Sitasahau: Tulitolewa nduki ukweni siku ya posa

Sitasahau: Tulitolewa nduki ukweni siku ya posa

and 998 others

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Posts
28,417
Reaction score
40,110
Nilikuaga na mpenzi wangu tunapendana kwa kweli toka chuoni (UDSM) basi tukawa tunapiga mechi peku peku (bila kondom) eeh ghafla bidada ananiambia ana mimba kiukweli nilishtuka but anyway tukakubaliana azae tu.

Basi bibie akaja kujifungua mtoto (mimi sikujitokeza huko ukweni kabisaa)mi nawasiliana na mchuchu tu.

Sasa tukakubaliana na mchuchu ni muda muafaka wa kwenda kujitambulisha.

Nikaandaa mshenga na ndugu wa karibu kwenda huko. Duuh ile kufika tu tukamkuta baba mzaa chema kakunja sura balaa ile tunapiga hodi anatuangalia tu (hajibu chochote) ghafla akaingia chumbani akatoka na panga.

Hakuna aliyeaga si mshenga wala mimi. "BA MKWE" anadai nilimzalisha mtoto wake na sijajitokeza siku zote.

Jamani sitamsahau yule mzee.
 
Nilikuaga na mpenzi wangu
kwa hiyo sasa hauko nae?
Nikaandaa mshenga na ndugu wa karibu kwenda huko.
kwa kawaida uchumbani huko wanaenda watu wazima kwa lengo kwanza la kuwekana sawa, mzazi na mzazi, sasa wewe kijana mdogo tu kwenda huko ilikuwa ni ishara ya kumshushia heshima mzee wa watu!
ghafla akaingia chumbani akatoka na panga
Hapo hata kama ningekuwa ni mimi, ningetoka na mipanga kabisaa! Haiwezekani mwanangu akae muda wote huo bila kuonwa, leo uje tu from nowhere!
"BA MKWE" anadai nilimzalisha mtoto wake na sijajitokeza siku zote.
MAIN POINT.. GOOD!
 
Sasa ataisoma namba ndo namuachia mwanae akitaka amuoe yeye mwenyewe. Mizee mingine kichefu chefu tu. Sasa kuzalishwa anaona bonge la dhambi. Wachaga punguzeni mila na sheria za kipuuzi

Sio upuuzi we hujui binti wa kichaga ni mtaji, mzee wa watu kawekeza we umeharibu hata kama ingekuwa mimi ningekukimbiza na cha moto hata bega nikuparaze
 
Sasa ataisoma namba ndo namuachia mwanae akitaka amuoe yeye mwenyewe. Mizee mingine kichefu chefu tu. Sasa kuzalishwa anaona bonge la dhambi. Wachaga punguzeni mila na sheria za kipuuzi

Sasa hapo uchaga umeingiaje hakika ki degree chako cha udsm hakijakusaidia kitu maana maneno yako hayana hekima hata kidogo, bora mzee angakucharanga ili uwe na akili, haya kama mmezaa mtoto wa kike ngoja aje afanywe kama ulivyomfanya binti wa watu afu mkweo ajilete kama wewe ulivyojipeleka tuone uta react vipi
 
Mi ndiyo maana siku hizi nimeanza kufuga vimbwa vidogovidogo najua mpaka mabinti wakue na venyewe vitakuwa vinazeeka kuna ile kitu wanaotumia jamaa fulani ndiyo nawalisha! Dah ni wakali balaa, sasa nikimpata mkwe kama huyu kwanza atacheza na mbwa mpaka akome, kwa kuwa na yeye alinikomesha na anakuja na swaga za kihuni
 
Sasa hapo uchaga umeingiaje hakika ki degree chako cha udsm hakijakusaidia kitu maana maneno yako hayana hekima hata kidogo, bora mzee angakucharanga ili uwe na akili, haya kama mmezaa mtoto wa kike ngoja aje afanywe kama ulivyomfanya binti wa watu afu mkweo ajilete kama wewe ulivyojipeleka tuone uta react vipi

Hajasema alikuwa degree level, huenda ni certificate kabisa.
 
Back
Top Bottom