Slaa awalipua Rostam, Riziwan

Slaa awalipua Rostam, Riziwan

Tumeshawajua janja yao,ukipeleka mahakamani wewe ukiwa mshitaki, obviously watahitaji evidence ulizonazo, watazikalia huku either wanazichakachua au la wakishindwa kuchakachua basi kesi inapigwa dil dale mpaka kesho na wahati huo HURUHUSIWI KUZUNGUMZIA TENA kesi iliyopo mahakamani. Dawa yao ni kuwaweka wao wawe washitaki katika jitihada za kujisafisha, wakati huo hawana clue kuwa una evidence kiasi gani.
Remmy,kwani wao wajinga hata wakubali kuchafuliwa hivyo? Si wapo waliotishia kushitaki kabla ya ku-mute bila maelezo,na baadhi yao kwa bahati nzuri wakajitokeza katika listi ya sacrifice ya Alex Sterwat Asseyers na wanaripoti kisutu hata leo? Kwani unadhani UWT au TAKUKURU hawana hizo evidences au wakiamua kuzipata unadhani watazikosa?
Ipo siku muafaka hizo evidences tutazihitaji tuu (when they matter most),wenzetu wa misri muda wao umefika na wanzitumia haswaa, baba na mwana wapo chini ya mkono wa sheria. Sisi kwa sasa hebu tugonge beats kisha wao wachague miondoko.
Hivi kama ana ushahidi si awapeleke mahakamani jamani, kwa niaba ya wananchi. Achukue hatua zaidi ya kutaja tu.
 
DR Slaa anaisafisha mno CCM utadhani bado ana mapenzi nayo! Kwa nini anakuwa na hati miliki na ushahidi anaopewa na Watanzania wanaomwamini? Nakuomba Dr Slaa, kwa kadri utakavyoona inafaa na ushahidi upo wa kutosha, uwakabidhi PCCB au POLICE. Wakishindwa kuufanyia kazi uje kwa wananchi utuarifu. Tunataka kwenda mbele zaidi ya hapa pa kutajana majina tu. CCM ina wanachama wengi mno. Wakiwaondoa hao unaowataja wana akiba kubwa tu ya VIONGOZI ingawa wengi ni wachafu. CHADEMA sasa hivi haiwezi kuivunja kamati kuu yake ikabaki salama. CCM wanaweza kuivunja hata mara tano. CCM ni kama BRAZIL kwa mpira wa miguu. Ina wachezaji wengi sana.
 
mh humu naona wanamagamba wameingia. hii kasi ya kuwatetea mafisadi siyo ya kawaida humu jamvini.ndio walivyotumwa kufanya toka Dodoma siku ile ama? maana naona kina MS wanapata wenzao sasa.
 
Wakishapoteza kinga waliyo nayosasa ni rahisi hatua zingine za kisheria kuchukuliwa.
Mfano unaona swala la Dowans linavyoihangaisha serikari. Iwapo wahusika wataweza kuanikwa wazi, ni rahisi hata nguvu ya umma kuzuia wasiendelee kuchakachua uchumi wa nchi hata kama serikari haina nia ya kufanya hivyo.
 
Tena wanufaikaji sio Dr Slaa na Chadema. Kwa ufinyu wa akili ni rahisi kufikiri CHADEMA kama chama wanatafuta faida yao wenyewe.
 

Senior Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png



Join Date : 16th February 2011

Hivi Kwenye Hiyo habari yenye zaidi ya paragraph 6 hilo la kuzomea tu ndo umeliona
ama kweli umetumwa kuja kuwakilisha chama cha Magamba!!!

Lakini sikushangai ni umejiunga siku mbili kabla ya Valentine day kwa hiyo mawazo yako yatakuwa ya Ki-valentine valentine.

Basically alijiunga mwezi wa chama cha magamba
 
Kama Rizwani anaona ameonewa aende yeye mahakamani mimi nimemaliza kesi kwenye mahakama ya wananchi".

This is too low kwa mtu anayetaka kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dr.Slaa!!hivi uwezo wako wa kufikiri kisiasa unaishia kwenye kutajataja tu majina?hauna habari njema ya matumaini yatakayoletwa na utawala wa Chadema?hauna habari njema za namna gani maisha yao yataboreshwa na utawala mbadala?namna gani heshima na ustawi wa nchi utarutubishwa?

Nasikitika kuwa bado sijaona tofauti ya tactics zako na zile alizotumia Mrema 1995-2000 na wote tunajua matokeo yake,ulipaswa ujue kuwa hizi sio strategy za kudumu na hazitaweza kukufanya usurvive kisiasa baada ya uchaguzi wa 2015 ambapo CCM watakuwa na mgombea mpya huku wakiwa wamejivua gamba la ufisadi kwenye mahakama ya wananchi.

Graphy ya umaarufu wako inazidi kushuka, huu ni wakati unaokupasa kuanza kubadilisha mbinu zako kabla haujafikia kwenye point of no return.
 
Luteni that was a nice way to present it! Nimeipenda Mkuu!
 
Tumechoshwa na wanyonyaji wa chama cha magamba,endelea na kazi Dr. Walidhani siri kumbe sio siri tena,tunakushuru kwa ujasiri wako.
 
<br />
<br /> nyerere alipoliachia kanisa kufanya litakavyo hata chumvi ilikuwa kipusa .ukivaa jeans unakodolewa macho kama vile umevaa dhahabu

Tatizo lenu ni kwamba duniani kote mekuwa second class sio kwa kupenda bali ni kwa sababu maalumu. Ishamel at work!
 
Masikini CCM, huu wimbo UMEWAGEUKA....

Slaa kweli ni VUVUZELA maana amewapulizia na sasa HAWAELEWANI..........

Kweli mla ni mla leo, mla jana kala nini?

Piiii Piiiiii----- Hawaelewani. Marlaw kweli ni GUNDU kwa CCM. Wasimwingize tena kwenye kampeni.

Pipiiiiiiiiiiiiiiiiiiii Piiiiiiiiiiiiiiiiiii Hawaelewani...................... kiduku kiduku... Ehh dada jiachie

 
Last edited by a moderator:
Thursday, 21 April 2011 08:17

123ridhiwan.jpg
Ridhiwan Kikwete

Geofrey Nyang'oro, Singida
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk Willbroad Slaa amesema chama chake kinajipanga kuhoji kile alichodai utajiri mkubwa wa ghafla wa Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji na pia Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).

Dk Slaa alisema hayo jana katika Kijiji cha Ikungi, mkoani Singida alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara.

Alisema anajua kuwa mjumbe huyo (jina tunalihifadhi kwa kuwa jitihada za kumpata kujibu tuhuma hizo hazikufanikiwa), licha ya umri wake mdogo hivi sasa ana fedha nyingi.

Katika mkutano huo Dk Slaa alimtuhumu kuwa na utajiri uliopindukia ambao alisema haulingani na umri wake.

Dk Slaa alisema chama chake kina shaka na wingi wa fedha alizonazo kijana huyo na kwamba atahakikisha kwamba kigogo huyo anaiambia Chadema na Watanzania alipozipata.

Alisema kijana huyo alimaliza masomo yake muda mfupi uliopita, lakini tayari amekuwa bilionea akisisitiza kuwa chama chake kitahoji alipopata mabilioni hayo.

"Ninajua kwamba ana fedha nyingi, lakini huyu alikuwa mtoto wa shule juzi tu. Leo amekuwa bilionea! Atatuambia amepata wapi hizo fedha, Chadema tutahoji ni wapi amezipata," alisema Dk Slaa.

Dk Slaa pia alizungumzia kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuwa kelele za wapinzani hazimnyimi usingizi na kusema watahakikisha halali.

Mgombea huyo wa urais kwa tiketi ya Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana alitoa kauli hiyo alipozungumzia ushindi wa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu akisema umeimarisha ngome ya upinzani bungeni.

"Rais Kikwete alisema kelele za upinzani hazimnyimi usingizi, lakini kwa kumchagua Lissu mmeongeza nguvu ya upinzani na sasa hatalala," alisema na kuongeza:

“Ujumbe wangu kwenu ni kwamba sasa mmemchagua mbunge jasiri anayeweza kumwambia Mwanasheria Mkuu wa Serikali, mbele ya Waziri Mkuu kuwa amekuwa mvivu kusoma.”

Alisema kutokana na ujasiri huo wa Lissu sasa miswada mibovu haitapelekwa bungeni.

Awali, akizungumza katika mkutano huo, Lissu alisema Halmashauri ya Wilaya ya Singida imetenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo akisema kuwa ni mara ya kwanza fedha hizo kutengwa huku akijigamba kwamba ni kutokana na wapinzani kubana mianya ya wizi
 
Na bado....CCM kujivua gamba is a mockery....gamba la nyoka likitoka jipya linaota na nyoka anabaki kuwa nyoka, hawi njiwa kwa kujivua gamba; na essence/essential elements are still there, so kama ni kutafuta popularity, watafute strategy nyingine sio kuvua gamba...that is danganya toto jinga na sisi si watoto, we scrutinize, analyze and weigh options
 
Maskini....namhurumia sana dogo Nape, sijuwi kama anaujua mdundo wa ngoma aichezayo!
 
mmmmmhhhh kumbe ana utajiri tayari???? Wengine tumefanya kazi karibu tunastafu hatujaweza hata kujenga kibanda.....kweli nchi hii imeliwa kisawasawa halafu wengine bado wanawatetea mafisadi....jamani amkeni, imetosha kudanganyika
 
Ni kama watoto wa Hosni Mubarak; they have 2 pay what dad gave them so does it mean Lau Masha atachunguzwa pia?

Lau is the Source... WOW Long Live Tanganyika
 
• Asema anapokea bil. 280/- kwa mwaka, ataka akamatwe

na Joseph Senga



KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza mapato ya Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), kwa kile alichodai yana uhusiano mkubwa na ufisadi.

Dk. Slaa aliyasema hayo juzi jioni katika mkutano wake mjini Igunga, mkoani Tabora katika mwendelezo wa ziara zake.

Alisema mapato ya Rostam kwa mwaka yanafikia sh bilioni 280, hivyo TAKUKURU haina budi kumkamata na kumchunguza kwani aliwahi kutangaza kuwa hana shida ya kuwa kiongozi au kung’ang’ania madaraka yoyote, kwani pesa alizonazo zinamtosha.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, ikiwa TAKUKURU haitamchukulia hatua Rostam, atawashawishi wananchi kutotoa ushirikiano wowote kwa taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwazomea maofisa wake kila wanapowaona.

Akifafanua tuhuma hizo za ufisadi, alisema kuwa kati ya makampuni 17 yanayosemekana kuwa ni ya Rostam hakuna jina lake hata moja.
Alisema kama Rais Jakaya Kikwete angekuwa na nia ya kweli angemshirikisha kuwakamata mafisadi badala ya kuwapa siku 90 kuondoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, ikiwa Kikwete amewapa mafisadi hao siku hizo kuondoka ndani ya chama pamoja na kuachia ubunge, naye hana budi kujipa siku hizo, kwani naye ni fisadi.

Alisema kujitokeza kwa mmiliki wa Dowans Brigedia Jenerali (mstaafu), Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi, ulikuwa ni usanii wa picha ya Rostam kwani baadaye ndiye atakayelipwa fedha hizo za Dowans.
Alisema CHADEMA haitakubali fedha hizo zilipwe na kwamba itaitisha maandamano nchi nzima kupinga.

Dk. Slaa alisema ufisadi mwingine wa serikali katika sakata hilo la Dowans ni serikali kuweka mawakili watatu kinyemela na kupanga kuwalipa sh bilioni tano.

“Nilimtaja Rostam kuwa ni mmoja wa mafisadi kule Mwembeyanga, naye alinitumia vitisho kwa ujumbe mfupi kuwa nina sekunde chache za kuishi hivyo nipige magoti, nisali. Nilimjibu na nasema …nilizaliwa siku moja na nitakufa siku moja, sitaogopa kusema ukweli,” alisema Dk. Slaa.
Katika hatua nyingine, Dk. Slaa alisema moto uliowashwa na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA) umeifanya serikali ya CCM akiwamo Rais Jakaya Kikwete kushindwa kulala.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ikungi katika Jimbo la Singida Mashariki jana aliposimama kuwasalimia wakati akitokea Singida kuelekea Dar es Salaam, Dk. Slaa alisema Lissu ni mbunge jasiri katika Bunge ambaye amediriki kumnyooshea kidole hata Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema.

Katika hotuba yake hiyo alisema wananchi hawana imani tena na serikali ya Jakaya Kikwete na kama atafanya mchezo hataweza kurudisha imani hiyo wala kumaliza kipindi chake cha utawala.

Alisema mambo mengi yamejitokeza ambayo yamesababisha wananchi kukosa imani naye, yakiwamo ya ufisadi unaofanywa na yeye mwenyewe pamoja na watu walio karibu naye. “Wananchi wanaona yanayofanyika, mtoto wa rais, Ridhiwani Kikwete, amemaliza shule hivi karibuni lakini leo ni bilionea. Haya yote hayawezi kuvumilika hata kidogo.”

Akiwashukuru wananchi wa kijiji hicho, Dk. Slaa alisema si tu kwamba wamemchagua mbunge wa Jimbo la Singida, bali ni mbunge wa nchi nzima na kwamba ni nyundo itakayotumika kuwaponda CCM.

Akizungumzia suala la CCM kujivua gamba, alisema neno fisadi alilianzisha yeye na chama chake na kwamba anayepaswa kujivua gamba hilo ni Kikwete halafu awavue wengine.
 
Back
Top Bottom