Single mums and dads come this way

Single mums and dads come this way

Usimlaumu wa kumshangaa Kilaza huwezi jua maumivu yake alivyoona mama kakimbiwa hana pakuanzia na watoto wanasubiri malezi wakati baba anahangaika
na wanawake wengine,ana uchungu jinsi mama yake alivyoteseka wakati mtu wa kumsaidia alikuwepo.Kilaza sikuhukumu katika hili ila najua umejifunza kitu,pole sana na Mungu atazidi kumbariki mama Kilaza.

Zamda Geuka sijahukumu wala. Ndio maana nikasema sijavaa viatu vyake.
 
Last edited by a moderator:
polen kwa changamoto za kuwa single parents.Devotha story yako imenipa simanzi.Na imebadirisha kabisa mtazamo wangu kwenu!!


Nafikiri moja ya chanzo cha kuwa s/mums ni kwamba wanaume wanao wapenda wanawake toka mioyoni hawapewi nafasi.Wale playboys ndio wana nafasi kubwa kwenu na ndio waumizaji wakubwa.Na kuwa s/mum sio choice ya mtu sema kuna mazingira yanalazimisha hali hiyo.Pia wenye status siyo wako mstari wa mbele kuwaaminisha watu juu ya maisha ya ndoa kama sio kitu vile!

Yeah. Kuna watu wanawadanganya wanawake wengine kwamba usingle mother unalipa na ni mzuri. Wanaishia kuwa na msongo wa mawazo na kusononeka kusikoisha. Hebu imagine mtoto anauliza baba yuko wapi? Halafu asipate jibu la kueleweka, na mtu anadai I am happy kuwa single mother na sijawahi kujutia! Hell No!
 
Na wala sidhani kumwita mtu singo parenti ni kumviktimaiz au kumdivalyu. Huo ndio ukweli, malezi yanayotolewa na mzazi mmoja ni usingo parenting huo.

May be, may be not...
Ukisoma btn the lines, utaona baadhi ya waandishi wanaonesha kama ni 'ushujaa usio wa kawaida' kwa kuweza kulea peke yake? Kwa nini? Deep down kuna feelings za kujiona aidha 'weak au abnormal' kwa kulea peke yake. Anyway, mtizamo wangu, na sijawahi mwita mtu single parent wala kuhisi amepungukiwa.

Kwa nini wanaolea wawili hawajilebo kama 'double parents'? Wako okay na walivyo.

Ndo maana hii 'haki za wanawake' sijui 'usawa wa kijinsia', between the line huwa mushkeli (hata wanaodai haki wenyewe deep down wanajiona dhaifu, ila majukwaani wanajikakamua), kama uko happy na ulivyo, kwa nini upige kelele sana ili usikike?
 
Hata mie Kilaza kaniacha mdomo wazi. Siwezi kuvaa viatu vyake coz wazazi wangu walikuwepo na wote walihakikisha napata malezi bora. Lakini kumtukana mzazi kiasi hicho...mmmmh!

mkuu nadhani hujui maana ya neno MZAZI
nakama unajua basi unalitumia vibaya
 
Last edited by a moderator:
Hongera, fomu wani huyo.

Why unataka ushauri wa kisheria? Usaidiwe kulea?

Je, kulea mtoto ni material things tu?

Wala sihitaji kusaidiwa kuela, kwani mpaka huu mwaka wa 12 nimeweza sidhani kama miaka ijayo nitashindwa. Kuna masuala ya kisheria nilitaka msaada. Unaweza kutafuta huko jukwaa la sheria kwa muda wako iwapo utaweza.
 
Usimlaumu wa kumshangaa Kilaza huwezi jua maumivu yake alivyoona mama kakimbiwa hana pakuanzia na watoto wanasubiri malezi wakati baba anahangaika
na wanawake wengine,ana uchungu jinsi mama yake alivyoteseka wakati mtu wa kumsaidia alikuwepo.Kilaza sikuhukumu katika hili ila najua umejifunza kitu,pole sana na Mungu atazidi kumbariki mama Kilaza.

hahaha hapo mwisho eti "mama kilaza " u cant be serious

by the way u a right I learned something

one more thing mimi sina uchungu wowote kwakuwa sijawai kujutia kutokuwa na kubwa jinga
 
Wababa wengine wanakera sana heri
uwe na baba asiye na uwezo lakini akujali kuliko awe na uwezo halafu anakutosa,inatia uchungu sana,lakini inshaAllah Mwenyezi Mungu atufanyie
wepesi kwa kila hali..

Amen.......
 
Zamda Geuka sijahukumu wala. Ndio maana nikasema sijavaa viatu vyake.

No,nilikutahadharisha tu kuwa kauli za kilaza zisikufanye ukamshangaa,katika mazingira kama yako uliyolelewa ni ajabu hata mimi najua,lakini kwa maisha ya kilaza tusishangae inawezekana yangetukuta sisi labda tungefanya hivyo.Tuko pamoja mkuu Eli 79
 
Last edited by a moderator:
nimejikuta nacheka sana. watu tumewahi kuchukia baba zetu ila hii ya kwako kali. yaani matusi yote ya kwake! hahahaaaaa big ass, kiazi, kubwa jinga................ Ila nakubaliana na ushauri uliompa devota.

wala simchukii ila ndio ukweli huo
 
Thank you Ukweli1, very few people will understand & respect my decisions. Thank you for your prayers, thankfully i am at peace with my decision and will never live to regret. Only the person wearing a shoe knows where it pinches the most!

Sielewi kwa nini umetumia hayo maelezo kama kweli umepitia comments za Miss Kim na kuzielewa, but anyway let us agree to disagree.

To you Miss Kim, I respect your decisions and you are in my prayers.
 
Poleni single mom's wote nikiwemo na mm.ila mm ckutendwa ila Allah alinipa mtihani mkubwa alimchukua baba Wa mtoto mapema Sana maskini mwanangu hajui hata Mapenzi ya baba yakoje! ila namshukuru Mungu ajaniacha najitahidi kumtimizia mwanangu akitakacho ili asione pengo la baba.Ana 12 yrs sasa yupo std six Mdada tayari.ila nimepitia changamoto nyingi zenye kuumiza na kukatisha tamaa ila nimesimama imara.wakati Mwingine humu ndani ndiyo mabingwa Wa kutuponda single mom's bila kujua ilikuaje mpaka tukawa single mom.
duh pole sana
 
mi naona tuwaache watu wafanye wanayoona ni sawa maana kitu kisipokuwa sawa kwa wote hakiachi kuwa sawa.

Basi na wewe niache na mie nitoe maoni yangu, ni wapi nimemlazimisha afanye asichotaka? Nimeweka arguments zangu mezani, ziponde kama zilivyo.

hizi habari za haki haki wakati mwingine hazina maana.
Sijui unaposema hizi haki hazima maana unakuwa unamaanisha nini? Kwa nini mtu akiua mwanae anafungwa? Au akitelekeza kichanga ama kutoa mimba? Si mwanae bana, what do you care, labda hana uwezo wa kumtuza.


watu wengi hapa wameonyesha walijaribu kutekeleza huo wajibu wa kuwataarifu wazazi wenzao juu ya watoto lakini walichoambulia ni maumivu tu. baba hataki kumtambua mtoto lakini mama bado anang'ang'ana kumtambulisha japo kwa ndugu wa baba. haki ya mtoto kufahamu mzazi. nilishawahi kutoa mfano wa ukweli hapa juu ya binti aliyeamua kumtafuta babaye ukubwani baada ya kufichwa na mamake. yaliyomkuta yule binti hatakaa asahau. aliponea kubakwa na babake siku ya kwanza tu waliyoonana. Inawezekana kabisa mama alijua amezaa na kichaa wa ngono - si ajabu naye alibakwa. Hatujui yanayoendelea kwenye vichwa vya watu, ikiwezekana tuwaache tu.

