Snitch ndiye mtu hatari zaidi🙌

Snitch ndiye mtu hatari zaidi🙌

Wahenga wanasema ni bora kuishi na mchawi kuliko mnafiki usiyemjua
Hivi umewahi kuishi na snitch na unajua kabisa ana kunafikia?

Then ukawa una mchora tu na unafiki wake anavyojimaliza?

Mara zote mnafiki ni mtu wako wa karibu sana, pengine unayemuamini zaidi na ku mkubari sana

Mtu hawezi kukufanyia unafiki kama hakujui vizuri, never
Wanaotuuza ni wale wanaotujua nje ndani, wanajua makazi yetu wanajua mishe zetu, wanajua siri zetu, time ya kutoka na time ya kurudi

Kisa changu, nilikuwa na rafiki yangu hivi mzurii wa muonekano
Yule rafiki yangu ukitoka naye out ukasifiwa wewe, alikua anaumia mno yaani unamuona kabisa uso unabadilika

Ukifanya vizuri anakusifia, ila maneno na uso havina ushirikiano
unaona kabisa ananyongea
Mimi nilimpenda mno na kumsifia, ila siku ikitokea akahisi nimependeza kuliko yeye alikua anachukia

Kipindi hicho alikua jobless, nikasema hapana ngoja nimvute niwe naye sehemu ninapofanyia kibarua
Aisee nilijuta 🙌🙌 kwa sababu alinijua nje ndani basi alinifanyia figisu kazini, karibu nianguke na pressure

Wewe binti popote ulipo nimekusamehe ila nimejifunza

Na ajabu sasa niliona dalili zake za wivu mapema japo zilikuwa ndogo nikawa nazipuuza najidai mtakatifu na mama huruma

Kilichonikuta ni fundisho

Issue ni kwamba bado sikomi, kuna muda najikuta tena naamini mtu haraka pamoja na kwamba nilishawahi kuumizwa( sijui kwanini)

Je wewe umewahi kuishi na mnafiki huku anajua hakupendi/hakufurahii/hakukubali?
Ulifanyaje mwisho ilikuwaje?

Ni namna gani ya kum escape snitch unaemjua kabra hajakusabahishia madhara?

ShesRise_1 👋…
snitch and hater’s… bila kusahau machawa hawa nao pi ni hatari 🔥
 
Kuna comment flani ya mwamba GT mshamba_hachekwi aliandika alisema ukiona tu ama kuhisi red flag kwenye mahusiano, urafiki ama any relationship usingoje chukua hatua na maamuzi mara moja na ninaishi na huo msemo.
Alisema ukweli kuna sehemu nafsi inakataa kabisa unalazimisha mambo yana kukuta
Mfano mleta mada red flags zilikuwa zinakujia mfano ukisifiwa unaona wazi rafiki yako anavyofeel mara moja ungechukua hatua yote hayo yasingekutokea.
Hakika
Naziheshimu sana red flags ni ishara za kweli zinazojitokeza kabla ya damage.
Nami najifunza aisee
 
Unatakiwa utofautishe kati ya wivu na roho mbaya maana usije kusema una wivu kumbe una roho mbaya
 
Unatakiwa utofautishe kati ya wivu na roho mbaya maana usije kusema una wivu kumbe una roho mbaya
Wivu huzaa chuki _chuki huzaa roho mbaya
Hivi hitu ni mashoga wa kutupwa
 
Miye na snitch km mafuta na maji, kuna best yangu alikata tuu mawasilino. Katokea rafiki yake akawa ananipa habari za yule. Nikamchana tuu tukionanaa usimtaje G kbs.
Mbona mate yalimkauka.
 
Miye na snitch km mafuta na maji, kuna best yangu alikata tuu mawasilino. Katokea rafiki yake akawa ananipa habari za yule. Nikamchana tuu tukionanaa usimtaje G kbs.
Mbona mate yalimkauka.
Alitaka utie neno ili aongeze chumvi ayapeleke
 
Alitaka utie neno ili aongeze chumvi ayapeleke
Nilimchana yule tumetoka mbali sana, familia zetu tumeziunganisha sisi. Home kwao wananijua kwetu pia .
Acha zako siku tukikutana tutaongea tuache. Alipotea km upepo na akawa hata anitafuti teena.
 
Nilimchana yule tumetoka mbali sana, familia zetu tumeziunganisha sisi. Home kwao wananijua kwetu pia .
Acha zako siku tukikutana tutaongea tuache. Alipotea km upepo na akawa hata anitafuti teena.
Dah nina hakika hii ilimuuma sana sana
 
Alafu lisomi lizuri lkn hafai kbs, niliona sms yake IG huko anasema mtt kakuwa nikija anifungulie geti.
Nikamjibu sina geti wala ukuta, unataka ukafananishe na G eenh.
Mkuu umefanya nimecheka sana nimewashtua wachawi lol 🤣🤣
Geti la nyoko
 
Back
Top Bottom