Snitch ndiye mtu hatari zaidi🙌

Snitch ndiye mtu hatari zaidi🙌

Usiwe na marafiki uliowazidi uwezo au kuwa level sawa kiuchumi, marafiki zako wawe watu waliokuzidi kiuchumi na status, unaoita marafiki inabidi wawe washkaji Tu wa Hapa na pale basi.
Sasa hao waliokuzidi wakiwa na mtazamo kama wako, bila shaka watakukimbia.

Kama wewe hutaki rafiki uliyemzidi, kwanini wewe utakiwe na aliekuzidi?
 
Wahenga wanasema ni bora kuishi na mchawi kuliko mnafiki usiyemjua
Hivi umewahi kuishi na snitch na unajua kabisa ana kunafikia?

Then ukawa una mchora tu na unafiki wake anavyojimaliza?

Mara zote mnafiki ni mtu wako wa karibu sana, pengine unayemuamini zaidi na ku mkubari sana

Mtu hawezi kukufanyia unafiki kama hakujui vizuri, never
Wanaotuuza ni wale wanaotujua nje ndani, wanajua makazi yetu wanajua mishe zetu, wanajua siri zetu, time ya kutoka na time ya kurudi

Kisa changu, nilikuwa na rafiki yangu hivi mzurii wa muonekano
Yule rafiki yangu ukitoka naye out ukasifiwa wewe, alikua anaumia mno yaani unamuona kabisa uso unabadilika

Ukifanya vizuri anakusifia, ila maneno na uso havina ushirikiano
unaona kabisa ananyongea
Mimi nilimpenda mno na kumsifia, ila siku ikitokea akahisi nimependeza kuliko yeye alikua anachukia

Kipindi hicho alikua jobless, nikasema hapana ngoja nimvute niwe naye sehemu ninapofanyia kibarua
Aisee nilijuta 🙌🙌 kwa sababu alinijua nje ndani basi alinifanyia figisu kazini, karibu nianguke na pressure

Wewe binti popote ulipo nimekusamehe ila nimejifunza

Na ajabu sasa niliona dalili zake za wivu mapema japo zilikuwa ndogo nikawa nazipuuza najidai mtakatifu na mama huruma

Kilichonikuta ni fundisho

Issue ni kwamba bado sikomi, kuna muda najikuta tena naamini mtu haraka pamoja na kwamba nilishawahi kuumizwa( sijui kwanini)

Je wewe umewahi kuishi na mnafiki huku anajua hakupendi/hakufurahii/hakukubali?
Ulifanyaje mwisho ilikuwaje?

Ni namna gani ya kum escape snitch unaemjua kabra hajakusabahishia madhara?

ShesRise_1 👋
dawa ya snitch yoyote ...wewe unakua snitch zaidi yake
 
Back
Top Bottom