Single mums and dads come this way

Single mums and dads come this way

Hakuna dhambi mbaya kama kujidanganya mwenyewe,HUWEZI KAMWE kuwa na furaha yakulea mtoto peke yako hata uwe na mali na utajiri mkubwa kiasi gani,kitu kinaitwa FURAHA huwa hakilinganishwi na mali hata kidogo,kinalinganishwa na usawa,haki na amani katika mazingira uliyopo,kuwa na mtoto unamlea peke yako kila ukimuangalia na yeye akikuuliza mzazi mwenzako(baba/mama) yupo wapi kisha ukakosa majibu SAHIHI naya kweli hapo ni LAZIMA tu amekunyima AMANI na hapo HUWEZI kusema kamwe una maisha ya furaha na amani eti kwa sababu una mali,ni UPUMBAVU ulioje uliochanganyikana na fikra mfu sanjali na ubinafsi wa hali ya juu kusema kuwa una Furaha na amani ya wewe/mimi wakati kuna kiumbe anayetupa kero ya moyoni kwa kila kumuona au atapotuuliza,HESHIMA na UBINADAMU wetu haupimwi kwa kiwango cha mali,kinapimwa kwa jinsi unavyojali furaha ya mwingine,kwa sababu furaha yako/yangu inakuja pale unapompa furaha mwingine,hii ni toka misingi ya dunia hadi milele..DAMU ya MTU haipotei kamwe,itachukua miaka mingi ijayo ila ipo siku tu itajulikana na hii ni kawaida,haijawahi kuwa kinyume,tutawaficha watoto wetu kuhusu mzazi wake halisi ila siku atakuja mtafuta tu..Watu wataandika hapa kujifariji ila moyoni tunajua jinsi gani tunavyojikaanga na haya mafuta,sisi siyo wanyama kuwa ulibeba tu mimba au kubebesha mtu mimba halafu tusiwe na uchungu wakupata uungwaji mkono upande wa pili katika malezi...kimsingi tunahitajika kuwaeleza ukweli hawa watoto wetu na siyo kuwaficha maana bado haitusaidii hata kidogo,unampa mtoto uongo mkubwa halafu bado moyoni unaumia...Kama ulimpa mimba binti wa watu na ukamkimbia,mtoto akija kwako mueleze ukweli uwe huru hata kama atakuchukia ila kwa MUNGU wako umenawa mikono,kama ULIOLEWA/KUWA KATIKA MAHUSIANO kisha ukaachika katika mazingira yakutokuwa muaminifu(kuchepuka) wakati huo ukiwa na mimba muambie ukweli mtoto kuliko kuendelea kumlisha maneno ya sumu kuwa baba alikutelekeza..UKWELI HUKUWEKA HURU TUSIJIFARIJI KINAFKI(tusijipake mafuta kwa mgongo wa chupa).
 
  • Thanks
Reactions: bae
Kutaka sana ukubalike na jamii unayoishi.ni dalili ya kuwa hujikubali, ukijikubali hutajali wengine wamekuweka kundi gani.

Ukiyakubali maisha yako, hutataka kuhamishia uchungu wako kwa mwingine. Mama kutomwonyesha mwanaye babake ni kuvunja haki za mtoto. Ni mama?Ndio, lini yeye si Mungu wa kuamulia baba na mtoto wakutane lini

Ni hayo tu.

Kumbe kujikubali ni kuishi kwa ukweli na vipimo vya watu wengine. Kwamba kuwa treated tofauti kwa sababu wewe ni binadamu shoga au mweusi au mzazi pekee ni sehemu yako inherent unatakiwa kuishi nayo. Basi sawa. Nashukuru kwa kunielimisha. Penye utulivu mtu hapayuki.
 
I am not worried about his future coz if you are a christian the bible says in Jeremiah 29:11 "For I know the plans I have for you,” declares the Lord, “plans to prosper you and not to harm you, plans to give you hope and a future."

My boy's future is secure with or without me.

i think i like ur positive attitude n energy... Impressing!!
 
Malezi ya mzazi mmoja Mungu atusaidie sana kama mi ninao 3 baba yao ashatangulia mbele ya haki. Kuna wakati inaniumiza sana ingawa kabla yakufariki tushakuwa tumetengana. Tukubali tukatae nikujidanhanya na kuonyesha tu majasiri ila mambo ni magumu
 
Ukweli unauma ujue. Mwanangu umlee vizuri, siku nikija kumchukua nimkute akiwa vizuri.

Wewe si unajua kushabikia sana? Sasa utakula jeuri yako.

Hata kuamua kuwa kimya ni hekima kubwa, sidhani kama kuna haja ya kunukuu na kujibu kila comment; mnatupotezea mtiririko wa michago inayojenga kwa kuingiza mambo binafsi.

Nimeongea nawe bro, kwa kuws comments zako zinamlenga mtu kibinafsi na una muattack. Jikiteni kwenye hoja.

Vv
 
Hata kuamua kuwa kimya ni hekima kubwa, sidhani kama kuna haja ya kunukuu na kujibu kila comment; mnatupotezea mtiririko wa michago inayojenga kwa kuingiza mambo binafsi.

Nimeongea nawe bro, kwa kuws comments zako zinamlenga mtu kibinafsi na una muattack. Jikiteni kwenye hoja.

Vv
Poa nimekusoma.
 
Thread hii imenifunza mambo mengi sana.Ila yote kwa yote Mzazi hana haki yoyote ya kumzuia mtoto kumfahamu mzazi mwenza yaani baba au mama. Kumdhulumu mtu haki ya kumjua mzazi wake ni sawa na kudhulumu haki yake yoyote ya msingi ambayo inampa furaha. Sitaki kuandika mengi nisije kuharibu uhondo uliokwisha weka humu jukwaani. Shukrani kwa wote walio tayari kuwajibika kwa makosa yao na hata ya wengine. Ila kamwe usiruhusu emotions zake ziamue namna yako ya kufikiri.
 
shem naangalia movie hapa inaitwa single moms club. usingle mom si mchezo. hongera zao sana.

Husninyo, kuna dada nimemsoma hapa nikamwelewa kuwa alikusudia kuwa single mother na mara baada ya kujauzito tu akamficha mzazi mwenziwe na kukata mawasikiano naye.

Ukweli ni kuwa simuelewi huyo dada, nadhani atakuwa alipata shida wakati anakua [grow] ama kuanzia kwa wazazi wake, au kuna ndugu zake walipata shida kwenye mahusiano yao ya kiunyumba yaliyosababishwa na waume zao.

Nasikitika amemnyima mtoto wake haki ya msingi sana: kumjua na kulelewa na baba yake. Matokeo ya hili hambo, kama mtoto hana akili nzuri, au neema ya Mungu haijaingilia kati maisha yake, mama yake asiji kushangaa mtoto wake hayuko normal, hata kukosa hisia za kimapenzi kwa opposite sex, na moja kati ya matokeo yake anaweza kuangukia kwenye mapenzi ya jinsia moja [God forbid].

Vv
 
Hili tatizo lipo sana huku ulaya single.mom ni wengi sana hasa dada zetu wa kibongo,tatizo ni.kuiga mambo ya wazungu hakuna heshima kwa mwanaume pia kutaka haki sawa ndani ya nyumba hapa ulaya mwanamke anakutukana na ni.mkeo wa ndoa kabisa,ukija juu fasta anapigs simu police na unakuja kuchukuliwa na kuwekwa ndani,sasa kwa style hio mwanaume ukitoka huko ndani tiyari lazima lazima ufunge vilango vyako hata kama una watoto,ndio chanzo cha usingle mom,unakuta mwanamke anajisifia bila kujua ndio chanzo,pia kuhusu gharama za mtoto mwanamme unakatwa juu kwa juu kwenye mshahara na serikali anapewa mwanamke ndio furaha yao,lkn baada ya muda wanajuta kuona tena wanapata pesa lkn hakuna mme,basi wahagaika kweli wengine wanajikuta wamekuwa malaya tu,nani aoe mwanamke ana watoto 2 hapa ulaya,inabidi mwanamke anajikuta anateseka na pia anatesa watoto pia,wanawake wengine ndio unakuta wanatafuta vijana ambao hawana vibari vya kuish ulaya ndio wanakuwa sex machine zao,kwa malipo ya kula na kulala.kwa hiyo single mom sio kitu cha kujisifia hata kidogo mara nyingi chanzo ni wao.
 
Hiyo movie bongo inapatikana mitaani? Kwa mfano down town kwenye maduka makubwa?

Comrade Matola, your insights on this movie would be highly rated...! ..teh!
 
Last edited by a moderator:
Wewe hapa inaonekana kama ulipitia shida kwenye huu usingle mama.


Halafu hapa chini unasema mnafanana na Miss Kim!!! Mwenzio kachagua kuwa single mama na anasema anafurahia hali hiyo iweje mfanane???!!

Unajuaje na mie nimechagua kuwa single mum kama yeye??
 
Last edited by a moderator:
umeongea point nzur sana. Hata mm nmeliona hilo watu walio wengi wanaelekeza lawama na chuki kwa mzazi mmoja ambaye n mwanaume.

Nmesoma commet ya mdau mmoja kafikia hadi hatua ya kumsema baba yake kiaz, lakn yote hayo ni kutokana na hasira zilizopandikizwa kwa upande mmoja.

Mm ningeomba watu hasa waliolelewa na mzaz mmoja wasifikie hatu ya kuwa na chuki na hasira sana, badala yake wajaribu kuvuta picha kutoka kwenye jamii hii tuliyo nayo.

Watambue kuwa kero na changamoto kama za kubambikiwa mimba, kutegeshwa mimba kwa lengo la kupata ndoa, kutopata mimba huku wakiwa kwenye mahusiano ya mwanaume zaidi ya mmoja hayo ni miongon mwa mambo yanayochangia akina mama kukimbiwa.

Tatzo wanapata malalamiko toka kwa mama tu lakn hata kama ingetokea nafas naye baba akajieleza kuwa kwann alimkataa nadhan pasingekuwa na hasira sana.

Hayo mambo wakat mwingne akina mama ndio huwa chanzo.
haya maswala ya single mums ad dadys kwa watu wenye kuona mbali huwa hawayazungumzii kuna factor nying na scenario tofauti sana zinazosababisha jamani kuna mateso mengi kwenye huu ulimwengu.mimi nawiwa kusema tu kwamba na Kongosho unisikie baba /mama ambaye hataki kumtunza mwanae kwa hata ushauri hata kumtakia hali anaishije anaishi wapi anakula nini hiyo haki ya msingi mnayoipigania eti ana haki yakuongea nakukutana na baba/mama yake kwangu haipo kabisa watakutana huko mbele ya safari mungu akipenda wakutane ila sio kwa gharama zangu hata sent 1 mtoto amtafute kwa his/her own risk sintaendekeza ujinga huo alwaz hata yuko hai naasume alishakufa long time.kuna watu waajabu ndugu zangu msitake kujua.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom