Sitasahau 2016, nilipungua kilo sita ndani ya wiki moja

Jiang Ze Dong

Member
May 28, 2020
34
125
Salaam wana jamvi

Hakika mungu anajibu maombi nakumbuka mwaka 2016 mwezi December kutokana na mambo kubana ilinibidi nibadilishe aina ya usafiri kipindi icho nlikua natumia Brevis cc2990 ilikua inakula mafuta mengi mno sasa nikawafata madalali wa Magomeni ili wanitafutie mteja lakini nikakumbuka ili niiuze inabidi nifanye ujanja nikaenda Kariakoo Mtaa wa Lumumba nikanunua kibati kinacho onesha cc2500 nikatoa kile kinachosomeka cc3000 nikaweka cha 2500

Safari ya kwenda kwa madalali ikaanza nilipofika nikakutana na dalali maarufu sana pale jina naliifadhi nikamwambia hii gari nauza kama ikitokea mtu wa kuvunja sawa akaniuliza unataka gari aina gani nikamwambia nataka Spacio na kuuza nauza Milioni 11.5 dili ikitiki nakupa laki tano jamaa akanambia subiri akamwita dalali mwenzake wakajadiliana wakanita akanambia Spacio hamna labda IST yule dalali kanipa funguo niiangalie lakini mimi muda wote lengo ilikua kuuza sio kuvunja nikaikataa ile IST sasa yule dalali mwenzie akaipiga picha Brevis akasema anamteja wake alikua anataka Brevis Full Option na kipindi kile Brevis Full Option ilikua bei juu kidogo sasa akaona kaokota dodo kwenye mpera

Tukasubiri mara mteja wake akapiga simu akamuuliza cc ngapi jamaa akajibu angalia kwenye picha cc 2500 wakaongea kwa muda alipomaliza akatueleza kuwa mteja kakubali ila yupo safari ila ataichukua yeye mteja wake akirudi atamuuzia tukakubaliana bei iwe Milioni na yule mwenzie nimpoze nikmwambia sawa yule dalali akasema kesho atalipia alivyonambia vile moyo ulifurahi sana nikamwambia yule mwenzie mwambie atoe kishika uchumba ili nisiuze basi yule dalali mwenzie akamwita chemba wakaongea walipomaliza jamaa akatoa laki tano akanipa akanambia tuandikishiane nikakubali mdhamini akiwa yule mwenzie akanipa laki tano nikampa yule mwenzie laki mbili tukaagana

Kesho yake saa tatu asubuhi jamaa akanipigia tukutane niende na document zote nikatoka nikaanza safari tukakutana pale pale kwa jana yake nilipofika tu jamaa akatoa pesa tukahesabu tulipo maliza tukaandikishiana mkataba nikamwita jamaa wa bajaji ninae mfahamu nikaondoka nakumbuka ile siku ilikua sikukuu benki zimefungwa nikaenda mpaka Magomeni Mikumi nikaingia kwenye show room walikua awajafunga nikachagua IST tukapatana nikamlipa akanambia kesho yake ataisajiri akanambia kama naweza itumia ikiwa na Chassis namba nikamwambia naweza akanipa funguo nikaondoka nayo

Wakati nataka kuondoka yule dalali akanipigia simu akaniuliza kwan hii gari cc ngapi me nikamjibu cc2500 akanambia mbona kwenye kadi imeandikwa cc2990 nikamwambia me nilikua sijui akataka kuonana na mimi nikamwambia nipo Tegeta naenda Tanga jamaa alichoka sasa nilipokua naendesha ile gari ilikua inatoa muungurumo mkubwa kama trekta nikaona haya mjanga mengine

Itaendelea...

=======

Tuendelee

Sasa akili ilianza kuwaza mambo mengi wakati huo nikiwa naelekea kinondoni biafra nilipofika biafra kiwanjani kuna jamaa nafahamina nae nika muelezea juu ya tatizo la gari jamaa akacheka sana akaniona kama wakuja hasa pale nilipomwambia bei nilionunulia nlikua nimeinunua ml 11 lakin nilimpa ml 10 kesho yake antamilizia akanambia twende nikakuoneshe ist ya bei hio hii umepigwa nikamwambia sawa tukavuka barabara pale biafra kama unaenda Morocco kuna show room zipo tatu sasa ile ya katikati siwezi kuweka jina hapa tukaenda tukamkuta jamaa ambae yeye anafanya kazi pale tukaongea nae akasema leo unaweza kuiona lakini ipo ofisi nyingine tukaenda

Ofisi yao nyingine ipo barabara ya kutoka Morocco kama unaenda victoria sheli ipo upande wa kulia tukaenda aseah ist ilikua nzuri hatari yaani imekaa kisasa yaan ipo poa sana nikaambiwa bei ml 11 dah yaan ilinibidi nijione boya kwakua niliipenda ilinibidi niongee na yule mfanyakazi wao wasiiuze jamaa akanambia inabidi nitoe kishika uchumba nikatoa laki tano ili isiuzwe mida ya saa kumi na moja jioni nikaondoka kurudi nyumbani huku nikiwa na mawazo juu ya kile kimeo nakirudishaje kwa mwenyewe
Usiku kucha nlikua nawaza jinsi ya kuirudisha ile gari ili nipewe pesa yangu nikalipie ile nyingine

