Single mums and dads come this way

Single mums and dads come this way

I wish watu wangeacha kuwa kutoa hukumu, tuwape nafasi single parents watoe changamoto za maisha bila wenzi/wazazi wenzao.

I wish niseme kitu ila nahisi nitatonesha kidonda ambacho kimeshapona...

Sitaki kukumbuka, sitaki kuwaza sitaki kuishirikisha akili yangu kuyakumbuka na kuyapatia uzito maisha ya single mum.... Naishi kwa Neema ya Mungu, nikiiona leo Alhamdulillah siku ikipita Ameen....
 
I am proudly a single parent and i have never regretted my decision to become one. Actually becoming a mother has been one of my greatest achievements so far. Waking up each morning besides my beautiful baby is a true blessing and i always thank God for this beautiful opportunity to be called a mother.

Just to recap a bit about my past.....nakumbuka ilikua mkwa 2010 nilipokutana na huyu kaka and right from the word go i knew he was bad news ila i have always had a thing for "bad boys", huwa niko attracted to such. Basi one thing led to another and all was beautiful & dreamy, everything i would have imagined about him came true. He gave me 6 good months of nothing but pleasure & heaven on earth (hihihihihiii). Anyways to cut the long story short, nikaja gundua i was 2 weeks pregnant surprisingly i was at peace with myself. Right from the word go i knew i wanted to have this baby and one thing i was certain about was that there was no way i was getting this dude involved. So taratibu i started cutting him loose, nikaanza punguza mawasiliano, akitaka tuonane mm nampiga chenga. Kuna kipindi akawa anatamani sana tuonane but mm nikawapa natafuta visingizio, luckily tupo mikoa tofauti & didn't have common friends so interaction was minimal.

Nikiwa almost 9 months pregnant nikakutana na ndugu yake kwa bahati mbaya, huyo ndugu yake si akaenda mwambia jamaa. He flew from wherever he was to where i was to come confirm if i was truly pregnant, tena alinifanyia suprise nisijue kama anakuja. We talked a lot that evening, akaniuliza maswali mengi sana & i never gave him the answers he was looking for. Eventually akarudi zake kwao na life likaendelea. He comes to visit whenever he's around & he supports us as a friend na hadi leo hii sijawahi mwambia kama yy ndo baba wa mtoto wangu.

Ukweli ni kwamba i had my reasons for keeping him at bay about my son's father's identity, hiyo ni siri yangu & i believe that God will understand, hopefully my son will come to understand me when he finally grows up enough to comprehend such things.

Being a single parent has been a blessing in disguise, nimepata breakthroughs za ajabu mno katika shughuli zangu & my life has changed for the best. Lifestyle yangu has changed for good & if i had a second chance at life i wouldn't change a thing about it! I am happy & thankful every single day.

Mnisamehe kwa Kiswaglish changu na story ndefu..hihihihiihihhiii... bottom line is i am a proud parent to the most amazing boy under the sun & would forever be grateful to my "bad boy" for giving me such a beautiful baby, by boy is gonna go places, Mungu atupe uzima tu!

Miss Kim pole na hongera, najua kuna watu hawatakuelewa ila mimi ninakuelewa make tunafanana kwa 99%.

Nahisi sababu zako na zangu zinaweza kufanana kwa asilimia kubwa....
 
Last edited by a moderator:
I wish niseme kitu ila nahisi nitatonesha kidonda ambacho kimeshapona...

Sitaki kukumbuka, sitaki kuwaza sitaki kuishirikisha akili yangu kuyakumbuka na kuyapatia uzito maisha ya single mum.... Naishi kwa Neema ya Mungu, nikiiona leo Alhamdulillah siku ikipita Ameen....

Unajua charminglady, ukikaa na kitu rohoni kinakuumiza zaidi na zaidi...spit it out na utapata relief �� kubwa mno.
Mungu akupe nguvu za kuweza kumlea mtoto katika hekima na kimo huku akimpemdeza Mungu na binadamu. Usife moyo.
 
Last edited by a moderator:
polen kwa changamoto za kuwa single parents.Devotha story yako imenipa simanzi.Na imebadirisha kabisa mtazamo wangu kwenu!!

Nafikiri moja ya chanzo cha kuwa s/mums ni kwamba wanaume wanao wapenda wanawake toka mioyoni hawapewi nafasi.Wale playboys ndio wana nafasi kubwa kwenu na ndio waumizaji wakubwa.Na kuwa s/mum sio choice ya mtu sema kuna mazingira yanalazimisha hali hiyo.Pia wenye status siyo wako mstari wa mbele kuwaaminisha watu juu ya maisha ya ndoa kama sio kitu vile!
 
Mkuu Eli79 hata nikisema won't help... 12yrs nshalia, nshaumia na sasa meamua kunyamaza tu....

Nishaomba ushauri jukwaa la Sheria lakini wapi haikusaidia, yote waliyokuwa wananishauri yalikuwa yana base kum favor baba wa mtoto...
 
Ooh..pole kwa ugumu huo. Naamini unapata ahueni ukimuona mtoto alivyokuwa mkubwa sasa. Japo malezi yake ni magumu pia. Mungu akutie nguvu rafiki.
 
Last edited by a moderator:
polen kwa changamoto za kuwa single parents.Devotha story yako imenipa simanzi.Na imebadirisha kabisa mtazamo wangu kwenu!!

Nafikiri moja ya chanzo cha kuwa s/mums ni kwamba wanaume wanao wapenda wanawake toka mioyoni hawapewi nafasi.Wale playboys ndio wana nafasi kubwa kwenu na ndio waumizaji wakubwa.Na kuwa s/mum sio choice ya mtu sema kuna mazingira yanalazimisha hali hiyo.Pia wenye status siyo wako mstari wa mbele kuwaaminisha watu juu ya maisha ya ndoa kama sio kitu vile!

Sipendi hali hii. Natamani mwanangu apate mapenzi ya pande zote kama nilivyopata mimi. Najua the dad I want is still there inside him and I want to bring him out. Nataka kuendelea na maisha yangu bila majuto labda ningefanya hivi au vile kwa ajili ya mwanangu na mimi pia sababu pamoja na yote bado nampenda sana. Sipajui kwao lakini kwa details kidogo nilizonazo ntafika at least nijue something about him
 
Am proud to be a single parent, sijutii na sijawahi kujutia! I thank God kwa maisha ninayoishi maana ninajua ni kwa neema yake tu, thanks Karucee tupo na tunasonga mbele

Miss you mdada, tutafutane!
 
  • Thanks
Reactions: ram
Kila la kheri, Mola akukuzie....ila kwa sababu ni dume halitokusumbua sanaa...Mtoto wa kiume huwa na mapenzi na mama yake....Nadhani angekuwa wa kike ingekuwa story nyingine....!

hii ni imani tu. mimi wa kike lakini sikuwahi kumsumbua mama kuhusu baba, wala sikuwahi kujiuliza kwa nini hayupo. labda kwa sababu na watoto wengine majirani pale kijijini walikuwa wanakaa hata miaka mitano hawajaona baba zao (baadhi ya mibaba ya kimachame ilikuwa na tabia ya kukaa mikoani na kuacha wake vijijini kwa muda mrefu. wastaarabu kidogo walikuwa wanakuja krisimasi). pengine labda ni kwa kuwa nilishashiba upendo wa babu na bibi walionilea toka mwaka mmoja mpaka 12 au kwa kuwa sikuwahi kukosa chochote ambacho kingenifanya nihisi baba angekuwepo mambo yangekuwa tofauti. nilimuuliza mama baada ya kutumwa na jirani mmbea (mama stivinii), na mamangu alihisi nimetumwa ila nikakanusha na sikurudi kwa jirani kutoa ripoti.
 
mmh Mungu tusaidie.
Inauma sana sanaaaaaaaa!
Imagine mtoto kunasiku akiamua anakuita Fadher na siku nyingine mother.
Ukifikiria babayake ulivyomwambia uko na ujauzito wake alikuambia toa haraka iwezekanavyo
 
polen kwa changamoto za kuwa single parents.Devotha story yako imenipa simanzi.Na imebadirisha kabisa mtazamo wangu kwenu!!

Nafikiri moja ya chanzo cha kuwa s/mums ni kwamba wanaume wanao wapenda wanawake toka mioyoni hawapewi nafasi.Wale playboys ndio wana nafasi kubwa kwenu na ndio waumizaji wakubwa.Na kuwa s/mum sio choice ya mtu sema kuna mazingira yanalazimisha hali hiyo.Pia wenye status siyo wako mstari wa mbele kuwaaminisha watu juu ya maisha ya ndoa kama sio kitu vile!

nikwambie kitu? kama unajua saikolojia kidogo au wale wa dini wanasema kurithi roho ya kitu flani. uchaguzi wa mwenzi kwa mtoto huchangiwa kwa 90% na mahusiano yake na wazazi na mahusiano ya baba yake na mama yake. mara nyingi mtoto aliyeshuhudia mzazi mmoja akimnyanyasa mwingine atakuja kuchagua mwenzi atakayemnyanyasa yeye ili arudi kwenye mahusiano aliyoyaona utotoni. au atakataa mahusiano hasa ndoa kwa sababu ndoa=mateso, au atakuwa anachagua wenzi wenye matatizo matatizo akiwa na nia ya kuwaokoa kwenye matatizo yao kama alivyokuwa akitamani kumuokoa mama yake kwa mfano (ila yeye anakuwa hajitambui). ndo unamuona kijana kila siku anaopoa wanawake vimeo tu, hawaishi kumliza mpaka anajiona mwenye mikosi kumbe akiwaona anamuona mama yake. ukiona mwanamke anayevumilia vipigo na matusi fuatilia makuzi yake. ukiona mwanaume anapiga na kutukana mwanamke fatilia makuzi yake.

mtoto aliyekosa mapenzi ya mzazi wa jinsia tofauti naye mara nyingi hukataa wenzi wanaompenda, badala yake hupenda wale ambao hawampendi, ambao watamuumiza kama mzazi wake alivyomuumiza au ambao hawatampa mapenzi ya kweli au ya kudumu. Mtoto wa aina hii akili yake iliyo hai (conscious mind) inajua kabisa kuwa ana uwezo wa kupenda, na anavutia sana tu watu wenye upendo lakini hujikuta akiwakataa wanaompenda na kuwakimbilia hata kwa gharama wale wasiompenda. akili yake ya zamani (uncoscious mind) ndo inamtuma huko kwenye maumivu. hao play boys nao wengi wao ni waathirika wa makuzi mabaya. wengi waliona kwa baba zao. nao pia wanaogopa upendo. na kama mzazi hakuwepo kabisa mtoto anakuwa hana kitu cha kumfanya avutiwe kuwa na mtu wa jinsi ya tofauti maana hana hiyo picha/schema kwenye ubongo wake.

watoto wanaopata mfano mbaya wa wazazi either utawakuta kwenye ndoa zenye kila aina ya vitimbi lakini hawatoki kwa kuwa wako kwenye utumwa wa kihisia, au utawakosa kwenye ndoa kwa sababu wanajua ndoa ni jehanam na haina maana.

Mtoto aliyekulia kwenye upendo na maelewano atapenda sana ndoa na familia, na kama ni binti hataolewa na yeyote mpaka apate mwanaume anayefanana na babake, atakayempenda kama baba alivyokuwa akimpenda mama na alivyokuwa akimpenda yeye. Na kwa wanaume hivyo hivyo. Kwa hiyo ukiona kuna wanawake wanakimbilia bad boys ujue kuna baba yake alimtenda. wachache walitendwa na wapenzi wao, lakini mpaka wakachagua watu wa kuwatenda kuna kitu kiliwasukuma. Kama wapo wasiotaka ndoa na wanailaani elewa kuwa wanamaanisha. waliona wapi ndoa nzuri? nani aliwapenda mpaka nao waamini kuna upendo duniani?

kwa hiyo ukiona hivyo ujue kuna wazazi hasa wa kiume hawakufanya majukumu yao sawa sawa. na ndiyo maana popote ninapokuwa napenda kusisitiza ubora wa malezi maana najua ustawi wa mtu binafsi na taifa kwa ujumla unaanzia kwa mzazi/mlezi. Mtu aliyeathirika na malezi anaweza kubadilika lakini si kazi ndogo. ni kazi sana ila inawezekana.
 
Sipendi hali hii. Natamani mwanangu apate mapenzi ya pande zote kama nilivyopata mimi. Najua the dad I want is still there inside him and I want to bring him out. Nataka kuendelea na maisha yangu bila majuto labda ningefanya hivi au vile kwa ajili ya mwanangu na mimi pia sababu pamoja na yote bado nampenda sana. Sipajui kwao lakini kwa details kidogo nilizonazo ntafika at least nijue something about him

natamani nikwambie kitu lakini hutanielewa. utajifunza huko huko mbele kwenye jitihada zako na Mungu akutie nguvu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom