Sioi Sumari achaguliwa na CCM kumrithi baba yake Arumeru Mashariki!

Sioi Sumari achaguliwa na CCM kumrithi baba yake Arumeru Mashariki!

Kitila. Ni lazima mtambue ya kuwa chaguzi hii mtakuwa mkipambana na Lowassa, kwa hiyo y'all need to be ready. Umeona alivyoweza kusambaratisha ukoo wa Kaaya hapo juu?
Kwa kungezea tu, EL atatumia nguvu za ziada sio tuu kumsupport mkwe, au kuproove kwa CCM that he is still in controll, hapa ataongeza nguvu kuwathibitishia Wameru kuwa yuko nao kwa vile japo wengi wanamfahamu kama ni Mmasai, kiukweli EL sio Mmasai ni Mmeru!. Hivyo atampigania mkwewe kwa nguvu zake zote ili pia to maintain his status quo yake ya Kimeru!.
 
Sisi mzigo tunaenda kupiga wala hatumuogopi mgombea yeyote. Mapambano yetu ni kuutoa mfumo huu ulioshindwa. Tumejiandaa vizuri mno kuliko ninavyoweza kuandika hapa.

Nilikuwa natoa maoni yangu kuhusu hali halisi kuhusu utamaduni wetu waafrika katika habari ya kifo.

Mkuu Mkumbo, ni habari njema kwamba mmejiandaaa vizuri kwa ajili ya kushinda, Kiufundi CDM wana nafasi kubwa ya kushinda pale kama watajipanga vizuri na kuepuka siasa za maji taka. Koo za kimeru zina migawanyiko mikubwa, CDM watumie hiyo kama siraha yao ya ushindi kwa kuweka mgombea asiyefungamana na upande wowote, na hicho ndicho walichofanya CCM.
Tutegemee mechi kali na ya kupendeza.
 
Tatizo kubwa ninaloliona Kwa huyu kijana ni timing. Kiafrika ilikuwa ni mapema mno kugombea baada ya kifo cha babake. Kimsingi bado yupo msibani na hii haiwezi kupokelewa vizuri na wapiga kura, unless uafrika wa wameru ni tofauti!
Mkuu mimi nililizungumzia mapema hata arobaini haijaisha mtoto wa marehemu anaanza kugombea urithi, kiafrika hii haikubaliki. CCM wamefanya kosa kubwa sana unaona hata kura zake alizopata hazi reflect matakwa ya wameru na wanaCCM wenzake. Hapa amechaguliwa si kwa merits alizonazo ila kwa sympathy ya baba yake na hicho ndicho kitakacho wa cost CCM.
 
Mkuu Rejao,
Nadhani huyo kijana atapeleka msiba mkubwa ndani ya Chadema.

Pro-Chadema JF wamebaki kujiliwaza na kujifariji huku wakitapatapa hovyo.

Wengine wanasema kachagulia kislutan wanasahau kuwa ndani ya Chadema wapo watu wengi tu wa familia moja.
Usultani CCM ni kama kazi kama hamna majina yanayojulikana mtabaki kubeba mabegi ya kina Nape Nnauye wenye majina hadi mabega yaende upande.
 
yeah right yanafuara

Pamoja na haki za kikatiba,watz tunahitaji kuwa wazalendo kwa kuonyesha moyo wa kupendana sisi kwa sisi.Nazungumza hivi kwa sababu huwezi kuwa na mtanzania ambaye ni mzalendo wa kweli akaenda kugombea nafasi ya kisiasa ambayo mzazi wake ameiacha ktk hali yoyote ama kifo au kujiuzuru eti fikra ni kwamba familia nyingine hazina uwezo kama familia ya kwetu.NILIPATA KUSEMA KUWA NCHI ILIYOJENGWA NA MASKINI AU MNYONGE HUWA NA MSINGI IMARA KULIKO ILE YA TAJIRI KWA TOFAUTI YA UMOJA NA UBINAFSI[MNYONGE NA TAJIRI],hii ndiyo Tanzania inavyo pokwa na matajiri na kubomoa nyumba iliyojengwa na wanyonge.TUSUBIRI ITAKAPOBOMOLEWA NA KUJENGWA UPYA KIUTAJIRI? Matajiri hawa tutawaweza?KAAAAAAZI KWELIKWELI,RUDI MWALIMU!
 
Chadema wapange timu bora kabisa kule! Wawatumie zaidi vijana wenye ushawishi! Ikitokea Chadema mkashindwa kulitwaa jimbo hili nawahakikishia tutegemee msiba mzito 2015! No justification this tyme mjue hilo,sijui kura zimeibiwa au chochote hatutaki kusikia! Tumewaamini lazima mshinde! Kama tunashindwa now ccm ikiwa mahututi ikiimarika kidogo kuna upinzani kweli? Chadema lazima mshinde na kampeni zenu ziwe Cost effective,efficient and economy! Lazima muwe na watu wanaojitoa kutumikia wananchi ili kuja kukomboa nchi mikononi mwa ccm iliyochoka! Msiwe na wanachama wa kulia na posho ktk harakati hizi ngumu! Fanyeni kazi usiku na mchana kwa gharama kidogo lakini mkiwa na timu ya watu wenye ari kubwa! Msiwaonee haya ccm hasa huyo EL ambaye atakuwepo huko! Waambieni yote wananchi kwa lugha nyepesi kabisa! Mwisho uchaguzi wa kuteua mgombea wenu uwe wa uhuru na haki! Haka kauchaguzi kadogo hatutegemei malalamiko! Wekeni process wazi ili hata atayekosea isíhitaji maelezo! Kila lakheri!

Very true.........
 
kama kawa kama dawa uongozi ni kwa ajiri ya watoto wa viongozi magamba kushney malegeha
 
Yes of course, tupo hapa kwa ajili ya kufanya ngumu. Nani alisema kazi ya ukombozi ni kazi rahisi?
Kitila sie tunakufahamu sana hili jimbo hamuwezi kulipata ukifikiria timu ya ccm dhidi CDM Utaona wazi kabisa mna kazi ngumu na hamuwezi kuifanikisha. Rasilimali CDM mlizo nazo ni ndogo, Chama kiko hoi bin taaban hakina vyanzo vya mapato zaidi ya ruzuku, na asikudanganye mtu kampeni bila pesa hakuna kitu, wakati wa watu kujitolea bure bure umekwisha
 
Hakuna Uslatan Dogo kashinda kura za maoni au mtu hukiwa mtoto wa kiongozi Tanzania ni marufuku kugombea nafasi yoyote?

Simaanishi kwamba hajashinda!

Ila kama siyo uchu wa madaraka!
Huyu bwana mdogo angeendelea na fani yake ya BANK aachane na mambo haya ya siasa kbs!

Lakini siyo mbaya maana huu usemi ndiyo utakamilika ya kwamba "Kupasuka kwa pakacha ni nafuu ya MCHUKUZI"

Tuombe uzima na tuone meli itakavyoanza safari!
 
Angekuwa mtoto wa Mbowe ingekuwa balaa! ila kwa kuwa ni wa kutoka kwa watani zetu hata wao wanashangilia na kuona ni sawa tu! Hovyo kabisa!!!!!!!!!!!!!!
 
Usultani CCM ni kama kazi kama hamna majina yanayojulikana mtabaki kubeba mabegi ya kina Nape Nnauye wenye majina hadi mabega yaende upande.

Mkuu, kabla ya kuandika hayo maneno yako ungeangalia upande wa pili wa shilingi.

Inawezekana kabisa na wewe ukawa mbebaji tu wa mabegi ya kina Ndesamburo, Mbowe, Lissu.

Huwezi kupata nafasi ya kupata ubunge ukiwa nje wa hizo koo.

Sioni Sumari, kapambana kwenye kura za maoni mpaka kashinda, naona toka usikie huyo kijana wa Sumari, kapitishwa na CCM unaangaika una pakushika na bado.

Hivi ukiwa mtoto wa kiongozi katiba inakukataza kugombea nafasi yoyote?
 
Angekuwa mtoto wa Mbowe ingekuwa balaa! ila kwa kuwa ni wa kutoka kwa watani zetu hata wao wanashangilia na kuona ni sawa tu! Hovyo kabisa!!!!!!!!!!!!!!

Mkubwa!

Mi naona hii furaha yao itawagharimu sana.
Kama leo nimepata habari toka kwa mmoja wa wadau toka pale palengwa ikisema tangu morning yule dogo anawapa raia chochote na hata watu wengine wakahisi mambo mengine.

Ila kwa kuwa tuna washikaji wametinga pale ngoja nitapandisha yote yaliyojiri leo pale kitaani.

Aluta Cont,,,,,,,,,,,,,,,!
 
Kwa kungezea tu, EL atatumia nguvu za ziada sio tuu kumsupport mkwe, au kuproove kwa CCM that he is still in controll, hapa ataongeza nguvu kuwathibitishia Wameru kuwa yuko nao kwa vile japo wengi wanamfahamu kama ni Mmasai, kiukweli EL sio Mmasai ni Mmeru!. Hivyo atampigania mkwewe kwa nguvu zake zote ili pia to maintain his status quo yake ya Kimeru!.

very true
 
Mkuu mimi nililizungumzia mapema hata arobaini haijaisha mtoto wa marehemu anaanza kugombea urithi, kiafrika hii haikubaliki. CCM wamefanya kosa kubwa sana unaona hata kura zake alizopata hazi reflect matakwa ya wameru na wanaCCM wenzake. Hapa amechaguliwa si kwa merits alizonazo ila kwa sympathy ya baba yake na hicho ndicho kitakacho wa cost CCM.[/QUOT

Amemwua babake huyo
 
Mkuu mimi nililizungumzia mapema hata arobaini haijaisha mtoto wa marehemu anaanza kugombea urithi, kiafrika hii haikubaliki. CCM wamefanya kosa kubwa sana unaona hata kura zake alizopata hazi reflect matakwa ya wameru na wanaCCM wenzake. Hapa amechaguliwa si kwa merits alizonazo ila kwa sympathy ya baba yake na hicho ndicho kitakacho wa cost CCM.[/QUOT

Amemwua babake huyo

embu kuwa mstarabu ndg yangu , haya sio maneno ya kutamkwa na mtu aliyesoma .
 
Sumari 361
Sarakikya 259
Elilehema Kaaya 205
Elishilia Kaaya 176

Anthony Musami 22 na
Ndg Urio 11

Utawala wa kifalme wa mbio za kupokezana vijiti kupokezana kama Korea vile vile.
Mambo ya uroho wa madaraka CCM hata watu wa familia moja wanashindwa kuachiana nafasi. Hizo kura za akina Kaaya ukijumlisha zilitosha kumwibua mmoja kuwa mshindi, mapato ya kugombania nafasi wameishia kugawana kura na hakuna mshindi.
​

uwe unauliza kwanza. Haya ni majina kama ya makabila ya kwenu kama vile Sanga, mwakajinga, Msuya, kalinga, Filikunjombe, Mrisho, Shomvi na Masanja si lazima muwe ndugu!! Au baridi ya Ulaya ulikosoma bado imekugandisha?
 
Back
Top Bottom