Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

Jamani sasa tumechoka. Hii ndiyo serikali ya kasi mpya, nguvu mpya ..... kweli waziri mzima mwenye dhamana ya kusimamia utawala bora anadiriki kusema wanaotuhumiwa na ufisadi wanaonewa eti kwakigezo kwamba wanaowatuhumu nao sio wasafi. Huu ndio uongozi? Je, kosa langu linafuta na kuondoa uovu wa mwingine? Hii nikusema kwamba kwakuwaviongozi wote walio madarakani waliingia huko kwa pesa za kampeni zilizoibiwa kutoka kwa uma kwnjia mbalimbali ikiwepo Epa, uuzwaji wa mbuga za wanyama, scandales za umeme, migodi ya madini... nk. tusitegemee kwamba kuna kesi ya ufisadi itakayoshughulikiwa.

Sofia ametoa ujumbe wa wzi kwa watanzania kwamba kikwete hawezi hata kidogo kudhibiti wizi kwasababu fedha za wizi ndizo zilizomweka pale. Wizi wa fedha za Epa ndo ulitumika kuendesha kampeni yake na viongozi wenzake, what do you expect? ndio maana Raisi mzima anachekacheka tu kama msanii, he has never been sereous any moment,. hakuna hata kauli yake moja alisha wahi kuitoa kama raisi nikaona ikitekelezwa. too weak for a president. Eti wasemaji wake ni kina Sophia simba, a true picture of a corrupt government.

Kweli inauma sanaaaa.

But the time has come, wananchi hawawezi kuendelea kudanganywa kama mazezeta kila siku. Yatakuja kulipukia pabaya.
 
Nothing's wrong with what Mr Mengi said,mmesahahu usalama wa Taifa umegawanyika?Nani anajuwa shinikizo la Pinda kuteuliwa kuwa waziri mkuu lilitokea upande upi wa usalama wa Taifa?

The way situation hii ilivyo,maneno yanayotolewa hayalingani na ukweli halisi ama hata uzito wa whats behind hayo maneno ama kwa kifupi vijembe wanavyopigana haviendani na serioussness ya matter yenyewe na ndio maana kuna wanaoshangazwa na maneno ya anayeitwa waziri wa usalama wa Taifa kwamba hayaendani na uzito wa wizara anayoiongoza kama kweli angekuwa anashauriana na wanausalama hao ambao wanaripoti kwake.

Wengi wetu hatutamwelewa Mengi kwasababu kubishana na mjinga ni lazima ujibu ujinga wake na hivyo wote kuonekana kama wajinga....Lakini kwa mwenye kutumia akili,utaona Mengi ameamua kujibu hayo kutokana na uzito wa issue yenyewe,kwa walioko ndani ya game hiyo ya siasa,baada ya maneno aliyoyatoa Pinda huko kikaoni,si rahisi kunyamaza kama uko ndani ya game kama ilivyo kwa kina Mengi,Sophia Simba,Pinda nk,kama kambi ya kina Sophia Simba inadai Mengi anyamaze kwasababu yeye si ccm mlitaka aendelee kunyamaza?

Kama mmesahahu kuwa UWT is divided kuhusiana na issue hizi za uongozi na ufisadi,basi hamtaweza kujua ni kwanini Mengi alimshauri Mh SS kwamba aombe ushauri kwa usalama wa Taifa kabla ya kuropoka.....Na Pinda kama kama waziri mkuu na mwanausalama mkongwe ambaye binafsi siamini kwamba yuko upande mbaya wa UWT na uongozi kwa ujumla na yeye pia ameona kasoro hiyo ya kina SS na kina RA ya kutupeleka pabaya kutokana na kuufagilia ufisadi na kushiriki kikamilifu. Issue za ufisadi zilishaugawanya usalama wa Taifa kwasababu wanajuwa yote lakini siyo wote walioshiriki ama kufaidika,na sio wote wenye kufurahishwa na ufisadi pamoja na mwelekeo wa Taifa kwa ujumla.