Kwa hiyo, huyu mtoto anyimwe haki yake kwa kuhofia yaliyotokea kwa wengine? Yaani sababu mtoto mmoja alitaka kubakwa na baba yake, basi kila mwanamke akizaa aogope kumjulisha baba mtoto kwa kuhofia atambaka? Does not make any sense to me.

Kumtaarifu baba mtoto ni A, mama kuumizwa na majibu ya baba mtoto ni B, havina uhusiano.

Halafu unavyodai ni haki ya mtoto kufahamu wazazi wake mbona kule juu ulimponda mama anayedai haki ya matunzo ya mtoto mpaka mahakamani kwa kusema malezi si material tu??? Kwa hiyo mzazi wa kiume ana haki ya kumjua mwanae ila ana uchaguzi wa kulea au kuacha?

Kumjulisha baba existance ya mtoto ni A, baba mtoto kukataa kulea ni B, havihusiani.

Nilimponda kwa sababu alitaka kujua haki zake kisheria, wakati huo huo hakuwa ameweka wazi madai anayotaka kusaidiwa ni yapi na hakuwa ameweka wazi kama yeye ni mke halali ama lah. Sasa hapo asaidiweje?
Lakini pia nilikuwa najaribu kumuonesha vita anayotaka kuipigana ina tija? Uhangaike na kesi RITA weee, afu unapewa 50K kwa mwezi? Si bora huo muda utumie kuchoma vitumbua.
 
hahaha hapo mwisho eti "mama kilaza " u cant be serious

by the way u a right I learned something

one more thing mimi sina uchungu wowote kwakuwa sijawai kujutia kutokuwa na kubwa jinga

ofcoz ni mama kilaza ndo jina lako nalifahamu, kwa nini ujute kama mtu mwenyewe hajielewi? Km huyu baba mtoto wangu hamjui mtoto kabisa kaja yuko form3 nimeongea nae friendly bado anatoa ahadi badala ya kujisafisha eti ananiblock jamani kwa nini Abdulaziz wangu asiwe kilaza mwingine?Wanaume nyie!!
 
Hatuombei yatokee but huyo mtoto I don know ana umri gani, na kama si mkubwa ipo siku atakua na kuwa na akili ya kutambua vitu.... narudia tena ... hatuombei yatokee but ikitokea baba yake kaaga dunia na mtoto alikuwa na uwezo wa kumuona baba yake angali hai ukamficha utamwambia nn mtoto wako akuelewa... huoni ya kuwa utakuwa umemkosesha mtoto wako kitu cha muhim sana ktk maisha yake.... thing beyond

mi naona kuna haja ya kuanzisha uzi watu waliolelewa na mzazi mmoja waelezee uzoefu wao tujue kama waliwasumbua wazazi wao kutaka saaana kuwajua baba/mama zao na waliponyimwa haki hiyo waliathirika vipi - kwa mfano ni wangapi waliishia kuwa machokoraa kwa sababu hiyo kama Asprin alivyojaribu kuonyesha. Machokoraa ni feature ya jamii maskini tu tena zenye idadi ndogo ya single parents ukilinganisha na zile jamii zilizoendelea. Naona tunakuuuuza sana baadhi ya mambo au hatuelewi undani wake. Watoto wengi tu wako mitaani wamekimbia vita na njaa majumbani kwenye wazazi wawili. kwa tz mtoto mwenye mzazi mwenye uwezo si rahisi kuwa chokoraa - simba hata akikonda vipi hawezi kuwa kama mbwa.
 
ofcoz ni mama kilaza ndo jina lako nalifahamu, kwa nini ujute kama mtu mwenyewe hajielewi? Km huyu baba mtoto wangu hamjui mtoto kabisa kaja yuko form3 nimeongea nae friendly bado anatoa ahadi badala ya kujisafisha eti ananiblock jamani kwa nini Abdulaziz wangu asiwe kilaza mwingine?Wanaume nyie!!

zamda wangu kwani Abdulaziz alishawai kukusumbua kuhusu mzee wake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom