Sizonje usichanganyikiwe, Mambo bado!!

Sizonje usichanganyikiwe, Mambo bado!!

Kama ni Sizonje ni kocha basi atakuwa ni DAVID MOYES.

Jamaa anauwezo mdogo sana kuliko hata KIKWETE. Tumelamba galasa asee
Mfugaji hana haraka .ngombe anazaliwa anakuwa miaka 3 anakamuliwa na kulimishwa miaka miwili .emefika miaka mitano anauzwa ndio pesa ya nguvu inapatikana ndio inatolewa hela ya karo ,mabati ya nyumba,pombe na nyama kidogo ,anavuta subira tena mpaka ngombe mngine tena akuwe.kwa hiyo ndio hivyo inabidi tuwe wavumilivu tuu
 
Hahahahahahahaha, sizonjeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee aaaäaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa anateleza paleeee, mashabiki waliiinuka kutaka kushangiria, naona bench la ufundi linaendabkumganga kidogo....

Huku wachezaji wengine wanaomba maji ya kunywa kidogo walegeze koo, timu imezidiwa sana dakika ni 15 kipindi cha kwanza, hali ni mbaya maji yakunywa hamna wamepewa glukozi wakazie na mate, ...........
 
Tatizo lenu mpo kama watoto walioachishwa ziwa kunyonya huwa wanalia usiku kucha wakiona wanaonewa na ni haki yao kunyonya siku zote kumbe hawajui kuna hatua zinazofuatia mbeleni pengine zitakuwa nzuri au mbaya huo ni mfano tatizo sio Magufuli tatizo ni mfumo na maisha tuliozoeya kuishi ya wizi, ulaghai ,rushwa, dhuluma na mengine yafananayo nayo, sasa Rais anajitahidi kurudisha katika misingi na mfumo uliobora wa kuyafikia malengo watu mnaona taabu ,

Hii nchi jama hata angelishuka malaika kwa hali iliyokuwa imefikia hangeweza kuiongoza humu kila mtu msemaji kila mtu mjuaji cheusi kita takatishwa kuwa cheupe inabidi kujitoa ufahamu tu kuiongoza hii nchi watanzania hatubebeki ,

Mmesahau kuna mikataba ya miaka mia moja humu hembu tuwe na utu jama tumsaidie Rais kuendesha hili gurudumu la maendeleo tuache kulia lia Mungu hapendi namalizia kusema asiyefanya kazi na asile na mikono milegevu hujenga paa bovu.
Kuzoea Maisha ya wizi ,ulaghahi,utapeli ni wewe na wenzako .sisi waTz 90% tunaishi kwa pato halali toka tupate Uhuru ,tafadhali usitupake matope
 
Ni wapuuzi sana hawa, hii nchi imejaa wanafiki sana, angalia majina ya kinafiki anayopewa raisi, nyie ndio mtasababisha hii forum ifungiwe, endeleeni kumchafua chafua, mwenzenu kafungwa kisa ameota, kufungiwa hii ni issue ndogo sana
Forum ifungiwe na watu jee
 
Sizonje bado nina imani n.a. wewe ila huku kwenye uchumi mambo si shwariii bado unamda wa kufanya vizuri mafuta yakawa asali tafuta watalamu as uchumi kaa nao meza moja uone
Heri yako wewe bado uko vizuri una poda yakuendelea kumpaka .wenzio huku ni vumbi tuu linatutimkia
 
Sizonje anafanya kazi
Mungu ampe nguvu usiku na mchana.., walozidi kuwanyonya wananchi na rushwa.
 
"

"Individual savings/holding is collectively harmful in economic growth"

Holding/savings ipo hazina tu,ndo maana inaona hali ni mbaya,Mtu mmoja kahold pesa
Ushauri huu umekosea kumpa sizonje .kwa kutumia hiyo lugha ni lugha ya adui hivyoo hiyoo kwake
 
Baso hakuna haja ya kuwa n.a. washauri wa rais n.a. kama tumeshidwa kisasa basi tufanyekienyeji tumletee kamati ya ufundi atuangalizie kuhusu uchumi
Tatizo ni kwamba hakuna anae thubutu kushauri vinginevyo .anaogopa kuambiwa amepewa rushwa ,embu fikiria unatoa ushauri pesa zirudishwe kwenye mabenki .embu piga hiyo picha
 
Takataka na uchafu agraahhhhhhhh! Mijitu mengine mnafaa kuishi gerezani tu
Sizonje kaanza kuwapunguzia mshahara na posho wachezaji. Kibaya zaid Sizonje hataki wachezaji waweke vocha kwenye simu zao, anadai hawatafanya kazi. Wanaongea tu hawatafanya kazi.
Sizonje huwezi kuuondoa au kuwapunguza umaskini kwa kuwachukia watu.
Ww sizonje! Ona sasa unataka kwenye timu yako uwe unalipwa ww tu mshahara mkubwa.
Timu kila siku inafungwa na bado umeng'ang'ania tu
 
Tatizo lenu mpo kama watoto walioachishwa ziwa kunyonya huwa wanalia usiku kucha wakiona wanaonewa na ni haki yao kunyonya siku zote kumbe hawajui kuna hatua zinazofuatia mbeleni pengine zitakuwa nzuri au mbaya huo ni mfano tatizo sio Magufuli tatizo ni mfumo na maisha tuliozoeya kuishi ya wizi, ulaghai ,rushwa, dhuluma na mengine yafananayo nayo, sasa Rais anajitahidi kurudisha katika misingi na mfumo uliobora wa kuyafikia malengo watu mnaona taabu ,

Hii nchi jama hata angelishuka malaika kwa hali iliyokuwa imefikia hangeweza kuiongoza humu kila mtu msemaji kila mtu mjuaji cheusi kita takatishwa kuwa cheupe inabidi kujitoa ufahamu tu kuiongoza hii nchi watanzania hatubebeki ,

Mmesahau kuna mikataba ya miaka mia moja humu hembu tuwe na utu jama tumsaidie Rais kuendesha hili gurudumu la maendeleo tuache kulia lia Mungu hapendi namalizia kusema asiyefanya kazi na asile na mikono milegevu hujenga paa bovu.
Acha porojo wewe mfumo gani watu wanarudishwa,kukamuliwa kodi zisizo na muelekeo,ajira za watu kupungua kwa kukosa muekekeo wa Uchumi,bandarini hakuna mizigo,mabenki yanakata mitaji huwo ndio mfumo toa poroja hapa.
 
Mpendwa Sizonje habari za siku.... natumaini u buheri wa afya kibaiolojia japokuwa kiroho u tofauti...

Rafiki yangu Sizonje nakumbuka enzi zile tukijadili mpira ulivyokua hodari kumlaumu kocha!! Kwamba kocha wa timu yetu hawezi... kocha mzembe na anafuga uvundo....

Kadiri tulipokutana kila baada ya sentensi tatu lazima umseme kocha kila siku ikawa hamkani si shwari!!

Sizonje utakumbuka kocha alikuvumilia sana japokuwa ulikua huwezi!! Mdomo na maneno mengi yalikubeba kwa mashabiki lakini wachezaji wenzio walikujua!! Ulikua bingwa wa kukariri tarakimu za mchezo bila ujuzi na weledi wa mchezo!! Hata kocha alipoonywa sana juu ya kiwango chako kibovu bado alikubeba ingawa ulimsogoa!!

Hayawi hayawi yakawa Sizonje!! Kauli zako zikalipa!! Kocha akastaafu na ukocha ukapewa wewe!! Kila mtu ndani ya timu akiduwaa mashabiki waliolewa kauli zako tamu ziso kifani walikubeba hatimaye ukawa kocha!!

Awali ulionesha uwezo wa kukonga mashabiki kwa sifa na vitimbi kemkem!! Siku zikasonga mashabiki wakaona timu inarejea nyuma kuliko ilikokuwa kwa kocha mzembe!!

Nakujua Sizonje!! Hupendi kukosolewa na wala hupendi kimya cha sifa!! Vigelegele vya mashabiki na vifijo vimekoma!! Mbinu zote za michezo ulizotumia zimebuma!! Timu inarudi nyuma kwa kasi na wachezaji wameshapoteza mori!! Kila ugusapo sasa hapagusiki!! Wachezaji wanaonesha ari machoni pako tu lakini uwanjani wamedorora!!

Sizonje usichanganyikiwe... mambo bado ndio kwanza safari inaanza!! Ishike ngao na kigao kuyahimili majira!!!

Kwa leo naishia hapa Sizonje nikija mjini ntakutembelea tule maboga ya enzi zetu.
Hawa ndio Washairi na Wagani tunaohitaji Tanzania. Kama kweli msanii ni kioo cha jamii anahitajiwa ajue yale yanayosemwa mtaani na ayatoa kwa wahusika kiusanii na pia kiuhalisia. Asante kwa shairi lako.
 
Hayo majina ya walimu najua sana, sometimes ni upumbavu tu wa wanafunzi, unakuta mwalimu anapiga kazi yake kiuweledi sana, kutokana na hulka ya kipuuzi ya baadhi yetu tokea kuzaliwa, utashangaa wanamtungia jina la kipuuzi puuzi.
Badala ya kujifunza na kuheshimu
Shukuru Akaa kamrija kako bado kanàtoa mvinyo,ila muda simrefu utakuja hapa uwanjani .Muulize Shigongo imekuwaje
 
Back
Top Bottom