SS alijaribu kuwasafisha mafisadi na alitingisha kiberiti kuona kama kimejaa ama vipi,upinzani walishapigwa kumbo kiaina na hoja ya ufisadi ni kama imeshatekwa na ccm,ila sasa ccm wako kwenye stage ya kuiuwa hoja hiyo mara baada ya kuiadapt,tatizo ambalo wako nalo ni kwamba maneno wanayotumia ama hoja wanazotumia haziendani na uzito wa issue yenyewe,issue ya ufisadi ni nzito kwasababu something has to be done ili ife ama isahaulike,ili issue ife kama baadhi ya wana ccm hao wanavyotaka,ni either wale wale wanaodaiwa kuwa ni mafisadi ambao wameshakula na bado wanaendelea kula,wawachie wenzao ili nao wale,ama wawashinde wenye kutaka kuwanyang'anya mlo huo either kwa kura ama kiubabe,option nyingine ni mafisadi washindwe bila hiari yao,lastly labda wakubaliane kugawana.....Zote hizo ni probabilities...So ikifikia kwenye bottom line ya issue yenyewe,maneno na kuropoka huwa havina nguvu tena zaidi ya vitendo.....Otherwise it will be an endless comic view ambapo matokeo yake ni worst than a banana republic.Kumwachia mjinga aendelee kuropoka ujinga na wakati matokeo ya maneno hayo ya kijinga ni kuhalalisha ujinga,then kunyamaza ndo ujinga wenyewe.
Dawa ya moto ni moto na wala si maji.
 
Hell yes.



The last time i checked, George Bush and Arnold (will be back) of CA were very rich guys before they became governors.



How do you separate (what is this anyway) politics and business?



Why should he not?



Tell me, how many?



How do you analyse things in bright day? is this a joke or what?

Ohh dear, Solomon, tunaongea two separate languages. So as long as someone has money na hanatoa misaada kwenye chama tawala/government then they tell peopl ehow to run the country!!! You asked me how many ministers mengi amengombana nao? uwwiiii you dont know? that explains all regarding your opinion, naomba usome magazeti na more JF topics unajua jibu la hii. I couldn't uderstand when you said hell yes when i asked you did you understand what i wrote previous in English? if that hell yah means you had no problem understand then what the hell you are complaing about me writing my comments in English and swahili!!!
 
Ha ha ha haha,

Ama kweli nyani haoni kundule. Zitto kawasema viongozi wenzake kwenye vyombo vya habari baada ya kushauriwa asigombee. Ulivujisha siri za chama hapa JF kuwa umezuiwa au kushauriwa kugombea. Ukamtuma rafiki yako Omar kuja kuwapondea chadema hapa.

Kama wewe ni mpenzi, mfuasi ama mwanachama wa CHADEMA nakushauri usinichokonoe.......

Najitahidi sana kujizuia hapa nilipo.

omarrilyas
 
Until his latest press showdown, I thought Mengi could have been either of the following:
1. a total idiot. why? because if he thinks JK & co are clean and steadfast against "fisadi's", then he has lost IT
2. a very smart and shrewd character and has got a secret weapon to hit at and down JK & co at the opportune time before 2010. why? because he believes JK & co a bunch of ****** and they have no slightest idea the difference between a monday morning and a friday afternoon!

Conclusion after this PC.........Mengi is nothing but the biggest IDIOT of all rich people I know in this country!!!
 
wewe ndiye unamchagulia mengi cha kusema na lini akiseme? kwani hii ni china au north korea?

kama sio north korea or china then let everyone have free speech and mengi should stop using his money kufanya watu wasifanye kazi zao. Nyie ndio watu mnaofikiria money has to rule everyone.. and that is why i said to you, you need to start thinking in a brighter day.. well of course it depends if you really EVEN thinking of maendeleo ya watanzania wasio na chochote
 
Ina shanganza kuona baadhi ya watu wanakiona kitendo cha Mengi kufanya PC na kuongea kuhusu anavyojisikia na kuzungumzwa kuhusu uanachama wake ni cha kimakosa.

