Madam Mwajuma
JF-Expert Member
- Sep 13, 2014
- 7,076
- 6,774
Kwani ni lazima umuoe??? kama umeshashikiwa panga unataka nini tena, sepa zako. kisicho rizki,(malizia mwenyewe) wanawake wako kibao, unaweza ukawa na mwingine tu, umeskia bwana kaka??
N.B hakuna mila ya wachagga inayosema unamshikia mtu panga, halafu kijana una kiherehere, umwshampa mimba mtoto wa watu unaenda kichwa kichwa bila hata kutuma intelijensia hali imekaaje huko na kutanguliza wajumbe kwanza, eti unajiamkia tu unajikokota, wa wapi wewe mkuu?? (hiki kijamaa kishamba eeh? halafu kinalaumu mila)
One more thing ulifanya makosa sana kutowasiliana hata na mama wa huyo binti kwanza akusaidie kumtuliza huyo mzee au hata na ndugu zake wengine wa karibu. Unaamka tu unaenda ukweni kama chooni, wengine unapigwa shaba halafu tunasema ni mwizi. (Kijana ukweni unatakiwa uende ukiwa umejipanga haswaaaa, hata baba mkwe akikuangalia anaanza kutetemeka mwenyewe unashangaa imekuwaje. sio unaenda kihunihuni tu na kijinsi chako na tisheti unafkiri unangojea daladala wataacha kukushikia panga kweli??
Umenisikitisha sana (kuna wanaume wengine wanahitaji kufundwa naona aisee eti The Boss mtu anakuwaje ana uwezo wa kumpa mwanamke mimba lakini hajui process za kwenda ukweni?)
unajua kazoea makabila mengine ukimzalisha mtu wanataman umuoe hata mahari usitoe. kaskazin wanadhamin watoto wao. atakuwa kaenda kisharobaro mlegezo nini! au binti alivyokuwa na mimba alijibu mbovu binti akawashirikisha wazaz wake
Last edited by a moderator: