Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

Mmh ajiuzulu nani? Sofia Simba? Labda mpaka kiama. Hakuna utaratibu wa kujiuzulu CCM, si kila mtu anamlinda mwenzie kwa sababu wote si wasafi? Sasa akijiuzulu atabaki nani? Laba serikali nzima iachie ngazi. Maana ni kashfa juu ya nyingine. Fikiria mawaziri kujiita Madaktari wa falsafa! Hata aliyewateua anawaangalia tu itakuwa Simba. Ingekuwa ni Kujiuzulu angejiuzulu angefanya hivyo alipomtukana Janeth Kahama kwenye uchaguzi wa UWT
 
Bado naungana na Mzee Mwanakijiji alipo mshauri sita kufikia mwisho wa wiki hii awe ameachia madaraka, naamini Luhanjo ameisha draft barua ya kumfukuza kazi huyu mama inasubiri JK AISIGN.
 
Kwa kifupi I dont buy any of those Bullishit.. its not waht we want to hear for God's sake... No offense it was poor and childish not to mention stupid press release i hv never heard b4

... sijaona alichokisema mabacho kinawasaidia watanzania.. yaani sasa wanachokifanya ni kama swlaal la wachawi wawili watoke mtaani waanza kuumbuana walivyokula nyama zawatu na kuchukua misukule watu wa watu mtaani.. we unafikiri itawasaidai wahanga.. zaidi ya kuwafanya mishkaki na wao.. yaani mungu anisamehe ila kuan wakati nafikia hatua ya kufikiri labda tuchapane kidogo (Mungu aepushe hili) ndio heshima itakaa.. hawawezi kufanya kama tamthilia au amshairi leo anasoma huyu kesho yule.. na kila mtu na vyombo vyake vya habari.. kuanzia huyu raisi mpaka mwenyekiti wa serikali za mitaa hakuna afadhali..

NINA HASIRA haaaaaahhh
 
Ndugu Mengi angetusaidia sana kama angekuja na majibu ya maswali aliyoyatoa bwana Mayega badala na yeye kuendeleza mipasho


Majina yao mazito. Wengine mwanzoni sikuwasikia, ningewasikia nisingepanda mbegu zangu pale kwa kuwa wamezoea kujiuzulu. Lakini tumeambiwa kuwa mwana mwema Reginald Mengi, ndiye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya NICOL akiwa na waziri wa zamani aliyejiuzulu, Iddi Mohammed Simba.

Ningependa kujua je, ni kweli ndugu Mengi alihusika katika kuiingiza NICOL kichwa kichwa kwa ununuzi wa Pharmacetical and Beverage Limited (IPBL) iliyokuwa inafilisika kwa kutumia fedha zetu kiasi cha sh bilioni nne?

Sijui kiwanda hiki ni cha nani na sijui kuna uhusiano gani, lakini ni matumaini yetu kuwa bwana Reginald Mengi atatokeza hadharani kutufafanulia jambo hili ili kulinda hadhi yake katika nchi hii. Fundo lililojaa katika mioyo ya wanahisa juu yao kwa ufisadi huu ni hatari kwao kuliko sumu ya nyoka.
Chanzo: Tanzania Daima

Kuna kesi mahakamani kuhusiana na gazeti la Mtanzania lililoandika kuhusika kwa Mengi katika NICOL, na story iko katika gazeti la Tanzania Daima la jana ambalo naona halijawekwa mtandaoni kama ambavyo Raia Mwema halijawekwa mtandaoni. Soma gazeti hilo utapata majibu. Hii ndio Tanzania. Tusubiri tuone.
 
Leo Mzee Mengi kakutana na waandishi wa habari (dakika chache zilizopita) na hiki ndicho alichoongea:

TAARIFA YA MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP LTD. BW. REGINALD A. MENGI KWA VYOMBO VYA HABARI
6 NOVEMBA, 2009

_____________________________________________​




Ndugu Wanahabari,

Kwa msemo wa kiingereza “Don’t argue with a fool because people may not know the difference between you and the fool”, wenye maana kwamba usibishane na mjinga kwa sababu watu wanaweza kushindwa kufahamu tofauti yako na huyo mjinga!

Hata hivyo wakati mwingine inakulazimu kujibu hoja unapomwona mtu anapotosha mambo kwa makusudi.

Kwanza, kuhusu kuropoka kwamba sitoi misaada kwa CCM, hilo ni jambo linalozushwa na watu binafsi na kwa malengo binafsi. Viongozi wakuu wa CCM ambao ni waadilifu na wanaosimamia ukweli wanajua undani wa jambo hili.

