Well, "mwenendo wa kesi upitiwe upya," ndio kesi kurudiwa mara mbili huko!
Ndio ilikuwa ni rufaa, lakini kuna wakati appeal on acquittal ni kama kesi kurudiwa upya.
Kwa kuelewa hilo, kuna msingi unaitwa double jeopardy kwenye nchi zilizopevuka kwenye haki za raia na misingi ya ki-katiba, ambapo serikali for the most part hairuhusiwi kukata rufaa wakishashindwa kesi.
India, Marekani, Afrika Kusini, kwa mfano, rufaa za serikali baada ya kushindwa kesi haziruhusiwi, isipokuwa for a few special exceptions. Hapa kwetu serikali ilishindwa na Shehe Ponda Morogoro, DPP akakata rufaa, mara ya pili Shehe Ponda akashindwa. Serikali imeshindwa kesi ya na kina Kamanda Zombe, DPP akakata rufaa, kesi ikarudiwa, kina Mageni wameshindwa.
Huku ni kuvunja misingi ya double jeopardy inayokataza serikali kuwa na nafasi ya kukushitaki mara mbili mbili mara tatu tatu kwa kosa lile lile.