Sizonje usichanganyikiwe, Mambo bado!!

Sizonje usichanganyikiwe, Mambo bado!!

Mpendwa Sizonje habari za siku, natumaini u buheri wa afya kibaiolojia japokuwa kiroho u tofauti.

Rafiki yangu Sizonje nakumbuka enzi zile tukijadili mpira ulivyokua hodari kumlaumu kocha!! Kwamba kocha wa timu yetu hawezi, kocha mzembe na anafuga uvundo.

Kadiri tulipokutana kila baada ya sentensi tatu lazima umseme kocha kila siku ikawa hamkani si shwari!

Sizonje utakumbuka kocha alikuvumilia sana japokuwa ulikua huwezi!! Mdomo na maneno mengi yalikubeba kwa mashabiki lakini wachezaji wenzio walikujua!! Ulikua bingwa wa kukariri tarakimu za mchezo bila ujuzi na weledi wa mchezo. Hata kocha alipoonywa sana juu ya kiwango chako kibovu bado alikubeba ingawa ulimsogoa!

Hayawi hayawi yakawa Sizonje!! Kauli zako zikalipa!! Kocha akastaafu na ukocha ukapewa wewe!! Kila mtu ndani ya timu akiduwaa mashabiki waliolewa kauli zako tamu ziso kifani walikubeba hatimaye ukawa kocha.

Awali ulionesha uwezo wa kukonga mashabiki kwa sifa na vitimbi kemkem!! Siku zikasonga mashabiki wakaona timu inarejea nyuma kuliko ilikokuwa kwa kocha mzembe.

Nakujua Sizonje!! Hupendi kukosolewa na wala hupendi kimya cha sifa!! Vigelegele vya mashabiki na vifijo vimekoma!! Mbinu zote za michezo ulizotumia zimebuma!! Timu inarudi nyuma kwa kasi na wachezaji wameshapoteza mori!! Kila ugusapo sasa hapagusiki!! Wachezaji wanaonesha ari machoni pako tu lakini uwanjani wamedorora.

Sizonje usichanganyikiwe, mambo bado ndio kwanza safari inaanza. Ishike ngao na kigao kuyahimili majira.

Kwa leo naishia hapa Sizonje nikija mjini ntakutembelea tule maboga ya enzi zetu.

-----------------------------------------------------------------
UPDATES:
----------------------------------------------- ---------------
Wakuu napenda kuwaarifu kuwa nimepata taarifa nyeti na rasmi kuwa kocha wetu mpendwa Sizonje ameusoma uzi huu na comments zenu zote. Shukrani kwa wote mliotoa ushauri kwa kocha wetu.
Sizonje hatunaye tena. Ulimuonya hakusikia.
 
Ungejua jinsi sisi wakulima wa korosho huku kusini tunavyofaidi uongozi wa Sizonje ungebadili hayo malawama.
Pikipiki na vifaa vya ujenzi vinatoka madukani kwa kasi ya ajabu.Juzi mkulima wa kawaida alifariki kwa mshituko baada ya kupokea milioni 17 za malipo ya korosho.Alishituka kwa kuwa hajawahi kupokea kiasi hicho.
Mkuu ya Kweli haya??
 
NNyie watumbuliwajwi mtaumia sana utawala huu. Utawala huu ni imara sana hauteteleki hata kidogo. Fanyeni kazi pesa za ovyo hazipo tena. TRA siku hizi hamna pesa za dili tena. Zamani nilikuwa nawaogopa sana wanaofanya kazi TRA lakini kwa sasa tunaheahimiana tu na Dada zetu hawawatombi tena ovyoovyo mana hela zimekata. Walimu walikuwa wanaonekana kama wasindikizaji lakini sasa hivi wanaheshimiwa mana wote almost wana income inayofanana. Heko magu umeleta usawa. There is low disparity of income levels.
Mnh......
 
Manyunyu yaliyodondoka leo si mchezo..

Wingu limetanda, mvua kali za mafuriko kutarajiwa... ya Sizonje yamepita.
 
Back
Top Bottom