Slaa awalipua Rostam, Riziwan | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa awalipua Rostam, Riziwan

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ms Judith, Apr 20, 2011.

 1. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Dk. Slaa afichua mabilioni ya Rostam

  • Asema anapokea bil. 280/- kwa mwaka, ataka akamatwe

  na Joseph Senga

  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza mapato ya Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), kwa kile alichodai yana uhusiano mkubwa na ufisadi.

  Dk. Slaa aliyasema hayo juzi jioni katika mkutano wake mjini Igunga, mkoani Tabora katika mwendelezo wa ziara zake.

  Alisema mapato ya Rostam kwa mwaka yanafikia sh bilioni 280, hivyo TAKUKURU haina budi kumkamata na kumchunguza kwani aliwahi kutangaza kuwa hana shida ya kuwa kiongozi au kung'ang'ania madaraka yoyote, kwani pesa alizonazo zinamtosha.

  Kwa mujibu wa Dk. Slaa, ikiwa TAKUKURU haitamchukulia hatua Rostam, atawashawishi wananchi kutotoa ushirikiano wowote kwa taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwazomea maofisa wake kila wanapowaona.

  Akifafanua tuhuma hizo za ufisadi, alisema kuwa kati ya makampuni 17 yanayosemekana kuwa ni ya Rostam hakuna jina lake hata moja.

  Alisema kama Rais Jakaya Kikwete angekuwa na nia ya kweli angemshirikisha kuwakamata mafisadi badala ya kuwapa siku 90 kuondoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Kwa mujibu wa Dk. Slaa, ikiwa Kikwete amewapa mafisadi hao siku hizo kuondoka ndani ya chama pamoja na kuachia ubunge, naye hana budi kujipa siku hizo, kwani naye ni fisadi.

  Alisema kujitokeza kwa mmiliki wa Dowans Brigedia Jenerali (mstaafu), Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi, ulikuwa ni usanii wa picha ya Rostam kwani baadaye ndiye atakayelipwa fedha hizo za Dowans.

  Alisema CHADEMA haitakubali fedha hizo zilipwe na kwamba itaitisha maandamano nchi nzima kupinga.

  Dk. Slaa alisema ufisadi mwingine wa serikali katika sakata hilo la Dowans ni serikali kuweka mawakili watatu kinyemela na kupanga kuwalipa sh bilioni tano.

  "Nilimtaja Rostam kuwa ni mmoja wa mafisadi kule Mwembeyanga, naye alinitumia vitisho kwa ujumbe mfupi kuwa nina sekunde chache za kuishi hivyo nipige magoti, nisali. Nilimjibu na nasema …nilizaliwa siku moja na nitakufa siku moja, sitaogopa kusema ukweli," alisema Dk. Slaa.

  Katika hatua nyingine, Dk. Slaa alisema moto uliowashwa na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA) umeifanya serikali ya CCM akiwamo Rais Jakaya Kikwete kushindwa kulala.

  Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ikungi katika Jimbo la Singida Mashariki jana aliposimama kuwasalimia wakati akitokea Singida kuelekea Dar es Salaam, Dk. Slaa alisema Lissu ni mbunge jasiri katika Bunge ambaye amediriki kumnyooshea kidole hata Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema.

  Katika hotuba yake hiyo alisema wananchi hawana imani tena na serikali ya Jakaya Kikwete na kama atafanya mchezo hataweza kurudisha imani hiyo wala kumaliza kipindi chake cha utawala.

  Alisema mambo mengi yamejitokeza ambayo yamesababisha wananchi kukosa imani naye, yakiwamo ya ufisadi unaofanywa na yeye mwenyewe pamoja na watu walio karibu naye.

  "Wananchi wanaona yanayofanyika, mtoto wa rais, Ridhiwani Kikwete, amemaliza shule hivi karibuni lakini leo ni bilionea. Haya yote hayawezi kuvumilika hata kidogo."

  Akiwashukuru wananchi wa kijiji hicho, Dk. Slaa alisema si tu kwamba wamemchagua mbunge wa Jimbo la Singida, bali ni mbunge wa nchi nzima na kwamba ni nyundo itakayotumika kuwaponda CCM.

  Akizungumzia suala la CCM kujivua gamba, alisema neno fisadi alilianzisha yeye na chama chake na kwamba anayepaswa kujivua gamba hilo ni Kikwete halafu awavue wengine.


  source: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=29939
   
 2. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  280 bilion kwa kweli hapa ndipo umuhimu wa kuwa na kiongozi kama Dr Slaa huyo RIZWANI kama ni bilioni hiyo n hela ya baba yake anamshikia tu kwa muda,
   
 3. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kumbe Dr Slaa ndio Mwalimu wa Kuzomea! Hopeless!
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza mapato ya Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), kwa kile alichodai yana uhusiano mkubwa na ufisadi.

  Dk. Slaa aliyasema hayo juzi jioni katika mkutano wake mjini Igunga, mkoani Tabora katika mwendelezo wa ziara zake. Alisema mapato ya Rostam kwa mwaka yanafikia sh bilioni 280, hivyo TAKUKURU haina budi kumkamata na kumchunguza kwani aliwahi kutangaza kuwa hana shida ya kuwa kiongozi au kung'ang'ania madaraka yoyote, kwani pesa alizonazo zinamtosha.

  Kwa mujibu wa Dk. Slaa, ikiwa TAKUKURU haitamchukulia hatua Rostam, atawashawishi wananchi kutotoa ushirikiano wowote kwa taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwazomea maofisa wake kila wanapowaona. Akifafanua tuhuma hizo za ufisadi, alisema kuwa kati ya makampuni 17 yanayosemekana kuwa ni ya Rostam hakuna jina lake hata moja.

  Alisema kama Rais Jakaya Kikwete angekuwa na nia ya kweli angemshirikisha kuwakamata mafisadi badala ya kuwapa siku 90 kuondoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kwa mujibu wa Dk. Slaa, ikiwa Kikwete amewapa mafisadi hao siku hizo kuondoka ndani ya chama pamoja na kuachia ubunge, naye hana budi kujipa siku hizo, kwani naye ni fisadi.

  Alisema kujitokeza kwa mmiliki wa Dowans Brigedia Jenerali (mstaafu), Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi, ulikuwa ni usanii wa picha ya Rostam kwani baadaye ndiye atakayelipwa fedha hizo za Dowans. Alisema CHADEMA haitakubali fedha hizo zilipwe na kwamba itaitisha maandamano nchi nzima kupinga.

  Dk. Slaa alisema ufisadi mwingine wa serikali katika sakata hilo la Dowans ni serikali kuweka mawakili watatu kinyemela na kupanga kuwalipa sh bilioni tano. "Nilimtaja Rostam kuwa ni mmoja wa mafisadi kule Mwembeyanga, naye alinitumia vitisho kwa ujumbe mfupi kuwa nina sekunde chache za kuishi hivyo nipige magoti, nisali. Nilimjibu na nasema …nilizaliwa siku moja na nitakufa siku moja, sitaogopa kusema ukweli," alisema Dk. Slaa.

  Katika hatua nyingine, Dk. Slaa alisema moto uliowashwa na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA) umeifanya serikali ya CCM akiwamo Rais Jakaya Kikwete kushindwa kulala. Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ikungi katika Jimbo la Singida Mashariki jana aliposimama kuwasalimia wakati akitokea Singida kuelekea Dar es Salaam, Dk. Slaa alisema Lissu ni mbunge jasiri katika Bunge ambaye amediriki kumnyooshea kidole hata Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema. Katika hotuba yake hiyo alisema wananchi hawana imani tena na serikali ya Jakaya Kikwete na kama atafanya mchezo hataweza kurudisha imani hiyo wala kumaliza kipindi chake cha utawala.

  Alisema mambo mengi yamejitokeza ambayo yamesababisha wananchi kukosa imani naye, yakiwamo ya ufisadi unaofanywa na yeye mwenyewe pamoja na watu walio karibu naye. "Wananchi wanaona yanayofanyika, mtoto wa rais, Ridhiwani Kikwete, amemaliza shule hivi karibuni lakini leo ni bilionea. Haya yote hayawezi kuvumilika hata kidogo."

  Akiwashukuru wananchi wa kijiji hicho, Dk. Slaa alisema si tu kwamba wamemchagua mbunge wa Jimbo la Singida, bali ni mbunge wa nchi nzima na kwamba ni nyundo itakayotumika kuwaponda CCM. Akizungumzia suala la CCM kujivua gamba, alisema neno fisadi alilianzisha yeye na chama chake na kwamba anayepaswa kujivua gamba hilo ni Kikwete halafu awavue wengine.

  Chanzo: Tanzania Daima
   
 5. p

  politiki JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  don't blame the messenger, blame jk who decided to sit on his hands and let his crooks friends destroying the country.
   
 6. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  dah! Kweli noma,wanataka nini zaidi ya hiyo mihela? Jamani tudanganyeni kwa kutujengea nchi yetu.na kuyawezesha maisha bora kwa kila Mtz
   
 7. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280

  Senior Member [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]


  Join Date : 16th February 2011

  Hivi Kwenye Hiyo habari yenye zaidi ya paragraph 6 hilo la kuzomea tu ndo umeliona
  ama kweli umetumwa kuja kuwakilisha chama cha Magamba!!!

  Lakini sikushangai ni umejiunga siku mbili kabla ya Valentine day kwa hiyo mawazo yako yatakuwa ya Ki-valentine valentine.
   
 8. H

  HomeSweetHome Member

  #8
  Apr 21, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 45
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Miasha bora kwa kila fisadi akiwemo JK na mapacha watatu!
   
 9. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #9
  Apr 21, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Dr Slaa siwezi kupinga unachokiongea maana wewe ni miongoni mwa viongozi wa kisiasa hapa Tanzania, je? vipi wananchi tunaweza kuthibitisha kauli zako unazosema tunaomba utuletee na ushahidi na sio maneno maana tunawaelewa wana siasa mulivyo na maneno mengi vinywani mwenu, kama unazo hizo documents za ushahidi wa mapato ya Muheshimiwa RA na RIZ kwa nini musiwatumie wanasheria wenu wa CHADEMA kuwapeleka mahakamani kama muna wasiwasi na source za mapato yao.

  Mengi unayoyaongea ni kwa ajili ya maslahi ya nchi lakini je Rizwan Kumiliki mabilioni ni kitu cha hatari? Naelewa kwa ufahamu wangu Rizwan ni mtoto wa RAIS na baba yake alikuwa waziri katika wizara nyingi sana hapa Tanzania kabla ya kuwa Rais; ninavoelewa mimi Rizwan kumiliki Bilioni moja si kitu cha ajabu, eti kamaliza shule juzi ndio asiweze kumiliki hiyo ela haiingii akilini hata kidogo kwa mtoto wa kimasikini sawa ila Riz sio mtoto wa kimasikini akashindwa kujiingiza kwenye masuala ya kutafuta pesa.

  Kama mna ushahidi wa wizi wa fedha muende mahakamani au kama ni siasa tu basi endeleeni (sikupingi Dr Slaa huwa napenda ila ushahidi wako uko wapi?) tuwekee ushahidi ila tunapomwita mtu fisadi kama Riz kweli tujue ili tusipate dhambi kumjadili mtu bila ya ushahidi.
   
 10. kinja

  kinja Senior Member

  #10
  Apr 21, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni sahihi mawazo yako, kama ni kweli tumekwisha
   
 11. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hapa Dr.Slaa anatupiga fix , Rostam Aziz hawezi kuwa mjinga hivyo!!
   
 12. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #12
  Apr 21, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Duh hii kali
   
 13. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #13
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ok lakini rostam ni mwizi, na kama unakubali hilo unadhani yuko tayari kuachia 280 bilion kwa sababu ya dr slaa?, tumia akili hapo vitisho ni most likely mkuu
   
 14. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #14
  Apr 21, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wewe ndo hopeless kwa kutoelewa mantiki ya yale yanayomfanya Dr. kuhamasisha watu wawazomee ninyi mafisadi na hila zenu za kujiegemeza kwenye vyombo vya dola kuficha utupu wenu.
   
 15. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #15
  Apr 21, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mke wa Mbowe alivyotishiwa kufa alikwenda polisi kushtaki na sasa kesi ipo mahakamani kama kweli Dr Slaa na wewe umetishwa kama utauwawa sasa peleka hizo taarifa polisi sio kuwashtakia wananchi suala lako la kuuliwa.

  RA ni Mtanzania na ana haki ya kumiliki hizo pesa, Dr Slaa naamini wewe ni Dr wa ukweli hasa nilipoangalia kwenye youtube ulipokuwa unamuelezea yule mama kuhusu mtoto wake mlemavu nilifurahi sana juu ya upeo wako wa elimu ya Afya ulionayo lakini je mbona kwenye suala hili la sasa la Riz na RA kutaka kukuuwa mbona huweki vidhibitisho? Tutakuamini vipi?
   
 16. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #16
  Apr 21, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Pepombili,

  Jamvi hili si maahali pa kutoa ushahidi. Kuna mahali pa kutolea ushahidi. Kauli zangu zimetolewa kwenye hotuba ya kuwaelimsha Watanzania, tena in this case wa Jimbo la Igunga Jimbo la Rostam Aziz. Kazi yangu kama Katibu Mkuu katika mikutano ya hasdhara si kutoa ushahidi bali kueleza na kuonyesha uozo ndani ya CCM na Serikali yake ili Watanzania waweze kufunguka macho. Mwenye kuona kaonewa ana mahali pa kutaka "redress" kama anafikiri nilichosema siyo kweli.

  Nilikwisha kueleza kuwa "mahakamakubwa kuliko zote kwa mwanasiasa ni 'wananchi' (Ibara ya 8 ya Katiba). Tuliowataja leo wako mahakamani, Fedha za EPA mlizobishia angalau JK aliutangaza Bungeni kuwa zimerudishwa sehemu (Japo CAG katika Taarifa yake ya Hesabu za Serikali Kuu anasema fedha hizo hadi Machi 2011 hajaona zimeingizwa akaunti gani japo zilihamishiwa TIB June, 20, 2010 (Jambo linalozua utata mpya kabisa katika historia ya ufisadi ikizangatiwa kuwa 2010 ilikuwa mwaka wa Uchaguzi-au zilirudishwa zikaenda tena kwenye uchaguzi kuisaidia CCM au hazikurudishwa kabisa na inakuwa usanii tu).

  Kama Rizwani anaona ameonewa aende yeye mahakamani mimi nimemaliza kesi kwenye mahakama ya wananchi, lakini nadhani ni vema ungelinukuu vizuri "conclusion yangu badala ya kuchakachua statement yangu".

   
 17. Mbutunanga

  Mbutunanga Senior Member

  #17
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 183
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mie ningependa wachapwe viboko kabisa!:sleepy:
   
 18. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #18
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  si bora kuzomea, nyinyi ccm mnawachoma vibaka motto kila kukicha sasa kipi ni bora?
   
 19. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #19
  Apr 21, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ahsante mheshimiwa DR Slaa kwa ufafanuzi wako mzuri.

  Naamini kwamba mnao wanasheria wengi kwenye chama chenu kweli umeshtaki kwa wananchi hilo sio baya je nini mpango wenu juu ya kupeleka ushahidi wenu mahakamani na sisi wananchi ili tuweze kufuatilia na kama ukweli ukithibitisha basi tukuunge mkono Mheshimiwa DR
   
 20. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #20
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mkuu, Dr wa ukweli kaisha kwambia kapeleka kwa mahakama kubwa ambayo ni wananchi sasa unataka apeleke kwenye mahakama za CCM ambazo wanachakachua haki kila siku? Kesi ya Mtikila kuhusu mgombea binafsi hukona jinsi mahakama zinavyokologana, halafu wakilipeleka mahakamani mahakama zitapiga marufuku kuzungumzia ufisadi kwa kisingizio kuna kesi mahakamani au wakatoa sababu kama kwenye kesi ya Mengi, na sisi wananchi tutakosa haki ya kujua nini mafisadi wanafanya maana kesi inaweza kuchukua hata miaka kumi.

  Hongera sana mh Dr Slaa tuko pamoja
   
Loading...