Slaa awalipua Rostam, Riziwan

Slaa awalipua Rostam, Riziwan

siezi bishana nawe bana umeongea point.ndo maana siwamini wanasiasa.alikuepo obama akajidai mtu wa wanyonge kumbe mnafiki mkubwa.anapokea amri kutoka kwa mabanker,oil companies kama agip,chevron,military industries complex wanaenedesha vita ili silaha ziuzwe na makampuni ya mafuta yapate contracter,huku makampuni ya kina dick chen ,HALIBUTON yakipata tenda za kusupply jeshini kuanzia magari,chakula hadi uniform,itakua hapa.we need evidence

Usije tuambia alikuwepo Yesu akaondoka akasema atarejea, miaka 2010 ishapita bado kuja aliowaambia wote weshakufa!!! sasa tuelezee wewe husadiki hadi uone na kugusa? CCM Wote wamefukuza magamba matatu yanayohisiwa ni mafisadi wameamini kwa kusikia wewe upo upande upi?
Hebu Jitokeze!!!! simama! mbele za watuu!! Nimeamini kuwa kiwi haichafui Kiwi Hung'arisha!:A S clock:
 
It's so sad how things like this are soo much in the open but people are scared to even mention a word about it!, up to this day kuna wanafunzi bado wanakaa chini TZ, watu wana mengi ya kujibu mbele za Mungu!
 
It really haults kuona majority ya wananchi ni mafukara haafu hao tuliowachagua wanajineemesha na family zao.
 
Dr Slaa endelea kuwapatia elimu watanzania.tunashukuru sana ipo siku watanzania waliolala wataamka tu na kuujua ukweli
 
Nawakubali sana wanachadema kwa kweli kwa hii kazi tunayofanya sijui mafisadi na CCM watajifichia wapi...?Hii timu ni sahihi kwa mapambano tuwe mstari wa mbele kuwasupport
 
Siamini kama kweli Ridhiwani ni tajiri kwani namjua sana. Hapa mzee umechakachuliwa. Hebu tutajie utajiri wake vizuri

Kweli wewe chechetuka na una mchecheto,ndo mana una chechetuka kila ukiona wafadhili wako mafisadi wanapewa kibano na Dr wa ukweli.Acha kujichetua.
 
wasukuma wakimkana kwamba sio msukuma ndipo nitaelewa lakini km sivyo` basi ni haki yake kula nchi kwani katiba ya ccm iko wazi kuwa mwenye uwezo wa kula nyama nyingi ni yule mwenye kisu kikali.................mwacheni rostamu wetu sisi ccm ametusaidia sana bila yeye kikwete asingeingia madarakani 2005 na km mnavyojua kikwete ametufanyia mengi sana...............mnafikiri tungeweza kupata rais km yeye hapa tz?......kwa hiyo rostamu kasaidia sana nchi hii ni haki yake naye kufaidi matunda ya jasho lake na pesa alizowekeza ccm na serikalini
Pesa zake au zetu tuwe makini jamani wanachota pesa huku wanapeleka huko ndio iwe pesa za jasho lake kha!
 
Nimepewa taarifa kuwa Ridhiwani ni mmoja wa wamiliki wa kampuni ya CAMELOIL na anamiliki malori ya kusafiria mafuta yapatayo 150.....kuna madai kuwa yuko pamoja na watu wanaochakachua mafuta
 
Hongera Dr. Slaa. Huyo Pepombili kaelewe ila katumwa. Jambo jingine ni kuwa kama waliotajwa na kushtakiwa kwa mahakama kubwa ambayo ni Wananchi, wanaona kuwa Dr. Slaa amewazalilisha waende mahakani ili Dr ndo aende na ushahidi. Kama mtu anatuhumiwa na anakaa kimya we utamuelewaje. Kwa busara za Dr. Slaa , pepombili kaanza kujichanganya na kutaka kuwapotosha wengine, Dr kajitokeza na kusawazisha mambo. Sasa na Hao kina Rizwan wajitokeze wapinge tuone kama wataweza kujenga hoja yoyote. DR SLAA ENDELEA HIVYO HIVYO NA kupitia falsafa yako ya nguvu ya umma tumekuwa na ujasiri zaidi where we dare to talk openly. Big up Sir.
 
Ridhiwan anatumia nafasi ya baba yake kujinufaisha,juzijuzi hapa alienda ubalozi wa India na kuomba kuonana na balozi,akapewa fursa,alipoingia akamwambia balozi amekuja kumuona ili amsaidie kwa sababu anataka kufanya biashara na wafanya biashara wakubwa wa India,Balozi akasema maswala ya biashara kati ya nchi na nchi yanaratibiwa na wizara ya mambo ya nje ya nchi husika kwa hiyo aende wizara wa mambo ya nje ili aweze kupewa taarifa huko,yeye akasema Lakini Mimi ni Mtoto wa Raisi Kikwete,Balozi akasema hata akiwa Raisi wa nchi hii anataka kufanya biashara na wafanya biashara wa India itabidi afuate utaratibu wa kidiplomasia ulivyowekwa,yaani ebu fikiria anaenda kutaka apindishiwe sheria na utaratibu kwa manufaa yake
 
Dr. Slaa unatuchezea kiini macho. Kama unajifanya hujui kuwa Chama chako kinafadhiliwa na hao mafisadi wanaofukuzwa CCM basi wewe ni kiongozi wa ajabu saana.

Hivi unamfahamu kiumbe mmoja anayeitwa Yusuf Manji? Je, unajua madhambi yake kwa watanzania? Inakuwaje mumruhusu kiongozi wenu tena mwenye heshima zake ktk jamii kumtetea fisadi huyu? Hili nitalizungumza kwa kirefu siku zijazo maana taarifa nilizokusanya zinatosha kuweka uozo huu hadharani.

Ningeweza kumuelewa Mabere Marando kama angekuwa amejiunga Chadema akiwa tayari ameingia mkataba wa kumtetea fisadi huyu wa kihindi anayewafanya watanzania wajinga na kwa ufukara wao.


Hii ishawahi kujadiliwa hapa JF na ikiwa bayana kuwao Marando ana haki ya kumtetea Manji. Ni mwanasheria na ndiyo kazi yake tofautisha hiyo na siasa au kumtetea kwenye kesi ya wizi au ufisadi ile ni kesi ya kudhalilishana. Hata kama atawatetea wezi wa wa EPA ni haki yake kufanya hivo ila akitoka hapo hapaswi kuwatetea kwenye majukwaa kama mwanasiasa. Ni ngumu sana kuelewa hesabu hii kwetu wabongo.

Umesema unamjua sana R1 kuwa hawezi kuwa tajiri; kumbe ndo walewale waliotumwa humu na wanaowajua kuja kuwatetea. Kumbe ndio maana unawatetea na kutafuta sababu za kuwachafua watu wanaowapinga. Ningekuwa mlipaji wako ningesitisha malipo make umewaumbua waliokutuma pasipo kujijua.
 
Du, Ridhwani bilionea mwenye vituo vya mafuta 30 na nini tena? Kazi kwelikweli.....

Just thought - Ningependa kuwajua watoto wa Dr Slaa na mapema ili tuwajue na kuwapima pale baba Wilbroad atakapo kuja kuwa Rais...
 
Ikiwa ninyi mna haki ya kushabikia upuuzi huu kwanini wengine wasiwe na haki ya kumtetea Ridhwani?

Na nani amekuambia kuwa katika mahakama ya watanzania jukumu, haki ama uhalali wa Marando kutetea mafisadi una nafasi? Kitendo cha Matando kujinasabisha na vita ufisadi ni kukejeli na kutusi akili za watanzania lakini pia kinatoa picha halisi ya hao wapiganaji na vita vyenyewe



Hii ishawahi kujadiliwa hapa JF na ikiwa bayana kuwao Marando ana haki ya kumtetea Manji. Ni mwanasheria na ndiyo kazi yake tofautisha hiyo na siasa au kumtetea kwenye kesi ya wizi au ufisadi ile ni kesi ya kudhalilishana. Hata kama atawatetea wezi wa wa EPA ni haki yake kufanya hivo ila akitoka hapo hapaswi kuwatetea kwenye majukwaa kama mwanasiasa. Ni ngumu sana kuelewa hesabu hii kwetu wabongo.

Umesema unamjua sana R1 kuwa hawezi kuwa tajiri; kumbe ndo walewale waliotumwa humu na wanaowajua kuja kuwatetea. Kumbe ndio maana unawatetea na kutafuta sababu za kuwachafua watu wanaowapinga. Ningekuwa mlipaji wako ningesitisha malipo make umewaumbua waliokutuma pasipo kujijua.
 
Du, Ridhwani bilionea mwenye vituo vya mafuta 30 na nini tena? Kazi kwelikweli.....

Just thought - Ningependa kuwajua watoto wa Dr Slaa na mapema ili tuwajue na kuwapima pale baba Wilbroad atakapo kuja kuwa Rais...
kumbe watu wengi wanaamini dr slaa atakuwa rais 2015
Keep up the good dr
 
... je Rizwan Kumiliki mabilioni ni kitu cha hatari? Naelewa kwa ufahamu wangu Rizwan ni mtoto wa RAIS na baba yake alikuwa waziri katika wizara nyingi sana hapa Tanzania kabla ya kuwa Rais; ninavyoelewa mimi Rizwan kumiliki Bilioni moja si kitu cha ajabu, eti kamaliza shule juzi ndio asiweze kumiliki hiyo ela haiingii akilini hata kidogo kwa mtoto wa kimasikini sawa ila Riz sio mtoto wa kimasikini akashindwa kujiingiza kwenye masuala ya kutafuta pesa...

Nahisi sijakuelewa! Rizwan kumiliki mabilioni ya WATANZANIA ni KITU CHA HATARI! Baba yake kuwa waziri hata kwa miaka 50 kwa mishahara ya serikali inayojulikana haiwezi kumfanya mtoto (hata yeye mwenyewe) kuwa bilionea! Tafadhali fikiria sana next time unapotoa mawazo yako huku!
 
Pepombili ni Riz. Dr.Slaa umesema ukweli.Kama Riz anaona ameonewa aende mahakamani ukatoe ushahidi unaothibitisha pasipo shaka lenye maana kuwa yeye si Bilionea.Kama Riz atakaa kimpya maana yake atakuwa amekubali kuwa yeye naye ni fisadi. Silence implies concerned. Nasubiri kwa hamu kesi itakayofunguliwa na Riz.
Riz naye apewe siku 90 ang'oke.Atoe gamba"skin shedding".

Sio lazima aende mahakamani ataje mali zake wazi na source na tax alizolipa kwakuanzia (tuanzie na uwazi na ukweli). Lakini tukumbuke kuwa watu wa usalama wa taifa hawana limit ya payroll i.e. they can spend as much as they want kwahiyo kama huyu yuko usalama wa Taifa ngoma itakua ngumu kidogo
 
Back
Top Bottom