Slaa awalipua Rostam, Riziwan

Slaa awalipua Rostam, Riziwan

Kumbe Dr Slaa ndio Mwalimu wa Kuzomea! Hopeless!

Si afadhali akifundisha kuzomea, kuliko wale wanaofundisha kuiba?
au kuliko wale wanaowafundisha watu kuchukua mapanga na kupigana kama nchi zingine!

You should be proud of him!
 
Wakishaachia ngazi hao wanaotajwa, Dr Slaa au CHADEMA watanufaika vipi? Hakuna namna nyingine ya kuzi-handle hizi tuhuma za mafisadi wa CCM na serikali yake NCHI ikanufaika?

haki na dhuluma can not co-exist
Mapacha wamefanya lipi la ajabu ndani ya CCM mpaka waondoke??? SIO HAKI NI KUWADHULUMU
Lingekuwa jambo la haki CCM msingejivutavuta kuwataja hadharani wanaotakiwa kuondoka
Currently Nape ameshaanza kutoa statment zilizo njee na yaliyoamuliwa Dodoma mwisho wa siku atakubali yaishe
 
Hapo ndipo watu wanapo muona dokta amechanganyikiwa, maneno ya Salva Rweyemamu aliyokwisha yatoa kuwa dokta ameanza kuchanganyikiwa ndio yanaanza kuthibitika kwa kweli.
 
Dokta acha wivu wa kike fanya kazi na ww upate hela, ww wenzako wanachacharika kufanya biashara na kupata kipato unawaonea wivu !:director::director::director::director:
 
Jamani tusiyapuuzie haya! Miaka hamsini toka tupate uhuru tuna sababu zipi za msingi za kujitetea kwa hali tuliyo nayo? Miongoni mwa aliyosema Nyerere ni kuhusu maadui watatau wanaotusumbua- Ujinga, Maradhi na Umasikini. Watu wanajitokeza kutupa mwanga kuhusu namna ambavyo watu fulani wanatukwamisha kwa uroho na ulafi wao, halafu wanajibu wengine, kwa kugubikwa na adui mkuu huyo ( ujinga) wanataka tuyapuuze ati hayana ushahidi! Ama kweli adui huyu ataendelea kutusumbua sana! Hamna hata aibu wala conscience?
 
Ccm wamechoka hawana mpya,wamepwaya kila kona bado kidogo hata familia zao zitawachoka,wewe unaekisaport chama hiki(ccm)hivi unaona sawa namna nchi ilivyo tangu tupate uhuru?Ukishindwa kujibu nenda Loliondo kwa Babu
 
Ccm wamechoka hawana mpya,wamepwaya kila kona bado kidogo hata familia zao zitawachoka,wewe unaekisaport chama hiki(ccm)hivi unaona sawa namna nchi ilivyo tangu tupate uhuru?Ukishindwa kujibu nenda Loliondo kwa Babu
 
Ajiulize watoto wa masultani (uchwara) wako wapi...aanze tu na karibuni pale kwa Saddam, aje Misri kwa kina Gamal & Alaa Mubarak, soon to be followed by Saad Gadhafi.

Hakuna giza linaloweza ficha uchafu wao.....historia iliamua kuhukumu hivyo. Kila kitu kitawekwa peupe. Na mwendo ndo ushaanza sasa

Kwendeni zenu. Hao masultani unaowataja waling'ang'ania madarakani miongo kadhaa kama Nyerere mnayemtukuza. Kulikuwa na chaguzi kama za enzi ya Nyerere, chama kimoja na mgombea mmoja. Sasa msitake kuwafananisha hao madikteta na JK kwani nchi hii kila miaka 5 wananchi wanapewa fursa ya kuchagua viongozi wao tena kwa mtindo wa ushindani. Sasa kama hizo ahadi zenu za mfuko wa cement 5000 na treni ya umeme kutoka Mwanza mpaka Dar wapiga kura hawanunui, hilo ni tatizo lenu. Msichanganye magimbi na dengu hapa.
 
Ulemavu wa akili ndiyo huu. Mtu akikuzushia uongo basi lazima uende mahakamani la sivyo ni ukweli. LAKINI unatishiwa kuuawa lakini hakuna kwenda polisi wala mahakamani. Sasa huu kama siyo ulemavu wa akili basi ni UNAFIKI wa kiwango cha juu kabisa.
 
Masikini CCM, huu wimbo UMEWAGEUKA....

Slaa kweli ni VUVUZELA maana amewapulizia na sasa HAWAELEWANI..........

Kweli mla ni mla leo, mla jana kala nini?

Piiii Piiiiii----- Hawaelewani. Marlaw kweli ni GUNDU kwa CCM. Wasimwingize tena kwenye kampeni.

Pipiiiiiiiiiiiiiiiiiiii Piiiiiiiiiiiiiiiiiii Hawaelewani...................... kiduku kiduku... Ehh dada jiachie


Wimbo umewageuka-------CDM wameanza kupiga honi-- Pii pii hawaelewani----------CCM Hayooo hayaelewani---CCM RACHEL na CCM-Magamba hayoooo hayaelewani---------jamani siyo mimi ni Marlaw.
 
Last edited by a moderator:
Swali na hoja nzuri... lakini nadhani hoja isiwe ubilionea, bali ameupataje

Labda anatumia majini kuupata hivyo we cant justify, but if he abuses powers, then he has to answer...

My point here is that not every billionaire is fisadi
lo, naona wadau mmemkalia vibaya dogo, atachomoka hapa kweli!!???? Inaelekea kila mtu alikuwa akisubiria ni nani alianzishe ...tuwekeeni picha hata moja basi ya 'fixed assets/investments'
 
Kama Rostam mapato yake bilioni 280 yeye DR Slaa inamuuma nini??

Kwani kuna limit ya kiasi cha pesa anazoweza kupokea mtu mmoja kwa mwaka kwenye Tanzania huru??

Atusaidie kujua alipoyapata. Huwezi kuwa mbunge wa Igunga kwa miaka yote hiyo uwe na pesa hizo wakati wananchi wako ni masikini kiasi hicho. Naona azimio la Arusha limeshakufa siku nyingi. Rostam atueleze anazipataje na Tax zake amelipa kiasi gani. Tuanzie hapo
 
Ulemavu wa akili ndiyo huu. Mtu akikuzushia uongo basi lazima uende mahakamani la sivyo ni ukweli. LAKINI unatishiwa kuuawa lakini hakuna kwenda polisi wala mahakamani. Sasa huu kama siyo ulemavu wa akili basi ni UNAFIKI wa kiwango cha juu kabisa.

Rostam anauwezo wakujibu source ya hizo hela na atuhakikishie analipa Tax. If not tunahitaji hela hizo ziende kwenye shughuli za maendeleo hayo mambo mengine watamalizana na Slaa sijui police au mahakamani.
 
si lazima yeye aende mahakamani...ame whistle blow na sasa ni kazi ya dola kuthibitisha mbivu na mbichi...
 
mmmmmhhhh kumbe ana utajiri tayari???? Wengine tumefanya kazi karibu tunastafu hatujaweza hata kujenga kibanda.....kweli nchi hii imeliwa kisawasawa halafu wengine bado wanawatetea mafisadi....jamani amkeni, imetosha kudanganyika

Mkuu hilo ni tatizo lako binafsi kabisa na wala usiisingizie serikali.

Wasomi wengi wamekuwa na uzembe mkubwa wa kutovishughulisha kichwa vyao na kutafuta vyanzo vingine vya mapato halali, kuna opportunities nyingi sana katika nchi hii, tatizo kubwa tulilonalo ni kuwa wasomi wetu wanaridhika na kuajiriwa tu kwa mishahara ya kujidharirisha badala ya kuanza sasa wao kujiajiri na kuwaajiri watu wengine.

Usipotoka kwenye hiyo mindset,kilasiku utakuwa ni mtu wakulalamika tu, na uzee wako utakuwa ni wakukatisha tamaa sana.
 
CCM oyeeee. Magamba juuuuuuu


Oooooyeeeeee..... tatizo letu
wa tz.. ni wazuri sana kupiga kelele zisizo na madhara.. na mtaona CCM itavyoshinda kwa kishindo 2015...... kelele za Silaha.. na za chura... Mtu mwenyewe padri....
 
Hapo ndipo watu wanapo muona dokta amechanganyikiwa, maneno ya Salva Rweyemamu aliyokwisha yatoa kuwa dokta ameanza kuchanganyikiwa ndio yanaanza kuthibitika kwa kweli.

Kuna viashiria vya hali hiyo,.

Yupo busy sana kutoa single zilizojaa majina bila contents za kutosha, usishangae kesho akiwa kwa wanavijiji wasiojua ata GB ni nani akakutaka umueleze vipesa vyako umevipata wapi wakati angeweza tu kukuuliza kwa simu na ukamjibu.

Anatafuta umaarufu kwa vitu cheap sana!!
 
Back
Top Bottom