Mtu yoyote anaweza fanya PC kama anauwezo wa kufanya hivyo na kuzungumza kile ambacho anaona kwake ni sahihi. Sijaona kosa La mr Mengi katika yaliyoandikwa.

Kama kweli kazungumzwa na Sophia kuhusiana na uanachama wake au kuhusu usafi wake na akaona si sahihi , na mahala pa yeye kujisafisha ni katika kuitisha PC kuna tatizo gani ? Yeye ni Mtanzania kama mimi na hawezi kuwa sahihi kwa kila jambo kama mungu, vile vile yeye si Kiongozi katika Tanzania na kwa kuzungumza vile si kwamba alizivunja kanuni za nchi yetu .

Kama uwezo wake wa kujieleza ni mdogo wewe inakupunguzia nini au kukunyima nini wakati yeye ana maisha yake na wewe unamaisha yako , KILA MMOJA ANAHAKI YA KUJIELEZA NA KUJISAFISHA MAHALA POPOTE NA KWA WAKATI WOWOTE. HAIJARISHI MTU HUYO ANAUWEZO WA KUZUNGUMZA KIASI GANI ILI MRADI ASIVUNJE SHERIA ZA NCHI ..!!

Viongozi wa ngapi wapo madarakani na hawajui hata wajibu wao ? Wangapi kati yao weshazungumza Utumbo na tumewasikia ? Kwanini Mengi ? Kila akizungumza kidogo ..Mengi kasema ..Mengi kasema...Kwanini na nyie msiende Kuzungumza ya kwenu ? Acheni unafiki watanzania hatutafika popote kwa mwendo huu.
 
Kuna mwenye kuuliza wa shauri wa mzee Mengi wapo wapi ? Labda ni ulize washauri upande gani ? Siasa au Kibiashara ?

Kama ni siasa Mengi hajajitangaza kwamba yeye ni Mwanasiasa bali tujualo yeye ni mwanachama wa chama cha siasa. Kwahiyo nadhani hata washauri wake humshauri sana vitu vihusuvyo Biashara zake na si Siasa .

Wewe unaetaka kujua washauri wake wanafanya kazi gani , We wakwako wanakupa ushauri gani ?
 
Huyu Mzee Mengi nae anatuzingua tu ,bora angekaa kimya tu
 
Mimi nitaamini kuwa watu wamesingiziwa na huyu mama hapo watakapoanza kwenda mahakamani!

Amandla......
 
Nchimbi na Guninita hawawezi kuwa neutral hawa ni vikaragosi vya Lowassa na Rostam; mmesahau ile dili ya jengo la vijana walivyoshirikiana Nchimbi na Lowassa kumpa Subash Patel?
 
Ningependa sana kupata majibu kuhusiana na NICOL not just talking about Chama ambacho sisi hatuoni manufaa katika jitihada za maendeleo ya taifa hili!

Ufisadi nafikiri haujapewa defination inayoeleweka kwa wote! Mengi ningekushauri unyamaze kimya kwa sababu hututakii memma!
 
Ndugu Mengi angetusaidia sana kama angekuja na majibu ya maswali aliyoyatoa bwana Mayega badala na yeye kuendeleza mipasho


Maji ya mkondo hayachagui njia

Na: Paschally Mayega

RAIS wangu, Waswahili husema maji hufuata mkondo. Wazamivu katika sheria wanasema sheria pia hufuata mkondo. Waswahili na wanasheria katika hili wanakubaliana kuwa katika kufuata mkondo, sheria na maji havina utashi wa kuchagua vielekee wapi bali kule mkondo ulikoelekezwa.

Rais wangu, kama itakupendeza naomba kabla ya kuendelea na mada ya leo, kwanza nitoe fundo lililopo kifuani mwangu. Inawezekana ukawa ni ukweli kuwa mfinyanzi analia vigaeni. Unamkuta mtu kutwa anahangaika, akitangatanga huku na huko akiwalilia wenzake.

Anajinyima na kujidhiki kwa ajili ya wengine. Mara nyingine watu hawa hujikuta wamejikita katika shida za wenzao na wakasahau kuwa wao nao wana dhiki zaidi. Na hawa, huwa hawana wakuwalilia. Nani atawalilia na wao ndio wanaowalilia wengine?

Rais wangu, habari za Kampuni ya NICOL kutetereka zimenigusa kwa namna ya pekee. Wanasema mbuzi wa maskini hazai. Ikitokea akazaa, huzaa mwaka wa njaa, mtoto lazima aliwe. Nimeusikia msemo huu tangu ningali mdogo, lakini leo nausikia kwa uchungu mwingi zaidi. Nausikia kwa sononeko.

Ndugu Rais, baada ya kuhitimu masomo yangu ya falsafa, mwaka 1975 nilijiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyovunjika katika Shirika la Posta na Simu. Niliitumikia nchi yangu kwa muda wa miaka 20 hadi 1994 nilipoomba kustaafu kwa hiari.

Zaidi ya miaka 15 sasa niko mtaani naishi maisha ya kubangaiza. Mhangaikaji. Jua langu, mvua yangu. Sina mchana sina usiku mimi. Nachakurachakura kama kuku jalalani ili mimi na familia yangu tupate kitu cha kuingiza tumboni.

Kama serikali yetu ingetulipa malipo kama yalivyokuwa yameainishwa katika barua ya kustaafu kwa hiari ya mwaka 1994, leo hii dhiki yangu isingekuwapo. Kesi yetu mpaka leo iko mahakamani. Pamoja na ukwasi mkubwa wa baadhi ya viongozi wetu, serikali yetu inathubutu kutulipa pensheni ya sh 20,250 kwa mwezi.

Matumizi ya sh 675 kwa siku ni unyanyasaji. Mcha Mungu anaweza akasema mimi ni mwongo. Tunapokutana na hawa jamaa katika nyumba za ibada tunawaangalia hatuwamalizi. Mungu hadanganyiki! Viongozi wetu hawaelewi kuwa dunia njia wote tunapita tu. Tanueni na teseni kwa jasho tulilolivuja sisi, lakini mkumbuke kila mtu ana siku yake.

Waziri, baba mtu mzima analidanganya Bunge kuwa anatulipa sh 37,000 na sasa atatulipa sh 50,000. Anadanganya ili iweje? Mpaka leo tunapokea sh 20,250. Kila tulipoenda kuulizia nyongeza ya pensheni ya wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki tuliambiwa kwanza hata hizo sh 20,000 haijulikani tunalipwa na nani! Tumemwachia Mungu!

Kiongozi anashika uongozi mara tu anaanza kuotesha majumba kila mahali. Anapasua mashamba makubwa na mifugo mingi ya kisasa bila hata kuwalipa majirani fidia. Wanaendeshwa katika magari ya anasa na wakielea angani dege lao la anasa linakula sh milioni sita kwa kila saa.

Bila aibu mtu anaenda nalo hata kwa safari za kipuuzi kushabikia uchafu nchi za mbali. Katika hali kama hii ni chizi peke yake anaweza kuwaambia watu kuwa serikali haina fedha ya kuwalipa wastaafu inavyostahili au kuwasomesha watoto wetu vyuo vikuu. Naye ataitikiwa na machizi wenzake.

Nimesema mbuzi wa maskini hazai, lakini ikitokea akazaa huzaa mwaka wa njaa, mtoto lazima aliwe. Hapo katikati serikali iliamua kutupoza kidogo, ikatulipa kiduchu katika kile kingi tunachoidai. Wakatokea watu wazima na heshima zao wakatutangazia kampuni iitwayo NICOL.

Wakasema ukiwekeza utaondokana na umaskini. Nani anautaka umaskini bwana! Mimi si nikapanda mbegu zangu pale! Nikawekeza hisa 3,000. Ninapoambiwa NICOL ni DECI nyingine, nguvu zote zinaniisha mwilini. Kama ni kweli, hawa ni binadamu gani wenye roho za kinyama namna hii? Kudhulumu mpaka yatima na maskini?

Majina yao mazito. Wengine mwanzoni sikuwasikia, ningewasikia nisingepanda mbegu zangu pale kwa kuwa wamezoea kujiuzulu. Lakini tumeambiwa kuwa mwana mwema Reginald Mengi, ndiye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya NICOL akiwa na waziri wa zamani aliyejiuzulu, Iddi Mohammed Simba.

Ningependa kujua je, ni kweli ndugu Mengi alihusika katika kuiingiza NICOL kichwa kichwa kwa ununuzi wa Pharmacetical and Beverage Limited (IPBL) iliyokuwa inafilisika kwa kutumia fedha zetu kiasi cha sh bilioni nne?

Sijui kiwanda hiki ni cha nani na sijui kuna uhusiano gani, lakini ni matumaini yetu kuwa bwana Reginald Mengi atatokeza hadharani kutufafanulia jambo hili ili kulinda hadhi yake katika nchi hii. Fundo lililojaa katika mioyo ya wanahisa juu yao kwa ufisadi huu ni hatari kwao kuliko sumu ya nyoka.

Kweli nyongo hukaa na ini. Sasa tunaanza kuwaza mambo mengi. Yawezekana wanaosimama majukwaani kila siku na kuonekana katika vyombo vya habari wakigawa fedha kama msaada wakawa wanagawa fedha hizi hizi zetu? Lazima kieleweke.

Haiwezekani tuwe wajinga ndio waliwao! Kumdhulumu mnyonge zaidi na kumpa mwenye nafuu ili wewe uonekane mwema unatoa misaada mingi ni nini kama si ufisadi uliopitiliza ufisadi papa? Unaweza kweli ukatumia jina la rais wetu au hata jina la Mwenyezi Mungu katika uovu huu?

Tunaomba serikali iwachukulie hatua za kisheria watu hawa hata kama ni kuwafilisi ili kunusuru mbegu zetu. Hapa padogo tunafisadi, tukifanikiwa kupata uongozi wa nchi kipi kitasalimika?

Ndugu Rais, na mimi ni binadamu kama wengine. Nina nyongo na moyo wangu ni wa nyama. Ninaililia nafsi yangu na wana NICOL wenzangu. Baba yetu Reginald Mengi sikuhukumu. Nayaelekeza haya yote kwako kwa sababu kati yao wewe waonekana u mwema.

Tuambie, ni nini hiki mlichotufanyia maskini wenu weusi? Wewe na sisi ni ndugu, mama yetu mmoja, Tanzania. Ukitueleza kwa ufasaha tutakuelewa. Ndugu Rais, ngoja sasa nirudi kwenye mada yangu ya leo.

Rais wangu, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa umepita. Mapungufu makubwa yaliyojitokeza kama yatafanyiwa kazi ni Mungu peke yake anajua. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ameteuliwa kushika wadhifa huo na mwenyekiti wa taifa wa chama chezaji.

Ndiye aliyempa kula. Huyu ndiye refarii. Kwa maneno mepesi ni kwamba anayempa kula au ushindi mchezaji wa kinyang’anyiro cha urais, ndiye baadaye naye humpa kula yule aliyempa kula. Hii peke yake inaondoa uwezekano wa kuiona haki ikitendeka hata kama haki hiyo itatendeka.

Mwenye akili timamu anayecheza mchezo ambao mwamuzi wake ameteuliwa na mpinzani wake, hachezi kwa faida ya mchezo huo. Anacheza kutimiza lengo lake tofauti na lengo la mchezo huo.

Wagombea wetu wa urais kutoka upinzani hali hii wanaiona, lakini wanashiriki katika mchezo huo kwa sababu nia yao kubwa si urais, nia yao iko katika mioyo yao. Chama chenye wanachama wengi kwa maelfu, watakuwaje na mgombea mmoja tu anayeshindwa katika kila uchaguzi?

Kila msimu mgombea ni yuleyule na sera zake ni zilezile. Huyu hana jipya. Ikijakutokea, kama itakujakutokea, wakaupata urais utashangaa kuwaona na wao wenyewe wakishangaa kuupata urais. Haiwezekani kwa mgombea wa upinzani kuupata urais kwa mkondo huu tulionao sasa, na wao wenyewe wanalijua hili.

Mgombea urais wa upinzani atagombea urais mara ya kwanza, anashindwa. Akishindwa na mara ya pili atataka na mara ya tatu na ya nne. Huyu bila kuzuiwa atataka awe mgombea shindwa wa maisha. Tumejipangia kuwa rais hata akipendwa vipi vipindi vyake ni viwili, wewe mgombea shindwa unapendwa vipi uwe mgombea wa maisha?

Hali ya uchaguzi katika nchi yetu ni sawasawa na mfereji uliokwishachimbwa. Ukimwaga maji (uchaguzi) ndani yake maji hayachagui yaende wapi. Yatafuata kule mfereji ulikoelekezwa. Kushindwa katika chaguzi kwa vyama vya upinzani mara nyingi, ni matokeo ya ubinafsi. Hali hii itaendelea kuwepo kwa sababu viongozi wabinafsi katika upinzani wanaendelea kupewa nafasi.

Wananchi lazima waelewe kuwa, lengo, nia na madhumuni pekee ya chama chochote cha siasa ni kutaka kutawala. Kwenda Ikulu. Viongozi wa vyama hivyo ndio wanataka kutawala badala ya hawa waliopo. Si vyama vya ukombozi hivi. Wananchi lazima watofautishe kati ya chama cha siasa na chama cha ukombozi.

Wanachowaambia wapinzani ni maovu yanayotendwa na viongozi wa sasa. Lakini hiyo haionyeshi usafi wao. Wengine wanaweza kuwa wabaya hata zaidi ya hawa tulionao. Ukitaka kuona uchu wa madaraka walionao viongozi wetu wa upinzani, wengi wao wako tayari hata leo hii kwa serikali ya mseto, wao wanaita serikali ya umoja wa kitaifa.

Nia waambulie hata u-DC tu. Jaribu kutafuta mawaziri bora 20 tu kutoka katika vyama vyetu vya upinzani maarufu kama NCCR-Mageuzi, TLP, CUF na CHADEMA. Wanaoleta fujo kwenye vyama vyao hivi sasa nao watataka wawe bora mawaziri kama baadhi ya bora mawaziri tulionao hivi sasa.

Kazi njema inayofanywa na upinzani naitambua na kuiheshimu sana na hasa kufichua maovu yanayotendwa na viongozi wetu wa sasa. Lakini hii peke yake haitoshi kuonyesha kuwa wewe utakuwa mtawala bora!

Ndugu Rais, bado nakubaliana na mawazo ya Mwalimu Nyerere kuwa, rais bora lazima atoke CCM. Uongozi wa CCM sasa hivi umejawa na uozo mwingi. Wema wengi wamefunikwa na waovu wakubwa wachache.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, Bunge la Jamhuri ya Muungano limekubali kuwa Katibu Mkuu wa chama tawala – CCM, Yusuf Makamba kafanya ufisadi, yaani ni fisadi na mtu huyu bado ni Katibu Mkuu, tena wa chama kinachotawala. Chama kitakuwaje kisafi? Unatenganishaje chama na viongozi wake, na hasa wa juu?

Wale wana CCM walio wema wanapaswa kumkana mtu huyu si kunyamaza. Ikishindikana matakwa ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere yatimie kwa CCM hii kupasuka katika vipande viwili. Na hapo ndipo utakapozaliwa upinzani wenye maana katika nchi hii.

Wapo wanaosema uongozi wa juu wa CCM na serikali ni dhaifu. Wengine wanasema uvumilivu na upole vimezidi. Lakini mtu mpole kupindukia na ***** wanatofautiana vipi? Wote hukaa kimya, hata pale wanapotakiwa kutoa maamuzi muhimu.

Idadi ya watu wanaojiandikisha na kujitokeza kupiga kura inazidi kupungua siku hadi siku. Hawaoni faida yake tena. Walitaka wakipiga kura mabadiliko wanayoyatarajia yatokee, lakini hiyo haiwi. Wamechoshwa na namna wanavyotawaliwa. Kupiga kura wanaona ni sawa na kumwaga maji katika mfereji.

Kadiri watu wengi zaidi wanavyozidi kususa kupiga kura, ndivyo tunavyokaribia maangamizi makubwa. Matakwa yao ya mabadiliko yanazidi kukua na kupanuka na kwakuwa wameishaona kuwa sanduku la kura halisaidii kuleta mabadiliko wayatakayo, watayatafuta kwa njia nyingine maana kiu ya mabadiliko haiachi kusumbua.

Ole wao wote walioufupisha upeo wao wa kuona kwa sababu ya ulafi tu. Rais wa nchi atachaguliwaje kwa asilimia chini ya hamsini kama si kutaka kuleta maasi katika nchi? Kwa mkondo huu, CCM 2010 hata wakimsimamisha mbuzi agombee urais, itashinda. Baada ya ushindi huo, hakuna kingine kitakachofuata bali machafuko na maangamizi.

Maafa makubwa yatakayoichafua historia nzuri ya taifa letu. Nani atakubali kutawaliwa na mbuzi? Mwenyezi Mungu atusaidie waja wake kwa kutuondolea kwa njia yoyote ile wote anaowajua yeye kuwa ni viongozi batili. Tunahitaji amani. Amani yetu inachafuliwa na wachache.

Rais wangu Kikwete, watu wako tutakwenda mbele tutarudi nyuma, lakini hakuna tutakachokipata bali kukurudia wewe. Tuondolee hizi baruti kabla hazijatulipukia. Tutengenezee mazingira ya kupata tume huru ya uchaguzi. Mgombea ashinde kwa asilimia inayoonyesha kukubalika na wengi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya aliye chini ya mamlaka yako kusimamia uchaguzi ambao na wewe ni mgombea ni ubatili mtupu. Watu wametawaliwa na tamaa zote, madaraka na mali, wao wenyewe, watoto wao mpaka wake zao.

Maskini na watoto wao wanabaki wakiwa, hata elimu tu nayo wananyimwa, fedha za madini na rasilimali nyingine za taifa lao pamoja na kodi zao vinalambwa na baadhi ya watawala wachoyo, manyang’au.

Ni kujidanganya kusema hali hii itaendelea milele. Iko siku inakuja na wala siku hiyo haiko mbali sana. Mwenyezi Mungu anijalie nisiione siku hiyo! Siku ya kihoro!
Chanzo: Tanzania Daima

porojo tu..ziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Ningependa sana kupata majibu kuhusiana na NICOL not just talking about Chama ambacho sisi hatuoni manufaa katika jitihada za maendeleo ya taifa hili!

Ufisadi nafikiri haujapewa defination inayoeleweka kwa wote! Mengi ningekushauri unyamaze kimya kwa sababu hututakii memma!

wewe ni mamluki tu...............
 
Big up mengi......................sofia paka huyu ni malaya tu
 
Mengi nae amezidi kulia lia.
 
Ohh dear, Solomon, tunaongea two separate languages. So as long as someone has money na hanatoa misaada kwenye chama tawala/government then they tell peopl ehow to run the country!!! You asked me how many ministers mengi amengombana nao? uwwiiii you dont know? that explains all regarding your opinion, naomba usome magazeti na more JF topics unajua jibu la hii.

Na kwa wewe kusema tu kuwa Mengi kagombana na mawaziri bila kuwataja hao mawaziri na kile ambacho waligombana na mengi, ndiyo inaeleza zaidi vile ulivyo.

I couldn't uderstand when you said hell yes when i asked you did you understand what i wrote previous in English? if that hell yah means you had no problem understand then what the hell you are complaing about me writing my comments in English and swahili!!!

Please, if this is what you call english, then, we have a problem. Check your grammar friend, take time to know the language better before you undress yourself this much.
 
Back
Top Bottom