Pili, kuhusu uwanachama wangu wa CCM:

Napenda kuwaambia kwamba mimi ni Mwanachama wa CCM tangu tarehe 18 Aprili,1977 na kadi yangu ni Na. B124595, iliyotolewa na Tawi la Kisutu, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam.

Hivyo basi madai yote kwamba mimi si mwanachama au nilijiunga na chama hivi majuzi kama inavyoelezwa na Mheshimiwa Waziri wa Utawala Bora Sophia Simba, Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Shaaban Kilumbe Ng’enda na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa DSM John Guninita ni uongo, uzushi na umbea wenye lengo la kudhoofisha juhudi za viongozi wa juu wa CCM na baadhi ya wanachama za kupiga ufisadi vita.

Ndugu Wanahabari,

Hawa wanaodai kuwa ndani ya CCM hakuna kiongozi msafi ni wazi kwamba wamedandia chama hiki hivi majuzi. Ningetoa ushauri kuwa waondoke na watuachie chama chetu kwa kuwa hawafahamu msingi imara wa CCM.

Mwisho napenda kumshauri Waziri Sophia Simba kwamba katika vita dhidi ya ufisadi ni vyema akanyamaza. Kwa sababu yeye si mwadilifu na hivyo hawezi kusimama kupinga vita ya ufisadi.

Aidha, ningemshauri kabla hajazungumza aombe ushauri kutoka taasisi za serikali kama vile usalama wa taifa badala ya kuropoka na kupotosha ukweli wa mambo.

Nawashukuru sana kwa kunisikiliza.


Reginald A. Mengi

MWENYEKITI MTENDAJI, IPP LTD.

Mwe mwe mwe mwe!!!
Kyama kyangu kimekwisa!!
Yaani wanadandia treni kwa mbele
 
lakini mimi naona huyu mzee anamis-use media zake!anaentertain public quarrels!
 
Huyu mama anajiamini nini,wasije mkolimba bure???

..hawawezi huyu mama ni spika ya JK......hamkuona alivyowanyamazisha waliotaka amtose baada ya kuonekana wazi ametumia cheo chake kupaka watu matope na kuwapiga..wakafikiri angeondolewa kugombea uwenyekiti UWT ...jk akajifanya haoni hasikii.....na siku ya uchaguzi akawaambia wabunge wamchague ......waachane na wazeee wasiosoma[janeth kahama]
 
lakini mimi naona huyu mzee anamis-use media zake!anaentertain public quarrels!

Mkuu Geof hivi Press Conference si waandishi wote wanaruhusiwa kufika ama ni wale wa IPP tu?
 
Yaani kuthbitisha yeye ni mwanachama wa CCM kunahitaji kuitisha press conference? Kweli sasa hizi PC hazina maana tena.

Why all these defensive measures now Mzee Mengi? au kwa kuwa brigade lako lote limteketezwa kule Dodoma na hii ndio namna fulani ya ku surrender?

Unalo hilo unatafuta pa kulitulia zigo lako.
 
"Ningetoa ushauri kuwa waondoke na watuachie chama chetu kwa kuwa hawafahamu msingi imara wa CCM"

Hili ndio jibu sahihi kwa CCM. Maana chama kimetekwanyara. na watu wasio na maadili bali wenye arrogance na uchuuuuu
 
Mkuu Geof hivi Press Conference si waandishi wote wanaruhusiwa kufika ama ni wale wa IPP tu?

wote wanaruhusiwa.lakini huyu mzee naona kama anapenda sana public quarrels.

ni mara nyingi sana ni mtu wa kutolea hasira kwenye medias
 
Yaani kuthbitisha yeye ni mwanachama wa CCM kunahitaji kuitisha press conference? Kweli sasa hizi PC hazina maana tena.

Why all these defensive measures now Mzee Mengi? au kwa kuwa brigade lako lote limteketezwa kule Dodoma na hii ndio namna fulani ya ku surrender?

Unalo hilo unatafuta pa kulitulia zigo lako.
hata mimi simuelewi huyu mzee!
 
naomba nimpe saluti mzee Mengi kwa kuzungumza mambo machache lakini ya msingi.Sijui Auntie Sophie atasemaje akija kujua kuwa Mzee tangia 77 ana kadi mkononi! Kweli usilolijua ni kama usiku wa giza

Kwani CCM hawana database ya wanachama wao?, Duh! mbona inatisha sana. Ndiyo maana chama kimevamiwa na mamluki wa kifisadi. Ila baba wa Taifa alishasema kuwa CCM ni Chama kikubwa, mi naongeza ni kama Bahari kuna madudu ya kila aina yanayoliwa na yasiyoliwa ambayo ni sumu.

Yaani waziri wa Usalama wa Taifa anakosa taarifa sahihi kuwa Mengi ni mwana CCM?. Inaonekana kuna gap kubwa sana kati ya waziri na watendaji wa UWT yupo kama "Shadow" tu pale hana analolijua zaidi ya mipasho ambayo ni Hatari sana kwa Usalama wa Taifa.

It's time sasa JK awe serious kama fadhila ameshalipa aweke watu wenye uwezo wa kufiri kwenye nafasi muhimu kama anayoshika huyu mama. Otherwise tunasafari ndefu sana Tanzania. Yaani tuna "Ombwe" ya uongozi.
 
Leo Mzee Mengi kakutana na waandishi wa habari (dakika chache zilizopita) na hiki ndicho alichoongea:

TAARIFA YA MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP LTD. BW. REGINALD A. MENGI KWA VYOMBO VYA HABARI
6 NOVEMBA, 2009


_____________________________________________


Ndugu Waandishi wa habari,

Nimewaita hapa leo kuzungumza nanyi kwa lengo la kuweka rekodi sawa.



Mwisho napenda kumshauri Waziri Sophia Simba kwamba katika vita dhidi ya ufisadi ni vyema akanyamaza. Kwa sababu yeye si mwadilifu na hivyo hawezi kusimama kupinga vita ya ufisadi.

Aidha, ningemshauri kabla hajazungumza aombe ushauri kutoka taasisi za serikali kama vile usalama wa taifa badala ya kuropoka na kupotosha ukweli wa mambo.


Nawashukuru sana kwa kunisikiliza.


Reginald A. Mengi

MWENYEKITI MTENDAJI, IPP LTD.




Eidha Mengi smart kama anavyotaka watu wafikirie au washauri wake ni watu wa HOVYO HOVYO

Kwanza hii ni wrong move strategically...for obvious reasons

Pili huwezi kutafuta ligi na Sofia simba...period!!

Tatu anasema Sofia simba akatafute taarifa usalama wa Taifa lakini kasahau kuwa huyo huyo sofia simba ndiye waziri wa Usalama wa Taifa

Nnne: Mengi keshaingia kwenye huo mtego sasa i hope next time hatowaambia mawakili wake wazungumze kwa niaba yake...huyo mama keshaingia ulingoni na by the look of things naamini kuwa keshavaa gloves

Tano: Hiyo ya kubishana na mjinga ingebidi afafanue je mjinga ni nani hapo?
 
Yaani nchi hii bwana.

Sasa kama hauchangii CCM unakosa nini?si bora ukae kimya

unachngaia CCM ili iweje?yaani mie nilishachoka kabisa na wafanyabiashara wa kibongo..ufisadi tu na hakuna cha kamanda wala kamandoo..

Vita ya Mengi na Mama simba ni kuhusiana na nini?yule mama wa mipasho lzima tamlipua Mengi tu
 
Yaani nchi hii bwana.

Sasa kama hauchangii CCM unakosa nini?si bora ukae kimya

unachngaia CCM ili iweje?yaani mie nilishachoka kabisa na wafanyabiashara wa kibongo..ufisadi tu na hakuna cha kamanda wala kamandoo..

Vita ya Mengi na Mama simba ni kuhusiana na nini?yule mama wa mipasho lzima tamlipua Mengi tu

inathibitisha kuwa Mengi isnt as smart as some people want us to believe

the same applies to hao the so called washauri wake
 
Ndugu Mengi angetusaidia sana kama angekuja na majibu ya maswali aliyoyatoa bwana Mayega badala na yeye kuendeleza mipasho
hayo ni maoni ya Mayega binafsi akitimiza haki yake ya kujieleza. Mengi mara zote hujitokeza hadharani akiona kuna umuhimu wakufanya hivyo, hii ni hekima kubwa, maana sikuja tu kutoa majibu kwa hoja zisizo nz mashiko.

Hajawahi kuogopa wala kusita kuulezea ukweli kuhusu yeye na biashara zake.

Kwako wewe hili lakutukanwa na simba hakupaswa kulitolea ufafanuzi. sio.
 
Back
Top Bottom