MADAM T
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 6,220
- 3,917
Huonyeshi kama unaakili za kitajiri hata kidogo!Akillizako ndio za kimaskini, wakati wewe unalialia wenzako tunachangamkia fursa na kuzitumia.
Huonyeshi kama unaakili za kitajiri hata kidogo!Akillizako ndio za kimaskini, wakati wewe unalialia wenzako tunachangamkia fursa na kuzitumia.
Teh teh teh teh! Mkuu paka akitaka kupita kwenye uchochoro mwembamba huwa anaupima upana wake kwa masharubu. Tatizo la huyu mwenye akili kuliko wote hakuchungulia ndani ya nyumba kuna nini matokeo yake hatujui tunakoelekea kila ukiamka utatamani ya jana. Nchi inaenda kimsopolosopoloMpendwa Sizonje habari za siku.... natumaini u buheri wa afya kibaiolojia japokuwa kiroho u tofauti...
Rafiki yangu Sizonje nakumbuka enzi zile tukijadili mpira ulivyokua hodari kumlaumu kocha!! Kwamba kocha wa timu yetu hawezi... kocha mzembe na anafuga uvundo....
Kadiri tulipokutana kila baada ya sentensi tatu lazima umseme kocha kila siku ikawa hamkani si shwari!!
Sizonje utakumbuka kocha alikuvumilia sana japokuwa ulikua huwezi!! Mdomo na maneno mengi yalikubeba kwa mashabiki lakini wachezaji wenzio walikujua!! Ulikua bingwa wa kukariri tarakimu za mchezo bila ujuzi na weledi wa mchezo!! Hata kocha alipoonywa sana juu ya kiwango chako kibovu bado alikubeba ingawa ulimsogoa!!
Hayawi hayawi yakawa Sizonje!! Kauli zako zikalipa!! Kocha akastaafu na ukocha ukapewa wewe!! Kila mtu ndani ya timu akiduwaa mashabiki waliolewa kauli zako tamu ziso kifani walikubeba hatimaye ukawa kocha!!
Awali ulionesha uwezo wa kukonga mashabiki kwa sifa na vitimbi kemkem!! Siku zikasonga mashabiki wakaona timu inarejea nyuma kuliko ilikokuwa kwa kocha mzembe!!
Nakujua Sizonje!! Hupendi kukosolewa na wala hupendi kimya cha sifa!! Vigelegele vya mashabiki na vifijo vimekoma!! Mbinu zote za michezo ulizotumia zimebuma!! Timu inarudi nyuma kwa kasi na wachezaji wameshapoteza mori!! Kila ugusapo sasa hapagusiki!! Wachezaji wanaonesha ari machoni pako tu lakini uwanjani wamedorora!!
Sizonje usichanganyikiwe... mambo bado ndio kwanza safari inaanza!! Ishike ngao na kigao kuyahimili majira!!!
Kwa leo naishia hapa Sizonje nikija mjini ntakutembelea tule maboga ya enzi zetu.
Sizonjeee uliona mepesi sasa wajuta Sizonje
Mkuu mara hii umesahau sizonje huwa hapendi kukosolewa? Yeye huwa anapenda vifijo, ndelemo na vigelegeleHivi wale "Forbes" waliotushindanisha na "peoples of Rwanda" hawawezi kutuletea mpambano kati ya Sizonje na Lusungo wa jf?Maana bandiko hili kama sizonje akilisoma kwa unyenyekevu linaweza kumsaidia na kumpatia fursa ya kujisahihisha.
FAIZA wacha masikio wazi usikie vizuri na wewe ustahimili usikie na unyamaze
Umemaliza mkuu!!Tujikumbushe kauli tata za Sizonje zilizopelekea Uchumi kudorora:
Uhalisia wa matokeo ya kauli za Sizonjee ni km ifuatavyo:
- Mimi ni wa TOFAUTI sana bwana huwa SIJARIBIWI.
- Nataka niwashushe kutoka mishahara waliokuwa wanaishi kama MALAIKA sasa waishi kama MASHETANI.
- Nchi hii TAJIRI sana isipokee MISAADA baali itoe MISAADA.
- Tanzania ya MAGUFULI itakuwa ya VIWANDA!
- Nikiingia madarakani wanafunzi wote watapata MIKOPO!
- Tayari ANAJARIBIWI na kisiki cha UCHUMI wa nchi!
- Watz wote tumeshushwa tunaishi kama MASHETANI!
- Misaada ya TETEMEKO kaitapeli kujenga MIUNDOMBINU!
- Mpaka sasa HAKUNA KIWANDA alichojenga walau KIMOJA.
- Hakuna MIKOPO tuna hakiki wanafunzi HEWA!
Kabisa mkuu, shida kubwa ya kocha Sizonje ni kujiona mjuaji sana!! Sasa anaharibu kila kitu!!Teh teh teh teh! Mkuu paka akitaka kupita kwenye uchochoro mwembamba huwa anaupima upana wake kwa masharubu. Tatizo la huyu mwenye akili kuliko wote hakuchungulia ndani ya nyumba kuna nini matokeo yake hatujui tunakoelekea kila ukiamka utatamani ya jana. Nchi inaenda kimsopolosopolo
Mi naikumbuka kauli moja ya kocha Sizonje... alimwambia kocha mwenzie wa timu ya daraja la pili kule kwenye visiwa... Kuwa laiti kama yeye ndo angekuwa kocha wa timu ile... asingesaini malipo ya kocha wa timu B inayopambana kupanda daraja. Kumbe Sizonje hata kanuni za soka hazijui... LoooTujikumbushe kauli tata za Sizonje zilizopelekea Uchumi kudorora:
Uhalisia wa matokeo ya kauli za Sizonjee ni km ifuatavyo:
- Mimi ni wa TOFAUTI sana bwana huwa SIJARIBIWI.
- Nataka niwashushe kutoka mishahara waliokuwa wanaishi kama MALAIKA sasa waishi kama MASHETANI.
- Nchi hii TAJIRI sana isipokee MISAADA baali itoe MISAADA.
- Tanzania ya MAGUFULI itakuwa ya VIWANDA!
- Nikiingia madarakani wanafunzi wote watapata MIKOPO!
- Tayari ANAJARIBIWI na kisiki cha UCHUMI wa nchi!
- Watz wote tumeshushwa tunaishi kama MASHETANI!
- Misaada ya TETEMEKO kaitapeli kujenga MIUNDOMBINU!
- Mpaka sasa HAKUNA KIWANDA alichojenga walau KIMOJA.
- Hakuna MIKOPO tuna hakiki wanafunzi HEWA!
Doh ni janga sugu la wazawa kuwa na huyu kocha!!!Mi naikumbuka kauli moja ya kocha Sizonje... alimwambia kocha mwenzie wa timu ya daraja la pili kule kwenye visiwa... Kuwa laiti kama yeye ndo angekuwa kocha wa timu ile... asingesaini malipo ya kocha wa timu B inayopambana kupanda daraja. Kumbe Sizonje hata kanuni za soka hazijui... Looo
Ama kweli sizonje ni mbabe kama Anodi Swaziniga, stelingi hauwawi.
PoleJamani mmeniacha Gizani.sizonje ndo nani
Sasa na wewe mbona unajifanya mjuaji?Tatizo lenu mpo kama watoto walioachishwa ziwa kunyonya huwa wanalia usiku kucha wakiona wanaonewa na ni haki yao kunyonya siku zote kumbe hawajui kuna hatua zinazofuatia mbeleni pengine zitakuwa nzuri au mbaya huo ni mfano tatizo sio Magufuli tatizo ni mfumo na maisha tuliozoeya kuishi ya wizi, ulaghai ,rushwa, dhuluma na mengine yafananayo nayo, sasa Rais anajitahidi kurudisha katika misingi na mfumo uliobora wa kuyafikia malengo watu mnaona taabu ,
Hii nchi jama hata angelishuka malaika kwa hali iliyokuwa imefikia hangeweza kuiongoza humu kila mtu msemaji kila mtu mjuaji cheusi kita takatishwa kuwa cheupe inabidi kujitoa ufahamu tu kuiongoza hii nchi watanzania hatubebeki ,
Mmesahau kuna mikataba ya miaka mia moja humu hembu tuwe na utu jama tumsaidie Rais kuendesha hili gurudumu la maendeleo tuache kulia lia Mungu hapendi namalizia kusema asiyefanya kazi na asile na mikono milegevu hujenga paa bovu.
Ha ha ha haWakulaumiwa hapa ni kikwete kutembea na karatasi mfukoni
Zisonje ualimu mkuu haumfai, labda afsa takwimu maana anakariri sana