Kesho ikafika nikaenda mpaka pale show room magomen mikumi nlipofika ilikua mapema sana saa mbili kasoro nilikaribishwa na dada wa mapokezi katika maongezi yule dada akaropoka kuwa ile gari ilikua inatumika Zanzibar na mdogowake mwenye show room dah apo ndo nikagundua ndo mana ipo vile dah sasa wazo lilikua napataje pesa zangu nikakaa mpaka yule mwarabu mwenye show room akafika alipofika akafurahi tukaingia ofisini baada ya salamu akanambia jamaa yake amefatilia usajiri mpaka saa sita atakua kashakamilisha dah nikaona huu mtihan

Ikanibidi niwe msanii palepale nikaanza kumwambia yule mwarabu kuwa baba wa kambo kachukua mkopo kaweka hati ya mashamba ya mama sasa benki wanataka kuyauza na leo ndo mnada unafanyika inabidi nimuokoe mama maana kazimia mara mbili na mimi ndo mkombozi wake wakati naongea huku machozi yananitoka dah yule mwarabu akaniuliza sasa ulikua unatakaje nikamwambia naomba biashara tuighairishe mwarabu akanambia subiri akampigia jamaa yake wakaongea kisha akanambia gari ishapata namba itabidi hii gari uniuzie maana yake mimi ndo nimuuzie yeye dah kwangu ilikua ngumu sana

Ikabidi tupatane akakubali kuinunua kwa ml 9.5 na mimi nlimlipa ml kumi jana yake basi akanipa ml 9.5 nikaondoka faster mpaka kinondon nikamchukua yule jamaa yangu tukaenda kuilipia ile gari kwa wale wahindi wakanambia kesho nikamalizie ml moja mana jumla ilikua ml 10 nikaondoka kesho yake nikamalizia ml 1 nikachukua gari nikaondoka lakini ile gari ilikua chinichini sana yaan kwenye tuta mpaka ulipande kiubavu kingine shokap zilikua zimechoka sana lakin nikaona sio tatizo kubwa nilivyofika home nikamwita fundi alipocheki zile shokap akanambia izi zinatumia coil spring moja laki mbili na nusu zote nne zinauzwa ml1 nikaona huu mkosi

Nikwapigia wale wahindi kuwaelezea wakanambia niipeleke kweli kesho yake nikaipeleka wakamwita fundi wao fundi wao akaichukua akaenda kuitengeneza nikaambiwa nirudi jioni nikaondoka naomba nitaje jina la mtu alienisaidia sana jamaa anaitwa Hassan mfanyakazi wa wale wahindi ambao show room yao inaitwa chief cars dah yule jamaa alisimama upande wangu kuhakikisha sidhulumiwi

Jioni niliporudi nilkuta gari imebadirika sana imekua na shape mbaya coz kafunga shokap za kawaida ikawa imeondoa ule uzuri wake alafu bampa la nyuma lilikua limemfumuka nahisi alipita njia za mashimo dah ilikua sio ile tena mawazo ya kubadirishiwa yakanijia lakin nitaanzaje nikapewa gari yangu nikaondoka mpaka njia panda ya kagera pale kuna sheli alafu pembeni wanaosha magari nikaiosha nikaondoka mpaka home kesho yake nikaenda kibaruani kuna jamaa akaipenda akataka nimuuzie lakin ilikua imeenda km nyingi sana mpaka jamaa akashangaa ilikua na km149000 akaikataa dah apo sasa mawazo yakanijia lazima nibadilishiwe gari tatizo lingine ilikua inawaka taa ya check engine ata ikiwa inatembea

Jambo la kushangaza tangu niichukue mshale wa mafuta ulikua upo palepale haupandi wala kushuka na mimi cjaongeza mafuta jioni wakati narudi home nilipofika magomen usalama gari ikazima ghafla nikahisi mafuta geji itakua mbovu jamaa wakanisaidia kuisukuma mpaka pembeni nikaweka mafuta ya elfu tatu gari ikawaka nikaondoka uku nikijisemea moyoni kesho nairudisha kiukweli ujalala vizuri usiku huo asubuhi nikaenda pale cheaf cars nikamkuta Hassan nikamweleza kuhusu taa ya check engine kuwaka akanambia tumsubiri boss wake aje boss wake alivyofika nikamuelezea akakasirika akaniona mimi mkorofi naleta vurugu ofisini kwake akaita walinzi wanitoe nikawaambia mimi ninaushahidi kuwa gari haipo sawa wakinisumbua naenda polisi then naenda tra dah muindi kusikia tra akanambia subiri akamwita fundi wake

Fundi alipofika nikamuonyesha video nilioirekodi ya taa ya engine akasema mie muongo yule muhindi akamwambia wapande waitest kweli wakaingia wakaondoka baada ya muda wakarudi wakabaki ndani ya gari huku wanajadiliana mara ghafla gari ilianza kutetemeka ikazima kila akiwasha haiwaki mshale wa gaji ya mafuta upo kati wakashuka yule muhindi akaniuliza mara ya mwisho lini kuweka mafuta nikamwambia jana nimeweka ya elfu ishirini akasema basi gari inashida ingia ndani chagua gari nyingine aseah nilifurahi sana nikachagua spacio new model wakanisajilia siku iyoiyo mida ya saa nane yule fundi kaja kanikuta natoka na gari akanambia we jamaa msumbufu kumbe geji mbovu nikamwambia mwambie boss wako yule Hassan nikampa laki akakataa akasema ametimiza majukumu yake

Namshukuru mungu mpaka mwaka jana nimeiuza haijawai nisumbua chochote hakika nimejifunza sana ilifikia hatua nilikonda na uzito wa mwili ulipungua ndani ya siku sita tu

Nawasilisha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom