Inategemea huyo mlezi aliye na mtoto/watoto yuko na hali gani kimaisha. Endapo mzazi pekee hajimudu na upande wa pili ungeweza kuwa na msaada basi mambo yatakuwa magumu, lakini kama mzazi huyo atakuwa na hali nzuri kimaisha na atakuwa commited kwa watoto wake basi maisha yanakuwa rahisi. Uzoefu wangu unanambia kwamba single mum anauwezo wa kutunza watoto vizuri kuliko single dad - hasa watoto wakiwa wadogo kwa kuwa mama ni mlezi wa moja kwa moja kwani baba atahitaji msaidizi na hapo matatizo yanaweza kutokea. Anyway si jambo la kujuta kuwa single mum/dad kwa kuwa wako wazazi wanaishi pamoja lakini malezi ya watoto yanawashinda, wakati wale wanaolea pekee wamefanikiwa kuwalea watoto wao vizuri kwa malezi mema na kuwapatia kila kinachohitajika. All in all malezi ya watoto yanahitaji wazazi wote wawili walio makini na wenye kujali familia. I am a single mum and I have not regretted for being one. Nina watoto ambao wanaishi vizuri kuliko baadhi ya watoto wanaolelewa na wazazi wawili. I thank God for that.
Malezi ya mzazi mmoja Mungu atusaidie sana kama mi ninao 3 baba yao ashatangulia mbele ya haki. Kuna wakati inaniumiza sana ingawa kabla yakufariki tushakuwa tumetengana. Tukubali tukatae nikujidanhanya na kuonyesha tu majasiri ila mambo ni magumu