Ama kweli ccm sasa imechoka, Waziri Simba ndiye anaye simamia utawala bora, vyombo muhimu vipo chini yake (Takukuru na Usalama wa Taifa) sasa kama amefika mahali pa kuona kuwa Jeetu Patel ni fisadi kwa kuchangia au 'kufadhili' harusi ya Anne Kilango anachelewa nini kumshughulikia kupitia vyombo hivyo tunavyovitegemea watanzania?
Kama kuchangia kampeni za uraisi ni tatizo wewe kama waziri mwenye dhamana ya kusimamia utawala bora unasubiri nini? Je una orodha ya wale wote waliomweka madarakani Mheshimiwa Rais kwa michango yao? Je wana kashfa yoyote ya ufisadi au la? Ni mpaka kamati ya Mzee Ruksa ikae ndio upate pa kuzungumzia?? kwanini usiwajibike maana huna faida na taifa hili.
Kama kweli kina Sendeka na wenzake wanaganga njaa kwanini
wasishughulikiwe na vyombo husika? Kwani nini cha ajabu kuweza kupata evidence ya kuganga kwao njaa ilhali vyombo vyote vya usalama na rushwa vipo chini yako?
Inavyoonekana sasa CCM imefika pabaya kwani wale wenye dhamana ya kutuongoza badala ya kufanya hivyo wanatafuta pa kuegemea.. sisi waongozwaji tuegemee wapi?? Haijalishi kiongozi anajifanya msafi kiasi gani kama kuna chembe ya ufisadi hatumtetei hata kidogo kwani tumechoshwa, anapaswa kuwajibika kama sio kuwajibishwa.
Ushauri wa bure kwako waziri Sophia Simbani ni huu.. majukumu yako kwa taifa hili ni kusimamia utawala bora, yote unayoyajua yaliyokwenda kinyume na dhana ya utawala bora wapaswa kuyafanyia kazi na kutoa taarifa kwa watawaliwa pia kuhakikisha unatumgoza vema kumalizia awamu hii ya kwanza ya Mheshimiwa Jakaya, vinginevyo kabidhi mikoba kuna wenye uwezo na uchungu na nchi hii.