Sioi Sumari achaguliwa na CCM kumrithi baba yake Arumeru Mashariki!

Mimi sikubaliani na siasa za CCM, lakini nitapinga wale watakaomgroup huyu jamaa na kina Ridhwani. Namjua Sioi tangu akiwa Forodhani Primary School, Lutheran Junior Seminary na hata baada ya kwenda kusoma Uingereza. Ni kijana mstaarabu na mwenye upendo. Nashindwa kuelewa kwa nini yeye amegombea badala ya kaka yake Kisali, kwani yeye ndio alikuwa na trait za siasa katika familia yao.
Kisali, AKA K-SOLO!
 
and that has been my point...:poa
 
Chadema wapange timu bora kabisa kule! Wawatumie zaidi vijana wenye ushawishi! Ikitokea Chadema mkashindwa kulitwaa jimbo hili nawahakikishia tutegemee msiba mzito 2015! No justification this tyme mjue hilo,sijui kura zimeibiwa au chochote hatutaki kusikia! Tumewaamini lazima mshinde! Kama tunashindwa now ccm ikiwa mahututi ikiimarika kidogo kuna upinzani kweli? Chadema lazima mshinde na kampeni zenu ziwe Cost effective,efficient and economy! Lazima muwe na watu wanaojitoa kutumikia wananchi ili kuja kukomboa nchi mikononi mwa ccm iliyochoka! Msiwe na wanachama wa kulia na posho ktk harakati hizi ngumu! Fanyeni kazi usiku na mchana kwa gharama kidogo lakini mkiwa na timu ya watu wenye ari kubwa! Msiwaonee haya ccm hasa huyo EL ambaye atakuwepo huko! Waambieni yote wananchi kwa lugha nyepesi kabisa! Mwisho uchaguzi wa kuteua mgombea wenu uwe wa uhuru na haki! Haka kauchaguzi kadogo hatutegemei malalamiko! Wekeni process wazi ili hata atayekosea isíhitaji maelezo! Kila lakheri!

Nashukuru umemaliza kila kitu mzee wangu.
 
Ama kweli utawala wa Kislutan bado ipo hapa Nchini!

Lakini kwa hawa mafisadi hili litakuwa fundisho ya kwamba Watanzania wamekumbuka shuka.

Hapa Arusha siyo Igunga iliyochakachuliwa mchana kweupe!
 
Tulijua tu magamba watatu iga kumsimamisha kijana, wote hawa ni vijana kwa hiyo wana mvuto mkubwa kwa jamii ya meru. Mchuano utakuwa mkali
 
Hatimaye mtoto wa Sumari (RIP) amechaguliwa na chama chake kupeperusha bendera ya CCM.

Hongera CCM kwakumpitisha "Mchaga" when it is convinient.
I hate to say this lakini I have to say it ili watu kama kina Nape na yule cheap politician kule Arusha waache ku-attack makabila ya watu kwa mtaji wa siasa.
 
Du tumefika huku kwenye ukabila tena duu, halufu mbaya hii!
 
Sioi is one of the brothers i admire a lot ila sijui kwanini kaingia huko kabisa.... anyway with EL behind him, he has a chance
the guy is gud. Naona yeye ndiye right person kwa Arumeru.
 
Tatizo kubwa ninaloliona Kwa huyu kijana ni timing. Kiafrika ilikuwa ni mapema mno kugombea baada ya kifo cha babake. Kimsingi bado yupo msibani na hii haiwezi kupokelewa vizuri na wapiga kura, unless uafrika wa wameru ni tofauti!
Nilikuwa sitegemei poor analysis kama hii kutoka kwako.
 
Tatizo kubwa ninaloliona Kwa huyu kijana ni timing. Kiafrika ilikuwa ni mapema mno kugombea baada ya kifo cha babake. Kimsingi bado yupo msibani na hii haiwezi kupokelewa vizuri na wapiga kura, unless uafrika wa wameru ni tofauti!

Mkuu Kitilia Mkumbo,
Ni mapema mno kusema haya maneno huwezi kuhukumu kitu ambacho bado akijotokea, siasa zina mbinu nyingi, CCM wao ndio wameona mtu muhimu kwao, ni kazi kwenu na nyie Chadema, kuchagua mgombea makini msijiliwaze na kujifariji kuwa mtashinda Arumeru kwa sababu CCM wamemsimamisha Sioi Sumari, baada ya matokeo mnaweza msiamini macho yenu.
 
Ama kweli utawala wa Kislutan bado ipo hapa Nchini!

Lakini kwa hawa mafisadi hili litakuwa fundisho ya kwamba Watanzania wamekumbuka shuka.

Hapa Arusha siyo Igunga iliyochakachuliwa mchana kweupe!

Hakuna Uslatan Dogo kashinda kura za maoni au mtu hukiwa mtoto wa kiongozi Tanzania ni marufuku kugombea nafasi yoyote?
 
Mkuu Kitilia Mkumbo,
Ni mapema mno kusema haya maneno huwezi kuhukumu kitu ambacho bado akijotokea, siasa zina mbinu nyingi, CCM wao ndio wameona mtu muhimu kwao, ni kazi kwenu na nyie Chadema, kuchagua mgombea makini msijiliwaze na kujifariji kuwa mtashinda Arumeru kwa sababu CCM wamemsimamisha Sioi Sumari, baada ya matokeo mnaweza msiamini macho yenu.

Mkuu unadhani ni nani atashinda?
 
Sioi Juu!!!!!!!!-----------------------------------------------------------------.I told you guys kuwa maji yanafuara mkondo
 
Tatizo kubwa ninaloliona Kwa huyu kijana ni timing. Kiafrika ilikuwa ni mapema mno kugombea baada ya kifo cha babake. Kimsingi bado yupo msibani na hii haiwezi kupokelewa vizuri na wapiga kura, unless uafrika wa wameru ni tofauti!
Kitila tunataka Chadema mshinde no justification this time! Mkishindwa Arumeru Ikulu ni ndoto! Ni chungu lakini ndio ukweli! Hakuna sababu ya kushindwa Arumeru! Angalieni timu mnayoipanga kusimamia kampeni kule! Msiende kujazana tu bila mpango! Tunataka kuona mbinu za kisasa na value for money ina apply kama chama cha kuigwa mfano!
 
Hadi ubunge wanarithishana!?kweli kazi ipo Tz,ngoja tuone wana Arumeru wataamua kuendeleza siasa za baba na wana au wataamua vinginevyo
 
the guy is gud. Naona yeye ndiye right person kwa Arumeru.
Mkuu Rejao,
Nadhani huyo kijana atapeleka msiba mkubwa ndani ya Chadema.

Pro-Chadema JF wamebaki kujiliwaza na kujifariji huku wakitapatapa hovyo.

Wengine wanasema kachagulia kislutan wanasahau kuwa ndani ya Chadema wapo watu wengi tu wa familia moja.
 
Tatizo kubwa ninaloliona Kwa huyu kijana ni timing. Kiafrika ilikuwa ni mapema mno kugombea baada ya kifo cha babake. Kimsingi bado yupo msibani na hii haiwezi kupokelewa vizuri na wapiga kura, unless uafrika wa wameru ni tofauti!

kamanda wameru ni tofauti,
  1. unakumbuka ule mtafaruku wa walutheri?
  2. unakumbuka jamaa wanaongoza kwa kuua watu kwa mawe?
  3. unajua wameru ni kabila moja lenye kalcha ya sultanate au kingdom na inafanya kazi
  4. unajua kwamba jamaa wanaabudiana??

the boy is an excellent personality, ila sijui ata-fair vipi kwenye hili... he has a lot of respect from ordinary youth kwani ni mtu wa watu wote,
 
Back
Top Bottom