Juaangavu
JF-Expert Member
- Nov 3, 2009
- 935
- 132
[Hamna kitu cha kufanya tuanze upyaa kabisa..tuwe tuna concentrate na service delievry na kuleta maendeleo nchini?
Nashindwa hata kuelewa tuanze wapi, inakatisha tamaa.[/QUOTE]
Pa kuanzia ni kila mmoja wetu kuweka dhamira ya dhati ya kubadilika, kuanzia jinsi tunavyofikiri mpaka tunavyoenenda. Taifa limepoteza mwelekeo, na mamilioni ya watanzania bado wanaimani kuwa mtu mmoja anayelala pale magogoni na kipenzi chake, wanatosha kushughulikia mambo yote ya msing ktk taifa hili.Haiwezekani na hata tukiamua kulazimisha iwezekani; hakika haitakuwa. Lakini kama tutasimama kila mmoja kwa nafasi yake, kuanzia wauza vitumbua kando ya barabara mpaka wanaoshindia kwenye viyoyozi (kwenye magari yao mpaka maofisini); na kila mmoja wetu akawa na dhamira iliyonyeupe ndani yake. Hakika tutarekebisha ubabaishaji unaozidi kujikita ktk taifa hili.
Mambo yanayofanyika ndani ya nchi hii kwa nyakati hizi, ninahisi hata shetani anashangaa wapi umetoka ujasili wa namna hii. Tuanza kujihoji kila mtu kwa nafasi yake, ni kwa jinsi gani tumechangia hali ilivyo leo -wengine tumeshiriki kuwasifa wanaoiba mali ya umma kuwa ni wajanja; na wale wanaofuata utaratibu kuwa ni wajinga, wamepewa nafasi wameshindwa kuitumia. Wengine kwa maamuzi mabaya au takrima ya Shs 3,000 (ambayo ni sawa na wastani wa Shs 1.65 kwa siku kwa muda wa miaka mitano) tumeshiriki kuwaweka viongozi madarakani; orodha hakika ni ndefu. Lakini wakati na majira ni sasa ya kutafuta mabadiliko ndani ya nafsi zetu kisha nje yetu. Hapo tutakuwa tumeinza safari salama.