Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumanne, Trh 15 Aprili 2014 - Majadiliano ya bunge zima kwa sura ya 1 & 6

Nduka Original

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
1,012
816
Kikao cha bunge maalum la katiba kinaendelea leo hii, kinachojadiliwa hasa ni sura ya kwanza na sita ya kwenye rasimu ya katiba.

Mh. Mbarouk anaunga muundo wa serikali mbili maana ndo anaamini utawapa Zanzibar utajiri na Zanzibar itakuwa half London.

Mh. Hija Hassan Hija anasema watanganyika hawana hasara ya serikali mbili wala moja maana walishachukua mali zote kwa miaka hamsini iliyopita na Zanzibar wameibiwa kwa miaka hamsini iliyopita.Zanzibar ilipwe fidia ya miaka hamsini iliyopita.

- Anasema wenye mali ni Tanganyika,mawaziri wa Zanzibar wamekuwa wakisema muungano umekuwa ukiwaonea na anashangaa ni nini kimewapata.Anasema kuna mawaziri wana maslahi yao ndo maana wanashindwa kuipigania Zanzibar.

- Anasema mawaziri hawatetei muungano bali wanatetea maslahi yao maana kuna watu walikuwa wanapigania muungano ila baada ya kupewa uwaziri wakakaa kimya kwahiyo hawa ni wasaka tonge wana njaa.

Mh. Silima anasema yeye ni muumini wa muundo wa serikali mbili.Anasema mfumo huu umesaidia katika nyanja mbalimbali katika kuleta amani,nguvu na mshikamano Tanzania.

- Hakubaliani na muundo wa serikali tatu kutokana na hofu anayoiona mbele.Anaogopa kusikia kuwa kuna serikali ya Zanzibar,Tanganyika pamoja na ya Muungano.

- Anawaomba wabunge wasiruhusu kuupa mwanya muundo wa serikali tatu ili kuleta amani na kudumisha utaifa uliopo.

- Anasema ni muumini wa serikali mbili zitakazofanyiwa marekebisho ili kutoa changamoto zilizopo sasa.

-Asema muundo wa serikali tatu utaleta gharama kama kutakuwa na marais watatu,mahakama za serikali tatu

Mh. Felisia .Anaipongeza tume kwa kazi waliyoifanya kwa kuandika sura zote za rasimu ya katiba mpya.

- Anasema yeye ni muumini wa serikali inayoleta umoja na mshikamano ambao ni tofauti na nchi nyingine ambao ni serikali mbili.

- Hataki kuona mzanzibar na mtanzania bara wakitengana kwa mambo yasiyo na msingi.

Mh. Mbarouk Ally - Anaunga mkono taarifa ya wachache ya kamati namba nne na marekebisho yote waliyofanya.

- Anasema Muundo wa kuwatoa kwenye matatizo yaliyopo ni muundo wa shirikisho wa serikali tatu.

-Anasema wazanzibar wamechoshwa na muundo huu wa serikali mbili na anasema hakuna mzanzibar ambaye anataka muundow huu uliopo maana umekuwa kero sana kwao.

-Anasema Miaka hamsini wanazungumzia kero hizi za serikali mbili naa badala ya kupungua zinaendelea kuongezeka.Anasema kamati na tume mbalimbali zimeundwa kutatua migogoro mbali mbali za muungano na bado zimeshindwa na nyingnie zilikuwa chini ya waziri mkuu wa muungano na viongozi wengine na bado zimeshindwa.

- Anasema wazanzibar wamechoshwa na udharimu wa muundo wa serikali mbili.

- Anawaumbua viongozi wa zanzibar wakija Tanzania bara wanaunga muundo wa serikali mbili lakini wakirudi zanzibar wanaanza kulilia muundo wa serikali tatu.Anasema wazanzibar wasipokuwa makini hata vyeti vya ndoa vitatoka Dodoma.

Mh. Pamela Masai - Anasema wajumbe wameacha maslahi yenye tija kwa watanzania na wote na kukimbilia kwenye muundo wa serikali.

- Anaunga mkono maoni ya wachache kwenye Kamati namba 10.Na anaunga mkono Lugha ya kiswahili kutumika kama lugha ya taifa.

- Anapinga vipengele vya Uadilifu,uwajibikaji uwazi na usawa kuondoshwa kweye tunu ya taifa.

-Anasema kamati zote zimeunga mkono sura ya pili ibara ya sita 2(6) ,anasema kwahiyo hata mamlaka waliyonayo wajumbe wa BMK ni mamlaka waliyopewa wananchi.

- Anapendekeza muundo wa Serikali tatu.Anasema kama wananchi wanataka serikali mbili basi waendelee na serikali tatu alafu wananchi wapendekeze maoni ya muundo wa serikali wanayotaka.

Mh. Mwinyi Haji Makame - Anasema muungano huu waasisi wetu wameleta muungano wa undugu na sio vinginevyo.

- Gari ya serikali mbili ishachemka na haizuiliki,anasema hata wakina Jussa wakileta unafiki na chuki muundo huu utaendelea kuwepo..

-Anasema miaka hamsini ya mapinduzi ndio umeijenga Zanzibar.

- Anamalizia kwa kusema kuwa matatizo ya Zanzibar kwa muundo huu wa serikali mbili yashashughulikiwa ndani ya kamati zote zilizoundwa kutatua matatizo ya wazanzibar.

Mh. Asumpta Mshama - Anaanza kwa kuelezea kinga ya bunge. Anasema wananchi ndo watajua na kupima yapi ya kweli baina ya wale wanayozungumza wabunge ili waweze kuamua.

- Anasema rasimu imeleta serikali tatu lakini walio wengi wamesema wanataka serikali mbili.Anaiponda tume ya Warioba kuwa pamoja na usomi wao kwa hili la kuleta serikali tatu haoni mantiki ya usomi wao na anasema anaona kama hawajasoma kabisa.

- Anasema watu waokaa na kuandaa maangamizi kamwe hawawezi kuwa wasomi kabisa.

