Nilivyokosa kumpiga mshenga wangu mawe mara baada ya kuungana na wazazi wa mpenzi wangu

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,917
24,670
Ni story sensitive kidogo ambayo sikuwahi kuileta hapo wakati huo niko na majanga ya mtoto wa diwani nilipatwa na mikasa haswaa.

Wengi mnajua kipi kilinikuta baada ya kumtia mimba mtoto wa diwani. Niliandika hapa.

Nilishikiliwa pale Kwa Mroto na kulazimishwa nilipe mahari ili nioe kabisa.

Kilichotokea baada ya kutoka pale Central na kukubaliana na wakwe nikamtafuta mshenga tukapeleka barua ya posa, tukaitwa kwa ajili ya kutoa mahali ambayo ata kabla ya posa baba mkwe diwani aliitaja pale kituoni ni milioni 1.5

Mimi nilikaa na mshenga wangu na kumwambia ndugu najua tukifika pale watataja kiasi hiki cha pesa, mimi kwa kweli sina.

Wewe ni mshenga naomba ongea nao mpaka kiasi hiki 800K (laki nane), ambayo nitaitoa kwa awamu 4, kwa kumaanisha:

-Awamu ya kwanza 250k
-Awamu ya pili 200k
-Awamu ya tatu 200k
Na Awamu ya mwisho awamu ya nne nitatoa nimalizie 150k. Ila kama watataka nitoe yote bila awamu mimi sina.

Tulikaa na kukubaliana fresh, hatimaye siku ikafika. Kama tulivyotaraji ndivyo ilivyo kuwa. Mahari ilitajwa lakini ile ile 1.5M, tena kwa maneno kibao kutoka kwa baba mkwe.

"Namuozesha mwanangu kwako kwa sababu tu umemsababishia ujauzito, lakini sikupaswa kabisa kumuozesha kwako. Mtoto muhuni kabisa wewe, unadiriki kumpa mwanangu mimba na kutaka kukimbia"

"Kijana mjinga kama wewe ilipaswa nikupe mwanangu na viboko hamsini matakoni ili ukakae naye kwa adabu huko kwako".

Wakati anaongea hayo mi kimya namtazama tu.

Kumcheki mshenga naye baada ya ku-bargain bei ya mahari ishuke, naye akaanza kuunga hoja za baba huku akinikandia zaidi.

"Huyu kijana ni mpumbavu sana kaharibu sana watoto hapa mtaani, siku zote nilikuwa namtazama tu na kujisemea ipo siku yatamkuta na leo kweli. Mimi ningekuwa ni wewe mzee..."

Mshenga akawa anazidi kuendelea kuongea.

"Huyu kijana ningepasawa anilipe mahari si chini ya milioni 2, akaendelea kukazia si chini ya milioni 2"

Mi niko namtazama tu huku hasira ziko hapa kwa utosi.

Yaani yeye badala ya ku-bargain bei mahari ishushwe, akawa anakazia iongezwe.

Aliongea sana siku ile mwisho wa siku tukamalizana nao mahari ilipwe ile ile tajwa milioni 1.5,

Tulivyotoka pale mi zangu kimya sikuongea wala nini licha ya yeye kujiongelesha ongelesha. Moyoni nikawa najisemea hanijui huyu.

Kilichotokea nilisimulia hapa ila kwa ufupi tu.

Siku ya kulipa mahari ilifika; nilichofanya nikaenda na 250k (laki mbili na nusu), bila kumwambia mshenga wala nini.

Kila akiniuliza namwambia mi niko sawa mahari ipo hivyo asiwe na shaka.

Tulivyofika ukweni tulipokelewa safi. Mshenga kwa mbwembwe zote akajitambulisha kwamba nimemleta kijana na mahari yenu yote hivyo leo leo tunamuhitaji mke wetu.

Kwa mbwembwe za kutosha huku wakicheka.

Muda ulivyofika wa kutoa mahari mimi bila hiyana nikawachana tu: "Jamani kusema kweli mimi kijana wenu sina kitu ila leo nimeleta hii 250k kama advance tu (kitanguliza mahari), lakini nitatoa mahari yenu yote kidogo kidogo cha muhimu kuvumiliana.

Mshenga akabaki hoi, baba mkwe hoi,
Mwisho wakakaa kujadiliana pale nikaambiwa niende nitaitwa tena.

Ndio hivyo mpaka leo sijaitwa na mtoto ameshazaliwa kila siku naenda kumuona. Nikifika pale mara nyingi namkuta anachezacheza na babu yake (diwani).

Kwa sasa haniiti tena kijana mpumbavu nikifika pale tunafurahi na kucheka sana, tunapiga story na mwisho wa siku huyo natembea.

Huwa anafurahi tu vile ninavyomuhudumia mjukuu wake; alijua nitamkimbia.

Cc Zero iq


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni story sensitive kidogo ambayo sikuwahi kuileta hapo wakati huo niko na majanga ya mtoto wa diwani nilipatwa na mikasa haswaa.

Wengi mnajua kipi kilinikuta baada ya kumtia mimba mtoto wa diwani. Niliandika hapa.

Nilishikiliwa pale Kwa Mroto na kulazimishwa nilipe mahari ili nioe kabisa.

Kilichotokea baada ya kutoka pale Central na kukubaliana na wakwe nikamtafuta mshenga tukapeleka barua ya posa, tukaitwa kwa ajili ya kutoa mahali ambayo ata kabla ya posa baba mkwe diwani aliitaja pale kituoni ni milioni 1.5

Mimi nilikaa na mshenga wangu na kumwambia ndugu najua tukifika pale watataja kiasi hiki cha pesa, mimi kwa kweli sina.

Wewe ni mshenga naomba ongea nao mpaka kiasi hiki 800K (laki nane), ambayo nitaitoa kwa awamu 4, kwa kumaanisha:

-Awamu ya kwanza 250k
-Awamu ya pili 200k
-Awamu ya tatu 200k
Na Awamu ya mwisho awamu ya nne nitatoa nimalizie 150k.

ila kama watataka nitoe yote bila Awamu mimi sina.

Tulikaa na kukubaliana fresh, Atimae siku ikafika,
Kama tulivyotaraji ndivyo iliyo kuwa, mahali ilitajwa lakini ile ile 1.5M, tena kwa maneno kibao kutoka kwa baba mkwe,

"Namuozesha mwanangu kwako kwa sababu tu umemsababishia ujauzito, lakini sikupaswa kabisa kumuozesha kwako, mtoto muhuni kabisa wewe unadiriki kumpa mwanangu Mimba na kutaka kukimbia,
Kijana mjinga kama wewe ilipaswa nikupe mwanangu Na Viboko hamsini matakoni ili ukakae nae kwa Adabu huko kwako".

Wakati anaongea hayo mi kimya namtazama tu,
Kumcheki mshenga nae baada ya kubagain bei ya mahari ishuke nae akaanza kuunga hoja za baba huku Hakinikandia zaidi,

"Huyu kijana ni mpumbavu sana kaharibu sana watoto hapa mtaani, siku zote nilikuwa namtazama tu na kujisemea ipo siku yatamkuta na leo kweli,
Mimi ningekuwa ni wewe mzee 'mshenga akawa anazidi kuendelea kuongea',
Huyu kijana ningepasawa anilipe mahari si chini ya milioni 2,akaendelea kukazia si chini ya milioni 2,"

Mi niko namtazama tu huku hasira ziko hapa kwa utosi,
Yaani yeye baada ya kubargain bei mahari ishushwe akawa anakazia iongezwe,

Aliongea sana siku ile mwisho wa siku tukamalizana nao mahari ilipwe ile ile tajwa milioni 1.5,

Tulivyotoka pale mi zangu kimya sikuongea wala nini licha ya yeye kujiongelesha ongelesha,
Moyoni nikawa najisemea hanijui huyu,

Kilichotokea nilisimulia hapa ila kwa ufupi tu,
Siku ya kulipa mahari ilifika nilichofanya nikaenda na 250k(laki mbili na Nusu), bila kumwambia mshenga wala nini,

Kila akiniuliza namwambia mi niko sawa mahari ipo hivyo asiwe na shaka,

Tulivyofika ukweni tulipokelewa safi, Mshenga kwa mbwembwe zote akajitambulisha kwamba nimemleta kijana na mahari yenu yote hivyo leo leo tunamuhitaji mke wetu,
Kwa mbwe mbwe za kutosha huku wakicheka,

Muda ulivyofika wa kutoa mahari mimi bila hiyana nikawachana tu
"Jamani kusema kweli mimi kijana wenu Sina kitu ila leo nimeleta hii 250k,kama Advance tu(kitanguliza mahari),
Lakini nitatoa mahari yenu yote kidogo kidogo cha muhimu kuvumiliana,

Mshenga akabaki hoi, baba mkwe hoi,
Mwisho wakakaa kujadiliana pale nikaambiwa niende nitaitwa tena.


Ndio hivyo mpaka leo sijaitwa na mtoto ameshazaliwa kila siku naenda kumuona,nikifika pale mara nyingi namkuta anacheza cheza na babu yake(diwani),
Kwa sasa haniiti tena kijana mpumbavu nikifika pale tunafurahi na kucheka sana, tunapiga story na mwisho wa siku huyo natembea,

Huwa anafurahi tu vile ninavyomuhudumia mjukuu wake alijua nitamkimbia.



Cc Zero iq



Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa wewe ni zero IQ utapata wapi mshenga mwenye IQ kubwa ??

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom