, haina maana wananchi wote pia tumeishiwa maadili, kuna ambao bado tunayo, tunayasimamia na tunayaishi, na tunazikataa kabisa hizi siasa za kwa kuwa mimi ni fisadi, basi ni lazima nihakikishe wote tunaonekana mafisadi,

- Hii tabia mpya iliyozuka ya viongozi uchwara na machangudoa kama Sophia, ya kuamka tu kuanza kuongea pumba bila facts, kwa Waziri Wa Ofisi Ya Rais anayesimamia Takukuru, anasimama mbele ya kamati muhimu kama hii ya Mwinyi na kujigamba kwamba CCM hakuna msafi, na kwamba Lowassa ni kiongozi bora na hana makosa yoyote, ni lazima wananchi wastaarabu kama mimi tuikatae na tutaikataa mpaka mwisho wa dunia.

- Katika kuongea siasa huwa tunatumia mifano yote ya kisiasa, Mwakalinga aliposhutumiwa hapa JF kuwa amepokea hela za Lowassa nilikuwa wa kwanza kusimama kama sasa kutaka facts, aliposhambuliwa tena hapa JF kwamba amepitia Monduli kwa Lowassa pia nilikuwa wa kwanza kudai facts kama ninavyodai facts kuhusu huu upuuuzi wa Sophia, na ahsante kwa kunikumbusha kwamba Sophia ameongea to the public, ninavyofahamu ni kwamba aliongea kwenye kamati tu, ambako hakuna waandishi wa habari wala vyombo vya habari, lakini nimekusikia sana mkuu na samahani sana mimi nilidhani kua hizi ishus zinafanana za kupakana matope,

- Again samahani sana na sitarudia tena mkuu, isipokuwa tu simtetei kiongozi yoyote, mimi huwa ninasimamia principle na sio watu fulani ukiwekwa ukweli sawa, lakini huu upuuuzi wa mitaani hapana bado hili taifa tupo wenye kusikia aibu, na kutumia commonsense as opposed na hawa kina Sophia,

- Again, Mkuu Mtanzania samahani sana kwa kukukwaza, my bad na it won't happen again, promise!


Field Marshall Es!
 
Mh! Jamani, lisemwalo lipo?

Sidhani kama huyu mama, pamoja na "uendawazimu" wake, atakurupuka tu na kutunga jambo kama hili. Lazima kwa wadhifa wake amezifuma hizi ishu mahali, na inawezekana hao anaopambana nao walikorofishana nae ndo akaamua kufumua mambo.

Sasa ndio naanza kujiuliza kwanini Mengi na Malecela waanze kumtangaza kuwa ni kichaa apimwe akili?....forgive me if this sounds like a conspiracy theory, but what if there's a plan to finish off this "Lioness"? Tusishangae tukasikia hali yake ya afya si shwari
 
I hate this tabia ya watanzania " aje ofisini kwangu ajitambulishe" hii statemet ni ya kimwinyi sana, kwani wanachama wengine wote anawajua, crazy!
 
SAY IT AGAIN: "Dr. Slaa for President 2010"

Sikonge,Ili tusonge mbele tunahitaji kuifanyia kazi hii signature yako,Period! Mengine yatafuatia baadae!
 
Haya jamani kwa sasa tumalize hii mipasho iliyoanzishwa na simba jike na tupange mikakati ya kuikomboa nchi hii.

Kwangiu mimi naona wote wanaorumbana ni vichaa tu, wanazidiana kidogo ukiangalia kwa jinsi wanavyotia watanzania umaskini, kwa kweli ukiwa na akili timamu sio lahisi kufanya haya wayafanyayo.

Simba ametusaidia kuvumbua watu akili kuwa kumbe sisiemu kuna viongozi vichaa ndiyo maana ya umaskini uliokithiri kwa watanzania hauishi na ni jukumu letu kuchagua viongozi wenye akil timamu na si hawa vichaa.

nawaombeni jamani tufunge hii mipasho kwa sasa
 
Mambo mazito haya.

Shalom, mbona kimya? Wamekukatia umeme na heater hazifanyi kazi (Baridi).

Njoo Sikonge tupate Maembe kwa wingi sana sasa hivi.

Ukitutafutia wawekezaji wawe wanatengeneza juice au kusindika itakuwa poa sana mwanangu (This is not a JOKE). Maembe ni mengi sana na mengi yanaharibika tu.

Naona mjadala unaishiaishia. Ila dalili za uchaguzi zinaanza kuonekana.

Mhhh, mwakani Tanzania inawaka moto. Siasa za kuchafuana mwakani zitakuwa zinatisha. Maadamu wote wameshajua jinsi mechi inavyochezwa, kazi ipo.

Mungu Ibariki Tanzania,
 

- Tatizo lako sio anything, isipokuwa ni mimi, na mimi nimekuhakikishia mara nyingi sana kwamba huna ubavu wa kusimama na mimi either hapa JF, aua hata in the real life, JF ninakuja kukata ishus sijali upande wa pili upo wewe au anybody, ninachojali facts sasa wewe ukileta za kuleta mimi sina peremende ninakurudishia zile zile za kuleta, uchafu wa CCM au usafi wao mimi haunihusu, kwa sababu ninaamini kuwa kama CCM wote ni wachafu, basi wananchi wote wa Tanzania tuliowachagua kutawala for he last 47 years tunakuwa kama wao CCM, yaani wachafu 100%.

- Ya kumtetea Malecela hayo ni yako, mimi ninatetea principle which Malecela happened to be involved, meaning kwamba hata wewe ungekua involved ningefanya the same, lakini hii ni demokrasia una haki ya kufikiri anyways you want kuhusu ninachokifanya hapa, who cares anyways!

- Mwalimu alimuita Malecela muhuni, kwa tabia zetu za Kitanzania ikiwa na maana ana wanawake wengi, kitu ambacho na Mwalimu alikuwa nacho yaani wanawake wengi, unless una maana Mwalimu alikuwa na maana nyingine labda uiweke hapa, otherwise unahangaika bure ndugu yangu, ufisadi unakuwa established na facts sio midundiko na uchangudoa,

- Jeetu kama nilivyoambiwa na wahusika, hajawahi kuifadhili harusi wala kampeni ya urais wa Malecela, isipokuwa anaweza kuwa aliachangia kama wananchi wengine walivyomchangia, na kama alichanga hazikuwa hela za kutisha maana wangejua especially kampeni za urais ambapo ni shabibu na Abson ndio hasa waliotoa contribution kubwa sana kwenye kampeni yake, sasa unless Jeetu amewahi kuwa a proven fisadi before harusi na kampeni za urais 2005, kama Malecela na mkewe walipokea hela zake hata kama ni senti tano knowingly kuwa ni za kifisadi, then wanahitaji kutangulia Segerea now! na nitakuwa the first kudai hilo!

Otherwise, ninakubali kuwa Sophia anakuwa kichaaa na anahitaji kwenda Mirembe kutibiwa. Na wewe huwezi kunifanya anything hiyo nafasi nimekupa mara nyingi na bado siku zote nimeiacha wazi kama una ubavu anytime tukikutana bring it on sitishiki na hizo chuki zako wivu, ukileta matusi hapa nitakujibu 24/7 na wala sikuogopi pamoja na michezo yako mingi unayoifanya humu JF inayotakiwa kufanywa na watoto wadogo kuliko mtu mwenye PhD ya online na mtumzima mwenye mke na watoto, lakini ndio demokrasia na akili ni nywele, na mimi nitaendelea hapa JF na kusimamia principle bila kujali inamhusu nani.


FMEs!
 

Ha ha ha ha ha ha!

Usiongee na mimi mpaka ukapime mirembe. Sikonge=Simba
 
Halafu mnasema huyu mama kichaa!Huyu mama siyo kichaa huyu isipokuwa ameamua kumwaga ugali baada ya hao wanaojiita wapiganaji kumwaga mboga ili wakose wote.
Mkuu Wazalendo shukran mkuu.Kama una mengi zaidi ya hiki kikao tumwagie mkuu na sisi tufaidike
 
Kaaazi kweli kweli! Tanzania bila mafisadi, inawezekana!
 

Umeonyesha ukomavu wa hali ya juu sana mkuu! Siku zote huwa najiuliza huyu ni Engineer wa matusi! Manake kwenye thread ya Uchaguzi serikali za Mitaa alichemka pia,Nashindwa kuamini kama huyu ni Baba/Mama wa familia.
 
Huyu mama asipuuzwe kwa 100%, haiwezekani kwamba eti yote aliyosema hakuna chembe ya ukweli kwa jambo hata moja! Anne Kilango mbona hajasema kwamba aliyosema Sofia Simba ni uwongo ila alisema ETI kwa nini hakuyasema muda huo wote! Kwa upande wa John Samwel Malecela naye hajakanusha zaidi ya kudai ETI Sofia Simba akapimwe akili! Remember you can extract sense out of nonsense!
 

- Ndugu yangu mbona unahangika sana, unahngaikia nini hasa? kinachikuwsha ni nini hasa mkuu haya maneno unatunga tunga ili yakusaidie nini?

1. Sophia amemsifia Lowassa kuwa ni Mwanaume wa shoka na kwamba hajawahi kuona kiongozi safi na mchapakazi kama yeye, amesifia Rostam, Karamagi, na Makamba kwamba ni viongozi imara sana an wasafi na hasa Makamba kwamba anakiweka chama pazuri sana.

- Hayo ya viongozi wanne umeyatunga na kuyabandika tu hapo uonekane uko objective kumbe ni ayako ni ile ile tu kumchafua Malecela na mkewe, unachohangikia nini hasa mkuu?

2. Mama Kilango alikutwa na madawa ya kulevya na nani? kampeni zote za uchaguzi wapinzani wake wameshindwa kuyasema hayo, kwenye kampeni za urais Sophia alikuwa upande wa Mtandao kwa nini hakusema haya? Waziri wa Takukuru anashindwa nini kutoa ushahidi wa madai yake na kummaliza adui yake mkubwa Mama Kilango?

Unahangaika bure ndugu yangu, hutafanikiwa mafisadi Tanzania tunawafahamu na wanafahamika sana, hizi dataz ni zako sio za kutoka huko kwenye kamati na unapoteza muda wako bure tu even though ninajua kuwa una muda mwingi sana wa mchezo, lakini unahangaika bure! Kama Mama Kilango is too good kuuza madawa ya kulevya ni upuuuzi usio na mfano! kama wazazi wenu ni mafisadi na mmeshiriki kula hela zao za kifisadi poleni sana lakini sio wote ni lazima ni mafisadi, unahangaika bure tu mkuu!

- Hizi dataz ni zako wewe tu mkuu wala hazina anything to do na huko Dodoma! Unatengeneza kichwa cha habari cha kujaribu kuwamanilulate watu hapa JF waamini uko serious unajipa thakns mwenyewe, unahangikia nini rudi kule kwenye ile thread tumalizie ngoma uliyoianza mwenyewe! acha huu utoto JF is bigger than this foolishness!

FMEs!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…