- Anasema utamuduni wetu ni muundo wa serikali mbili na hawawezi kuchomoka kabisa na ansema ili serikali tatu iwepo lazima kwanza muundo uliopo uvunjwe na hayupo tayari kuona hilo jambo likitokea na hakuna wa kutenganisha mchanga wa Zanzibar na Tanganyika na anasema muundo wa serikali tatu ni mzigo kwa wananchi maana kodi ya watanzania itapotea bila sababu za msingi.

Mh. Chiku Abwao - Anaanza kwa kusema yeye ni muumini wa muungano na muungano wa shirikisho ndo utaondoa muungano wa manung'uniko na kuhakikisha Tanganyika inapatikana kwa ghalama yoyote, ananukuu ''Jasiri ni yule anayejali kwao''

-Anasema bora muungano uvunjike ila Tanganyika ibaki na anaunga muundo uliopendekezwa na tume ya Warioba maana ni maoni ya wananchi walio wengi.

- Anamnukuu Lukuvi kuhusu jeshi kutawala nchi kama muundo wa serikali tatu ukipita na kusema hata hivyo jeshi lipo kwa ajili ya wananchi wa Tanzania pia anawasifu wazanzibar kwa kupigania utaifa wao.

- Anasema wabunge walio wengi wa tanzania hawapo bungeni kuunga muungano wa tanganyika na zanzibar bali wapo kuunga mkono muungano wa TANU na AFRO-SHIRAZI Party.

- Mh. Anaunga mkono kamati yake no saba na waliofanya marekebisho sura 1&6 kwa muundo wa serikali 2 na anawaunga mkono wananchi wengi waliokubaliana na muundo wa serikali mbili.

- Analaani kitendo cha mh. Hija kwa kitendo chake cha kutukana mwanamke maana naye kazaliwa na mwanamke.

- Anasema wapemba wameanza ubaguzi baada sherif Hamad kuukosa urais na anamtuhumu mh sherif Hamad kuwa muasisi wa ubaguzi wa kipemba na kingazija.

- Anataka hati ya muungano wa pemba na unguja iletwe bungeni na ioneshwe kwa wajumbe.Anasema viongozi CUF Zanzibar ndio wanaotaka kuuvunja muungano na sio wazanzibar wote.

Mh. Oluoch - Anasema kumbe bungeni ni sehemu ambapo ukweli unaachwa na uongo kuchukuliwa. Anasema hata waasisi waliunganisha mchanga wa Tanganyika na Zanzibar ili kuunda serikali moja na sio mbili kama ilivyo sasa.

- Anasema ikiwa wazanzibar wakitaka muungano hawatapika kura ya kuunga muundo wa serikali mbili...

- Anasema walimu wanaunga hoja serikali tatu.

Shamsa Mwangunga - Anatoa pongezi kwa serikali ya JMT kwa kulea muungano huu mpaka kufikia miaka 50 maana malezi yanapitia changamoto nyingi.

- Anasema muungano huu ni tunu maana nchi nyingi zimejaribu kuwa na muungano na shirikisho ila hawakuweza kufika mbali ila kwa muungano huu wa tanzania ni swala la kujivunia kuwepo mpaka sasa hivi. Uvumilivu na upendo wa watanzania ndo umeleta muungano huu kuwa imara na kero mbali mbali zimeweza kutattuliwa na kubaki kero moja ya uchumi.

- Utawala bora tumekuwa tukisifiwa duniani kwa kuwa na utawala bora kwa kuweza kuudumisha muungano huu na kuna watu wamekuwa wakipotosha kuwa kuna kero wakati sio kweli hakuna kero na kero zilizobaki ni ndogo na zinafanyiwa kazi.

Anasema serikali ya nchi mbili ni zimwi tulijualo na tumelizoe na serikali ya nchi tatu hatulijui ''Zimwi likujualo halikuli likakwishaaaa''

Mh. Salehe Nassoro Juma - Anaelezea msimamo wake ni muungano wa serikali tatu na anawatoa wasiwasi watanzania na wapemba wanaofanya biashara ya vitunguu tanzania bara kuwa serikali tatu hazivunji muungano na kama ukivunjika tanzania imeasini mkataka wa haki za binadamu na wataendelea kuishi kama DIASPORA hata muungano ukivunjika.

- Anamshukuru mh. Kikwete kwa kuanzisha mchakato huu wa katiba mpya,maana kabla ya mchakato huu ilikuwa kosa la jinai kuzungumzia muundo wa muungano.

-Anasema hakuna asiyejua kuwa muundo wa serikali mbili una tatizo na suluhisho la matatizo haya ni muundo wa serikali tatu,anasema pia kuwa mawazo ya waasisi wetu yamezeeka inabidi yafanyiwe modification na ametolea mfano wa China jinsi walivyofanyia modification mawazo ya waasisi wao na mambo yanaenda vizuri.

Mh. Haji Omar - Anaanza kwa kuunga mawazo aliyoyatoa kwenye kamati no 7 mawazo ya walio wengi kwenye sura ya 1 & 6 juu ya muundo wa serikali mbili.

- Uhalai wa Karume kuchukua dhamana ya watu wa zanzibar kuhusu muungano,anasema mzee Karume alikuwa anatimiza ilani ya chama chake cha ASP juu ya umoja na kuhakikisha elimu inakuwa bure,matibabu bure,makazi bora kwa wazanzibar wote.

Faida za muungano, anasema
1.Umeme jimbo la Tumbatu
2.

-Anasema wananchi walio wengi Zanzibar wanaunga muundo wa serikali mbili

Mh. Panya Abdallah - anaunga mapendekezo ya wengi kutaka serikali mbili iendelee.

- Anawapongeza waasisi wetu kuweza kuunda muungano huu na maadui wengi wameshindwa kuuvunja na wataendeleza yale yote waliyoyaacha.

- Anasema muungano hauwezi kuvunjwa kwasababu ya kero wako kero ni jambo linaloweza kufanyiwa kazi na kutekelezeka.

- Anasema kuwa CUF wanataka serikali tatu na CCM wanataka serikali mbili na CUF ndani ya Zanzibar wanasema wanataka serikali ya ''M(N)KATABA''.

- Anasema CUF hawautaki muungano ila njia nyepesi ya kurudi mkoloni.

Mh. Ezekiel Maige anasema kuwa lugha zinazotolewa na Wazanzibari zina ukakasi. Anasema kuwa Zanzibar ina wilaya 10 ambazo zote zina barabara za lami na umeme tofauti na Tanzania Bara.

- Anasema kuwa hayo yote hawayaoni na badala yake wanazidi kulalamika kuwa wanaonewa na Bara. Anahoji iwapo ikatokea Zanzibar kukawa na utajiri Mkubwa kuliko Bara, je Wazanzibari watakuwa tayari kuisaidia Bara.

Mh. Fahmi Dovutwa anasema
, Alama za taifa zitakua Wimbo wa taifa, nembo ya taifa na bendera. Dora haimtambui Mungu kwa hiyo iyo wimbo wa taifa itolewe kwenye alama ya taifa. dhana ya Kuomba Mungu asaidie inamaana Dola inasilikiliza wanaMungu tu wakati taifa hili halifungamani na dini. Nami ntasimama ntapigana kuhakikisha Katiba inamtambua Mungu.

- Kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine. Sera ya TANU iliruhusu wazee watoto na walemavu kunyonya. nataka iwe kutegemeana sio kunyonyana.

- Watu wanaoamini serikali tatu mpaka sasa wameshindwa kutuonesha jinsi watakavyo tatua matatizo tulio nayo. watu wa serikali tatu wameshindwa kujenga hoja. Namlaumu sana Mbowe. Chadema wana wana serikali za majimbo lakini wanashindwa kufafanua vizuri.

- Natoa shukrani za pekee za rais kwa kuridhia hii ijadiliwe na kusimamia elimu za kata. namshukuru pia Lowasa aliye mshauri Rais.

Mh. Joseph Mbilinyi anasema: Naunga mkono serikali tatu kama ilivyoletwa na Tume ya katiba,kwa hiyo tunaunga mkono maoni ya wananchi.

- Aliye haribu huu mchakato ni Rais aliyekuja kuelezea msimamo wa chama chake badala ya kuzindua bunge.
Hiki ni kipindi cha kwaresma acheni unafiki. Tumeharibu pesa nyingi. CCM wameishiwa mikakati wameanzisha mkakati wa kuzomea. Mwingulu anataka serikali moja lakini anaogopa kusema. Tuko kwenye nafasi nzuri sana la kujadili hili swala la sivyo tutalijadili kwa kulazimishwa.

- Leo Lukuvi anatutishia nchi itatawaliwa na jeshi vizuri,mbona rais wetu alikua mwanajeshi na anatuongoza? wanajeshi ni ndugu zetu, wakitawala kuna tatizo gani?

- Serikali tatu ni tija. kila chenye gharama kina faida. Mara nyingi viongozi wa dini wanakosea wanapokuwa upande wa dola dhidi ya wananchi. Mfano Rwanda. Unapopima maralia au ukimwi inapimwa kwenye kidole sio mwili mzima acheni kuzingua eti walio hojiwa ni wachache.

Mh. Mahamood Mussa anasema, Naomba Muongozo wako. Humu ndani ulituambia anakuja Rais au mwenyekiti wa CCM?.

- Katika kamati yetu baadhi ya wajumbe walikua wanazungumzia sikukuu za kitaifa upande wa zanzibar. wenye walikua wanatambua 10/12. wenzetu wanakubaliana na katiba ya 63 ya mkoloni.

- Walitudanganya wamepita kutafuta hati za Muungano hadi un hawakuzipata wakati zipo dar. sasa zimepatikana, wataongea nini tena?

- Tuliungana kuunganisha ulinzi, kutumia soko na ardhi ya Tanganyika. haya ndo yalikua malengo ya muungano. Tunaendeleza serikali mbili asanteni sana.

Mh. Pindi Chana, Anaanza kwa kuunga mkono serikali mbili.

- Anasema haiwezi ikawa nchi na shirikisho lazima tuchague moja ama nchi ama shirikisho. Iwe serikali mbili kwa sababu imetokana na hati ya makubaliano.

- Anauliza serikali tatu imetokana na chimbuko la hati ipi?

- Wananchi wananiuliza hivi hayo Marais watatu watalipwa na nini? je wataishi wapi au hapa Ludewa. Walimu wana vipaumbele vyao sio serikali tatu..

- Serikali wanazozitaka watanzania ni serikali mbili. hata humu ndani watu wengi wanaochangia wanataka serikali mbili. Hiyo serikali yenu ya tatu haina bunge, mahakama wala visa.

- China nchi ni kubwa lakini ina rais moja. USA kubwa lakini ina rais mmoja sisi eti marais watatu, watanzania tuwe makini sana.

- Namshukuru Balozi Ombeni Sefue kwa kutuonesha hati ya makubaliano.

- Kabla ya 1992 tulikua na chama kimoja CCM,kulikuwa na document za kidumu chama cha mapinduzi.

- Serikali mbili hazikwepeki, kama tukitaka kutest tusitest kwa watanzania.

Mh. Jesca Msambatavwangu,anaanza kuzungumzia kero za muungano,

- Ibara 34(1) ya katiba ya JMT, inaonesha Tanzania Bara imechukua sehemu kubwa ya muungano,anasemna hayo yalikuwa mawazo ya waasisi wetu.

- Malalamiko yaliyo mengi ni kwamba tumechukua mambo ya muungano na tumeyachukua kuwa ya kwetu ndo maana Zanzibar wanalalamika. Sasa tuandike katiba mpya kwa upendo na hekima.

- Orodha ya mambo ya muungano iliyo elezwa wakati wa muungano yanaendelea kuongezeka kila siku. Tuache kuongea maneno ya wanaume waliyo tangulia bali tuongee maneno yetu sio fulani alisema hivi.

- Kama tunasema orodha ya muungano yatakua saba tupange sisi hakika tutaridhiana.

- Mimi naunga mkono serikali mbili lakini inaonekana tumeimeza Zanzibar.

- Mimi naomba swala la muundo Rais wa Zanzibar abaki kuwa ni makamu wa rais wa Muungano na rais wa muungano aendelee kuwa rais wa Tanzania bara.

- Zikiwa serikali tatu halafu hizo serikali tatu zikazembea kuwalisha haya majeshi ya serikali tatu haya majeshi yatatugeuka.

- Hoja ya gharama. Unaposema serikali ya tatu haina gharama ni uongo usiopingika.

- Hati ya muungano. ukiona mtu anazungumzia maswali ya hati ya ndoa jua kuna mawili ama kapata mtu mwingine au anataka kwenda mahakamani kuvunja ndoa, muogope sana.

Mh. Abdallah anasema, Mimi na wananchi wangu tunaunga mkono serikali tatu. Lengo kuu ni kuondosha utata uliopo wa kikatiba. Msomaji wa maoni ya walio wengi alisema;

- Marekebisho ya walio wengi yakipita Zanzibar itabidi irekebishe katiba yake.

- Nilivyosikia hivyo nikaogopa,nikajiuliza kama hoja hiyo ikienda kwa wananchi ili mipigiwe kura watakataa?

- Wanasema Zanzibar imeruhusiwa kujiunga na OIC ni uongo. Sisi ndugu zenu mbona hatujui? Hadi leo hakuna fedha iliyopatikana toka Zanzibar kwenda benki kuu.

- Njia pekee ya kuondokana na hili tatizo ni muundo wa serikali tatu, hizi pesa za Zanzibar kila siku wanakokotoa zimekua kokoto hadi zisiletwe?

- Zimekuwa kama Balali au ndege ya Malaysia hazionekani?


==============
Mwenyekiti wa BMK anasema muda umeisha na hata kama wakimpa nafasi mjumbe anayefuata kuongea muda hautatosha.

Anaanza kusoma matangazo na anatangaza kamati ambazo zitakuwa na vikao jioni.

Anatangaza baadhi ya wageni wa wajumbe wa bunge maalam la katiba na wageni wengine waalikwa.

Anamkaribisha waziri wa katiba na sheria wa SMZ kutoa muongozo wa kuahirisha bunge maalum la katiba kabla ya muda ili waweze kujiandaa na vikao vya jioni.

Walioafiki wameshinda na mwenyekiti kwa utani anasema ''Ambao hawajaafiki basi wabaki ndani ya bunge''.

Mwenyekiti anaahirisha BMK mpaka leo saa 10 jioni.

==== Bunge la Katiba maalum la jioni===

Wabunge washaingia bungeni tayari kwa kuendelea na vikao.

Mwenyeketi anasema majina ya watakaochangia kesho majina watayapata leo na kama kuna mjumbe ana udhuru asisite kusema.

Mh. John Chiligati. Anasema Tanzania inapata heshima kubwa kimataifa kutokana na muungano maana kuna nchi mbalilimbali wameshindwa kudumisha muungano na sisi tumekuwa km mnara na kielelezo cha africa na dunia nzima.

Anasema pamoja na miaka hamsini kuna ambao wanaubeza huu muungano na anawahasa watanzania kutojali hao wanaokataa muungano.

ANasema ambao wanakataa huu muumngano kuna waliolelewa na kusomeshwa na huu muungano na anasema mungu awasamehe maana hawajui walitendalo.

Anasema wenye haki wanayongngania ni kueza tu kujua kama muumgano ni batili.

Hao hao wasiotaka muungano ndo hao wanaotaka muungano wa serikali tatu,anasema waasisi wetu walipima muungano wa serikali moja,mbili na tatu na kuona serikali mbili ndo unafaa.

Anadai serikali tatu ni ghalama wa wananchi na waendelee na muungano wa serikala mbili lakini wanachotakiwa ni kuuboresha muungano huo na kutatua kero zilizopo.

Anazungumzia kwa mapana matatizo mbali mbali ya muungano na jinsi ya kuyatatua.

1.Mfuko wa pamoja
2.Chombo cha kutatua matatizo ya muungano
3.Uchumi wa zanzibar

Anaunga hoja serikali mbili.


Mh. Sira Mwamboya- Anasema kundi lake ni no nne lenye Lissu na Mtikila unaeza ona jinsi lilivyo na anasema wana matusi kwenye kamati.

Anasema kuwa msimamo wake ni serikali mbili na anaamini serikali mbili itashinda.

Anausifia muungano kuwa umemsomesha na mpaka anautumikia,anasema Zanzibar hakuna shida ya barabara na maji na anasema huduma ya uzazi ni bure.

Anasema thekuthi mbili ya watu wa zanzibar wako unguja na theluthi moja ipo pemba.,

Anatoa takwimu ya maoni ya muungano yaliyochukuliwa pemba na unguja na anasema kwa hilo basi tume ya warioba ilikuwa na matatizo.

Anasema kuwa cuf na chadema wamefunga ndoa ya mda mfupi na anashangaa toka lini chadema akawa na huruma na Zanzibar.

Anasema cuf wamepoteza mwelekeo na ripoti zote wamemwachia Tundu lissu.Anasema cuf wamejenga msingi kwenye tope basi watazama maana wameishiwa kisera.

Anasema cuf walikuja na mkataba na baada ya kufika huku maalim seif anatangaza kibanda mkaa kuwa wanataka serikali tatu.

Anasema hapa serikali mbili mpaka kieleweke.


Mh. Selasini,
anaanza kwa kushukuru mwenyekiti na wananchi wa Rombo.

Anaipongeza tume ya warioba kwa kazi waliyoifanya na anasema sio vizuri kuibeza kamati ya jaji warioba.

Anasema sio vizuri kwa kuwabeza viongozi wa nchi maana ni tabia mbaya na watoto wetu hawana la kujifunza kwa kubeza viongozi.

Anazungumzia waasisi wa muungano na wanazunguzwa kwa ucheleweshwaji wa kuleta hati ya maridhiano ya muungano.

Anasema waasisi walifanya kazi nzuri lakini kuna mapungufu hasa hati hii iliombwa kwa muda mwingi bila kuletwa.

Anasema Nyerere alikuwa mtu wa kubadilika kutokana na matukio ya muda wake.

Anasema katiba sio ya ccm wala wapinzani bali katiba ya wananchi.Anasema katiba ni mkataba wa maridhiano.

Katiba inayojadiliwa ni ya wananchi hivyo lazima ijadiliwe ili katiba ya wananchi wote ipatikane.


Mh .Nchemba- Anasema inabidi kutambua muundo huu na kama unapaswa kuwepo. Ananukuu maelezo ya Mwalimu kuhusu kuanzishwa kwa muungano huu uliopo.

Anasema kutamani ni hatua moja,kupata hatua nyingine na kupenda kuendelea kuwepo ni hatua nyingine na angependa labda tanganyika iwepo lakini haiwezekani maana wanahitaji kupunguza matumizi ili pesa hizo ziende kwenye miradi mingine.

Mh. Mwigulu anazungumzia hasa ghalama za serikali tatu na matatizo yanayoweza kuikumba.

Mwigulu anampiga kijembe mwl Oluochi kuwa hata yeye amashindwa kutatua matatizo ya walimu na anasema kuwa kuna walimu wanamwambia asimpitishie bajeti maana anazipiga juu kwa juu.

Anasema wanaotaka serikali tatu wamevimbiwa na demokrasia na anawaasa kupunguza ghalama za serikali tatu.

Anasema sio vizuri kuwasema vibaya waasisi wetu maana wanaheshimika sana mfano wakatoliki wanataka mwl Nyerere aheshimike lakini sisi tunabaki kumsema vibaya.

Anasema anayetaka serikali tatu aseme hizo pesa za kuendeshea zitatoka wapi maana masharti ya mikopo sasa wanayopata ni magumu.



Mh. Honoratha Chitanda,
anasema yeye ni makamu wa rais wa cwt,anasema mapendekezo yalipelekwa tucta na tucta iliunda balaza na kupitia maoni na kila balaza lilipeleka maoni.

Tucta ilipitia mapendekezo na maoni na kutoka na mapendekezo ya serikali moja.

Anasema labda makamu wa tucta anaweza kuwa amejiskia vibaya au kudhani amedharauliwa na anaomuomba radhi ndugu Mgaya.

Mchakato,tume na bunge hili sio wa kawaida na anasema waache kuchepuka.

Anawapongeza tume ya jaji warioba kwa kazi nzuri.

Anaishukuru serikali kukata mishahara ya wafanyakazi ili iweze kuleta maendeleo na hawatakuwa tayari kukatwa tena mshahara endapo kutaongeza serikali tatu na ghalama zisizo na msingi na ndo maana wakapendekeza muundo huu wa serikali mbili.

Mh. Hamad Masauni, Anasema walitathmini ripoti mbalimbali na kuona ripoti ya warioba ni hatari sana na maoni yake hayatekelezeki

Anasema mapendekezo ya serikali tatu yanaibua kero nyingine nyingi.

Changamoto na matatizo ya serikali mbili yanatekelezeka na utekelezaji wake sio serikali tatu bali serikali tatu ni kuongeza matatizo mengine.

Anasema kuna watu wana misemo ambayo sio ya kutaka muungano,na hawashtuki kuona watu hawa wanamkebehi Sheikh Karume jemedali wa mapinduzi ya zanziba.

Anasema kuna wajumbe hawana hofu wanadai hati ya muungano haipo,anasema wanailinganisha hati ya muungano kama barua ya mapenzi kwamba inahifandhiwa chini ya mto.

Anaichambua rasimu ya warioba kwa kusema upande wa zanzibar wananchi wa unguja walio wengi hawakutoa maoni kuhusu rasimu ya katiba mpya anasema maoni yalichambuliwa ni maoni ya mikoa miwili ya pemba.

Anasema wazanzibar walio wengi hawataki muungano wa serikali tatu bali serikali wa muundo mbili.

Anasema wazanzibar hawawezi kuingia kwenye mfumo wenye matatizo na malumbano.

Mh.

Anasema alikuwa kwenye kamati no mbili, na anasema tanganyika ili surrender madaraka yote ndani ya muungano.

Anasema nchi mbili haziezi kuungana na kuunda nchi mbil au tatu bali nchi moja.

Anasema tanganyika haijapata hasara yoyote maana yenyeewe ndo nchi,zanzibar ndo inapata madhara makubwa kwenye huu muungano.

Anasema serikali imekosa uaminifu na uongozi bora.

Anasema suluhu yake ni kwenda kwenye muundo wa serikali tatu,ya tanganyika,mapinduzi ya Zanzibar na ya shirikisho.

Ili kuondoa kero zilizopo lazima tusiwe na mawazo mgando,tutoke tulipo na twende mbele maana kubaki hapa tulipo ni kujidumaza.

Mfumo unaotufaa ni muundo wa serikali tatu.

Mh. Nassoro Salim Ally, anasema yeye ni muumini wa serikali mbili na kuunga mkono marekebisho ya kamati no 7 ya kuondoa neno shirikisho.

Anamshangaa mjumbe alotoka kuongea pamoja na kuwa mwalimu wake lakini haoni busara yake na maneno aliyoyasema sio mazuri.

Anasema baada ya muungano huu wa miaka 50 kuna faida na maendeleo ambayo yamepatikana ndani ya serikali mbili,anayesema hakuna maendeleo ni mnafiki.

Anasema CUf ndio hawataki serikali mbili maana wana lao jambo,hawataki amani,mshikamano na nguvu,anasema sio kwamba hawataki serikali mbili bali muungano na wanataka kurudisha utawala wa kisultani.Usultani haurudi ng'ooo.

Anasema historia iliyokuwepo nyuma ni kwamba hawa wenzetu hawana nia njema.

Anasema Cuf wanataka kuleta serikali tatu ili kutugawa watanzania maana hawana nia njema.

Anawaomba wapemba wenzake kuunga mkono serikali mbili unaoleta upendo,mshikamano na umoja.

Anasema ametukanwa na kutishwa kwenye balaza la wawakilishi lakini ataendelea kushika msimamo wake wa kuunga mkono muundo wa serikali mbili,atatetea muungano wa serikali mbili kwa nguvu zake zote na hakuna kutishana.

Anaunga hoja ya muundo wa serikali mbili.


Mh. Yasmini, hakubaliani na rasimu hii maana kuwa na shirikisho ni kuunga muundo wa serikali tatu.

Anasema yeye ni muumini wa serikali mbili na anasema waasisi wetu walikuwa na nia njema kuunda serikali mbili.

Anasema kutaka serikali mbili ni kudumisha umoja wetu na kuleta maendeleo baina yetu.

Anawaomba wajumbe kukubaliana kwa kina suala hili na anasema serikali tatu ni kuongeza mzigo kwa wananchi.

Tunu ya taifa anapendekeza lugha ya taifa iwe kiswahili na lugha nyingine zaidi ya kiswahili zitumike pale kwenye uhitaji.

Anazungumzia pia sikukuu za kitaifa,anasema mwaka wa kiislam uanishwe katika siku zinazotambuliwa kitaifa.

Anaunga mkono hoja ya serikali mbili.

mh. Shamim Khan,anasema kuwa BAKWATA inapendekeza serikali tatu ila akashtushwa na habari hizo mpaka kuwasiliana na viongozi wakubwa wa bakwata.

Anasoma maelezo yanayosema kuwa bakwata kupendekeza muundo wa serikali 3 ni uongo,hakuna sehemu bakwata imependekeza muundo wa serikali tatu au muundo wa serikali.

Anasema bakwata wao wameomba mahakama ya kadhi na kujiunga na OIC.

Bakwata inasema kuna mapendekezo hakuna ambayo yanataka mahakama ya kadhi ishughulikie masuala na ndoa,mirathi na iwezeshwe na serikali ila anashangaa hayo maoni hakuna.

Anasema yeye kama Mrs khani ni muumini wa serikali mbili na pia anaomba ieleweke bakwata haijazungumzia muundo wa serikali tatu.

Mh. Bernadetha Mshashu anaanza kwa kusema ni muumini wa serikali tatu.

Anasema kuna watu wamezidi mipaka hasa jana kwa kuwadanganya watanzania kwa kusema muungano si halali kumbe nia yao ni kuuvunja muungano,na watu hao wakawa na mapenzi ya ghafla kwa watu wa zanziba kumbe nia yao ni kujenga chuki.

Anasema kuwa kuna mjumbe alisema waasisi wetu hawakuwa na mamlaka na muungano si halali.

Anazungumzia kuwa waasisi wetu waliweza kuunganisha makabila zaidi ya 120 na kuwa na amani,SA wanamuenzi tata Madiba lakini anashangaa sisi huku tunawabeza waasisi wetu.

Anasema muundo wa serikali tatu sio mapendekezo ya serikali tatu.Anazungumzia kuhusu takwimu walizopewa kwenye vitabu vya utoaji wa maeneo na kusema kuwa takwimu hizo zina walakini na hazina uwiano.

Jumla ya watu waliotoa maoni hawana uwiano na population ya sehemu husika.

Anamalizia kwa kusema maoni ya wengi ni serikali mbili na serikali tatu ni mzigo kwa wananchi.Anasema kama hela za kuudumia hiyo serikali tatu zipo basi zipelekwe kwenye huduma nyingine muhimu.

Mh. Omary Ally, Anaanza kwa kuunga mkono muungano wa shirikisho la serikali tatu kama haiwezekani basi turudi kwenye muungano wa mkataba.

Anasema tanzania kuna matatizo mengi ila wananchi wamekuliana nayo wakidhani watapata suluhisho kwenye katiba mpya.

Anasema kama ccm walikuwa wanajua wanachokifanya kulikuwa kuna haja gani ya kuanzisha mchakato mzima wa kupata katiba mpya?.

Anashukuru wazee wetu kwa muungano lakini anasema huu muungano ni wa namna gani? Kumekuwa na malumbano mengi katika muungano na kuna watu wamepoteza maisha na kazi kwa kujadili muungano huu.

Anasema hakuna njia nyingine ya kuimarisha muungano huu zaidi ya muundo wa serikali tatu.

Anasema kuwa kilichotokea mwaka 1964 ni tanganyika kuitawala zanzibar hivyo haoni ajabu watanganyika kuusifia muungano huu,atamshangaa mzanzibar kuunga mkono muungano huu wa serikali mbili maana unawanyonya sana.

Anasema kama muundo wa serikali tatu ukishindikana basi wakirudi zanzibar watapigania muundo wa muungano wa mkataba.

Mh. Marina Joel Thomas,anakubaliana na wajumbe walio wengi wa kamati no 7,

Anazungumzi kifungu kinachozungumzia muungano wa tanganyika na zanzibar,hivyo anakubaliana na muundo wa serikali mbili na anakataa muundo wa muungano wa shirikisho.

Anazungumzia ibara inayozungumzia muundo wa muungano.

Anasema serikali mbili kweli ina changamoto lakini muundo wa serikali mbili sio suluhisho la changamoto bali ni kuweza kupambana na changamoto zilizopo.

Muundo wa serikali tatu unawagawa wananchi na ananukuu maneno ya mwalimu Nyerere kuhusu ''Dhambi ya Ubaguzi''.

Anasema kuwa suala la lugha hapa bungeni ni lazima lugha inayotumika iwe ya kueleweka na nidhamu.Anasema jana kuna mjumbe alisema kuwa rais Kikwete ni ''kigeugeu'' lugha ambayo sio nzuri kwa viongozi wetu na alitegemea mwenyekiti kuchukulia hatua.

Tunu za taifa anasema lugha ya taifa iwe ya kiswahili.

Mh. Bahati Ally Abeid anaanza kwa kusema ni muumini wa serikali mbili maana serikali mbili imeleta upendo na tanzania nia inajulikana dunia nzima kwa amani kutokana na muundo huu wa serikali mbili.

Anasema wapinzani waache kuwatilia maneno watanzania kuhusu serikali tatu,wananchi wanataka maendeleo.

Serikali tatu anaiona kama mdudu kupe maana inamnyonya damu binadam,anasema hakuna serikali isiyo na vyanzo vya mapato ikaitwa serikali.

Nchi hii ni ya demokrasia na vyama vingi hivyo anawaomba wapinzani watulie maana nchi hii ni ya amani.

Anasema waasisi wametuonesha njia nyeupe ya muungano maana unatuletea uchumi na kila mtanzania ana uwezo wa kwenda kila ncha ya nchi kutafta.

Anasema kuwa kauli ya Chiku Abwao kuwa muungano huu bora uvunjike ni kauli ya kijinga na kugawa watanzania,kuna wazanzibar washajijenga maisha Tanzania bara ikiwa muungano utavunjika huyu mtu ataenda wapi?

Anasema muungano wa serikali mbili ndio utakaotupeleka mbele na vizazi vyetu.


mh. Anastazia Wambura
, anasema kazi ya tume ilikuwa nzuri na ya kupongezwa na walijitahidi kadri walivyoweza.

Anasema yeye ni muumini wa amani na upendo na haungi mkono muundo wa serikali tatu bali serikali mbili.

Pia anasema kuwa kutokuwepo kwa takwimu za mabalaza ndio kunasababisha awe muumini wa serikali mbili lakini pia mabalaza mengi yalipendekeza muundo wa serikali mbili.

Anasema takwimu za mabalaza haya hazikuletwa kwenye BMK ili ziweze kufanyiwa kazi badala yake maoni yao yakapotea.

Mh. Agustino Mrema, anasema anaomba azungumze kama mpinzani,mwenyekiti wa TLP na mtu aliyekuwa na nyadhifa kubwa katika nchi hii.

Anasema kuwa muundo wa kuwapeleka katika hatua nyingine ni muundo wa serikali mbili.

Anazungumzia machafuko yaliyotokea Zanzibar na kule Arusha na kusema kuwa kwa usalama wa nchi ili kuleta amani basi muundo wa serikali mbili ni sahihi.

Anasema serikali ya tatu itakuwa tegemezi isiyo na vyanzo vya mapato,isiyo na jeshi haiwezi kufika kokote itapotea tu.

Anazungumzia takwimu za kilimanjaro kwa waliopiga kura ya muundo wa serikali basi wengi walikubaliana muundo wa serikali mbili.

Anasema watu wa vunjo na kilimanjaro kwa ujumla wanataka maendeleo na anasema anawaomba wananchi kuunga mkono muundo wa serikali mbili.

Mh.Said Zubeiry,anaanza kwa kutounga mkono rasimu hii ya katiba hasa sura ya 1&6,anasema zanzibar hakuna aliyezungumza suala la serikali tatu ila walipendekeza serikali mbili na muundo wa mkataba.
 
'MTAGHARAMIA': Mfumo wa Shirikisho ni mzigo kwa wananchi kwani huenda kodi ya kichwa ikarudi kulipia gharama, N/Waziri wa Fedha M.Nchemba asema punde via TBC1.
 
Wachangiaji wawili wameshachangia tayari bi fahalia na mh mbarooku wote kutoka zanzibar kwa pamoja wanaunga mkono muundo wa serikali mbili nakupinga muundo wa serikali tatu.
 
Dah watakata hadi kodi ya mikono eti, ngoja waanze fatilia tv
 
Vitisho vya nini!!!????
Mikataba ya madini ikipitiwa upya na vyanzo vingine vikiimarishwa itapatikana tu!!!!

What if watu wako tayari kwa kodi ya kichwa!!!!??????


Kama kweli kasema hivyo basi tuna shida kubwa sana ya uongozi katika hii nchi
 
Wachangiaji wawili wameshachangia tayari bi fahalia na mh mbarooku wote kutoka zanzibar kwa pamoja wanaunga mkono muundo wa serikali mbili nakupinga muundo wa serikali tatu.

ccm joka lenye sumu linagonga kila linaye jisikia kumgonga hao tayari wameshatishwa na wametishika.

BACK TANGANYIKA
 
Akichangi kwa hisia kali, huku akizomewa na mashabiki wa serikali 2 ambao wengi wao ni CCM. Jana Mjumbe wa BMK kutoka Zanzibar Mhe. Rukia Salum alimunanga Kikwete na Watanganyika wote, pale alipodai kwamba, Zanzibar ni NCHI. Ndiyo maana Jakaya Mrisho Kikwete alipokwenda kwenye sherehe za Mapinduzi ZNZ aliingiwa kwanza uwanjani na kuketi kitako na kumusubiri mwenye nchi aingie Mhe. Dr. Shein. Mwenye nchi alipoingia alikwenda kukagua gwaride la majeshi ya ulinzi na usalama ya Zanzibar. Baadaye majeshi hayo yalikula kiapo kwa Dr. Shein. Aidha Mhe. Rukia aliendelea kusema kwamba, hata wakati wa kutoka uwanjani MWENYE NCHI Dr. Shein alitoka wa kwanza huku akimuacha Kikwete ameketi kitako jukwaani na wageni wengine. Aidha Mhe. Rukia aliendelea kudai kwamba ZNZ ina wenyewe na ni Wazanzibari, hivyo Watanganyika tukome kupotosha kwamba ZNZ sio nchi. Mhe Rukia alienda mbali zaidi kwa kudai kwamba hayati Karume hakuuliwa na Shamte, bali aliuliwa na Mwanajeshi wa JWTZ aitwaye Hamudi, hivyo kifo cha Karume aulizwe JK Nyerere kwasababu Nyerere ndiye alikuwa Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya JMT. Pia akaendelea kumtuhumu Nyerere kuwa alikuwa na tabia ya kuwahifadhi watuhumiwa wa UHAINI wa Zanzibar na kwapata vyeo kwenye SMT. Aidha aliendelea kudai kwamba zaidi ya 61% ya Wazanzibari wanataka Serikali ya Mkataba ambayo ni sawa na serikali 3 na mkataba wenyewe ni KATIBA YA JMT ya serikali 3. Pia aliwashangaa wazanzibari ambao ni wajumbe wa BMK kwamba wanaoshabikia muundo wa serikali 2 wakiwa Dodoma. Lakini wakirudi ZNZ serikali 2 wanazisemea chooni au visimani. Akamalizia kwa kibwagizo kwamba SERIKALI 2 HAZIKUBALIKI WALA HAZIVUMILIKI ZNZ. Kusema kweli Mhe. Rukia aliongea kwa HISIA KAL SANA japo alikuwa anazomewa na CCM. Kama kweli Kikwete ni Mtanganyika na ni Amri jeshi mkuu wa majeshi ya JMT inabidi aone aibu na kuchukua hatua. Aidha akubari awaachie Wazanzibari nchi yao. Au basi atumie nguvu kuunda serikali 1.
 
Mchangiaji wa tatu ni mwakilishi wa cuf anaunga mkono muundo wa serikali tatu huku akigongo mipasho ya ajabu.
 
Akichangi kwa hisia kali, huku akizomewa na mashabiki wa serikali 2 ambao wengi wao ni CCM. Jana Mjumbe wa BMK kutoka Zanzibar Mhe. Rukia Salum alimunanga Kikwete na Watanganyika wote, pale alipodai kwamba, Zanzibar ni NCHI. Ndiyo maana Jakaya Mrisho Kikwete alipokwenda kwenye sherehe za Mapinduzi ZNZ aliingiwa kwanza uwanjani na kuketi kitako na kumusubiri mwenye nchi aingie Mhe. Dr. Shein. Mwenye nchi alipoingia alikwenda kukagua gwaride la majeshi ya ulinzi na usalama ya Zanzibar.

Baadaye majeshi hayo yalikula kiapo kwa Dr. Shein. Aidha Mhe. Rukia aliendelea kusema kwamba, hata wakati wa kutoka uwanjani MWENYE NCHI Dr. Shein alitoka wa kwanza huku akimuacha Kikwete ameketi kitako jukwaani na wageni wengine. Aidha Mhe. Rukia aliendelea kudai kwamba ZNZ ina wenyewe na ni Wazanzibari, hivyo Watanganyika tukome kupotosha kwamba ZNZ sio nchi.

Mhe Rukia alienda mbali zaidi kwa kudai kwamba hayati Karume hakuuliwa na Shamte, bali aliuliwa na Mwanajeshi wa JWTZ aitwaye Hamudi, hivyo kifo cha Karume aulizwe JK Nyerere kwasababu Nyerere ndiye alikuwa Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya JMT. Pia akaendelea kumtuhumu Nyerere kuwa alikuwa na tabia ya kuwahifadhi watuhumiwa wa UHAINI wa Zanzibar na kwapata vyeo kwenye SMT.

Aidha aliendelea kudai kwamba zaidi ya 61% ya Wazanzibari wanataka Serikali ya Mkataba ambayo ni sawa na serikali 3 na mkataba wenyewe ni KATIBA YA JMT ya serikali 3. Pia aliwashangaa wazanzibari ambao ni wajumbe wa BMK kwamba wanaoshabikia muundo wa serikali 2 wakiwa Dodoma. Lakini wakirudi ZNZ serikali 2 wanazisemea chooni au visimani.

Akamalizia kwa kibwagizo kwamba SERIKALI 2 HAZIKUBALIKI WALA HAZIVUMILIKI ZNZ. Kusema kweli Mhe. Rukia aliongea kwa HISIA KAL SANA japo alikuwa anazomewa na CCM. Kama kweli Kikwete ni Mtanganyika na ni Amri jeshi mkuu wa majeshi ya JMT inabidi aone aibu na kuchukua hatua. Aidha akubari awaachie Wazanzibari nchi yao. Au basi atumie nguvu kuunda serikali 1.
 
Mchangiaji namba tatu...viongozi wa zanzibar ni wanafiki na njaa ndio inawasumbua na kuwafanya wawe wasaliti kwa wenzao
 
Silima anasema:
mimi ni muumini wa Serikali mbili, chini ya mfumo huu utulivu umeenea kote Nchini na tumeishi kwa furaha.
Wazo la serikali tatu sikubaliani nalo kwa sababu Serikali mbili zina matatizo twende ya tatu hilo sijalielewa. Ukiwa Zanzibar si ajabu kuwasikia wazanzibar wenzangu wanasema Watanzania waondoke. Mtu akikamatwa na madawa Zanzibar hawasemi Mtanzania kakamatwa bali wanasema Mzanzibar au Mpemba kakamatwa.

Nataka serikali mbili ambazo zitafanyiwa marekebisho. Kama mzanzibar naona kuna mambo nataka yafanyiwe marekebisho
1. Nafasi ya Rais wa Zanzibar.
2.gharama za muungano.
Miaka michache ijayo ushuru wa forodha hautaweza kusaidia Nchi yetu. kamaliza
 
kwann kwenye kambi ya serikali2 ni ccm watupu?lkn kwenye kambi ya serikali3 wako baadhi ya wana ccm kama Lugora,Filikunjombe. Inamaanisha mkiwa ccm lazima mfikiri kama mwenyekiti wenu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom