Snitch ndiye mtu hatari zaidi🙌

Snitch ndiye mtu hatari zaidi🙌

Bado mnaendekeza ushost na wanawake tu? Hamkomi

Mi wanawake wenzangu nishawakatia laini zamani Sana,wivu roho mbaya, husda, uchawi...wanini mimi aku!

Wanaume wako poa sana,hata michongo ya hela asee ndo wananivuta na kunipa ramani
Wanawake tumekaliaga majungu na fitina tu! Ukiwa na mwanao mmoja au wawili hukosi michongo ya hapa na pale!
 
2017 Ilinitokea hii, sisahau maishayangu yote.

Jamaa alikuwa akifanya kazi sehemu flani sasa alikuwa akija kunitembelea kazini kwangu.

Tukazoeana, baada ya muda akawa rafikiangu sana sana asana.

Sikumoja akaniambia anaomba nimtafutie nafasi kwenye ninapo fanyia kazi mimi kwasababu kazi anayo fanya anapata ela ya kulatu hawezi fanya kitu kingine chochote.

Nikaona sio ishu nikamvuta nikamtambulisha kwa mkurugenzi nikamtafutia nafasi nzuri mambo yakawa fresh.

Siku zilivyo kwenda nikaamua kumfundisha kaziyangu kwa vitendo then nikamwambie aende akasome kidogo akapata cheti, alivyorudi
Nikamfanya kuwa msaidiziwangu,daah.

Kilicho fuata Mungu mwenyewe ndio anajua jamaa rohoile ya kunisnich aliipatia wapi.

Yani kunaishu nilimfundisha nikamuonyesha jinsi ya kupata pesa, tukawa tunafanya pamoja lakini jamaa alinirecodi na kupeleka kilakitu kwa mkurugenzi, aisee, sitaki hata kukumbuka.

Baada ya muda mflani nilipokwenda rotation kurudi nikakuta mambo yame haribika na kazi imeisha,.
Nilijiuliza sana what happened, sikupata jibu, alafu lijamaa linanipigisha stori tu na kuchekacheka lenyewe.

Mungu mkubwa baada ya kuondoka skumoja mkuu akanipigia sim akaniambia A To Z nilicho fanya na aliempelekea taarifa zote.

Nili huzunika sana, ila Mungu mwema this time na fanya mambo yangu mwenyewe na jamaa linajua nasonga mbele mara kumi ya linivyo kuwa pale.

Nikama Mngu alinifanyia njia kuondoka ili mambo yangu yazidi kunyooka.

Thanks God umefanya njia pasipo na njia.
Kwenye ishu hapo ulimfundisha wizi sio?
 
Wahenga wanasema ni bora kuishi na mchawi kuliko mnafiki usiyemjua
Hivi umewahi kuishi na snitch na unajua kabisa ana kunafikia?

Then ukawa una mchora tu na unafiki wake anavyojimaliza?

Mara zote mnafiki ni mtu wako wa karibu sana, pengine unayemuamini zaidi na ku mkubari sana

Mtu hawezi kukufanyia unafiki kama hakujui vizuri, never
Wanaotuuza ni wale wanaotujua nje ndani, wanajua makazi yetu wanajua mishe zetu, wanajua siri zetu, time ya kutoka na time ya kurudi

Kisa changu, nilikuwa na rafiki yangu hivi mzurii wa muonekano
Yule rafiki yangu ukitoka naye out ukasifiwa wewe, alikua anaumia mno yaani unamuona kabisa uso unabadilika

Ukifanya vizuri anakusifia, ila maneno na uso havina ushirikiano
unaona kabisa ananyongea
Mimi nilimpenda mno na kumsifia, ila siku ikitokea akahisi nimependeza kuliko yeye alikua anachukia

Kipindi hicho alikua jobless, nikasema hapana ngoja nimvute niwe naye sehemu ninapofanyia kibarua
Aisee nilijuta 🙌🙌 kwa sababu alinijua nje ndani basi alinifanyia figisu kazini, karibu nianguke na pressure

Wewe binti popote ulipo nimekusamehe ila nimejifunza

Na ajabu sasa niliona dalili zake za wivu mapema japo zilikuwa ndogo nikawa nazipuuza najidai mtakatifu na mama huruma

Kilichonikuta ni fundisho

Issue ni kwamba bado sikomi, kuna muda najikuta tena naamini mtu haraka pamoja na kwamba nilishawahi kuumizwa( sijui kwanini)

Je wewe umewahi kuishi na mnafiki huku anajua hakupendi/hakufurahii/hakukubali?
Ulifanyaje mwisho ilikuwaje?

Ni namna gani ya kum escape snitch unaemjua kabra hajakusabahishia madhara?

ShesRise_1 👋
Kuna comment flani ya mwamba GT mshamba_hachekwi aliandika alisema ukiona tu ama kuhisi red flag kwenye mahusiano, urafiki ama any relationship usingoje chukua hatua na maamuzi mara moja na ninaishi na huo msemo.

Mfano mleta mada red flags zilikuwa zinakujia mfano ukisifiwa unaona wazi rafiki yako anavyofeel mara moja ungechukua hatua yote hayo yasingekutokea.

Naziheshimu sana red flags ni ishara za kweli zinazojitokeza kabla ya damage.
 
ulijuaje kama wote ni snake? alf umewezaje kukutana na member wote hao ndugu au mlikutana kwenye issue za biashara?
Naona tu, mm nina id karibia 20 hapa zotezinakutana na watu tofauti tofauti. Had il ya mwashamba. Yani nina multiple identity humu mpaka utashangaa.

Mtu jukwqani chadema kabisa lakini laivu mjumbe wa kamati kuu ya ccm nec. Huyu si snake huyu?
 
Naona tu, mm nina id karibia 20 hapa zotezinakutana na watu tofauti tofauti. Had il ya mwashamba. Yani nina multiple identity humu mpaka utashangaa.

Mtu jukwqani chadema kabisa lakini laivu mjumbe wa kamati kuu ya ccm nec. Huyu si snake huyu?
kwanini uwe na multiple aidii mkuu nimeogopa😂😂,, watu mpo kimasta sana
 
Back
Top Bottom