Miss Neddy
JF-Expert Member
- Nov 3, 2013
- 14,684
- 8,754
mbona wadada tu ndio wanafunguka........ ina maana wanaume hakuna????
wanaume mara nyingi ndo wanakana mimba na single dads wapo ila wachache sana
mbona wadada tu ndio wanafunguka........ ina maana wanaume hakuna????
Duh Kilaza siwezi kukulaumu wala siwezi kukupongeza nilichojifunza hapa ni kwamba bado una hasira na Baba yako tena baada ya kujitambua.Unajua mara nyingi watoto walioangukia katika fungu lako si kwamba walikosa mapenz na malezi ya wazazi wote wawili katika maisha yao lakini pia sheria na wakati mwingine mila zinawaweka kando katika kupata haki.
Binafsi nimelea mtoto wa Dada yangu baada ya kupata ujauzito akiwa chuo,nikaamua kumchukua mjomba nikamsomesha hadi akafikia mahali pa kijitegemea.Kipindi chote napambana na malezi yake sikumwona Baba wala nani toka hiyo familia ingawa sikupenda awe karibu nayo kwasababu za kiimani (niliogopa wangeweza kumbadilisha).
Dada yangu alikuja kuolewa na mwanaume mwingine ambaye pia sikupenda abebe mzigo usiomhusu.Maajabu yalikuja tokea wakati kijana yupo Chuo cha Ushirika Moshi Baba yake akishirikiana na Dada yangu wakafanikisha mipango ya kumtambulisha katika familia ya Baba bila kunishirikisha.Ukweli ni kwamba nilikasirika sana tena sana kiasi nakosa maelezo sahihi ya kuelezea hasira niliyokuwa nayo dhidi ya Dada na huyu Baba mtoto.Ifahamike nilianza kuishi na mtoto hata sijaoa halafu anajitokeza Pimb.i anajifanya anampenda leo.
wanaume mara nyingi ndo wanakana mimba na single dads wapo ila wachache sana
Kuna kitu nlisikia siku moja. Dada mmoja alisema hawezi kwenda sehemu na mumewe, the guy is no presentable enough to go out with her. Niliwaza sana. Inawezekana mke/mume anaishi na mwenzake lakini hata kutoka nae kwenda kwa mangi kununua sukari hawezi.
Sijajua unachojaribu kunieleza, ila kama ilivyo haki kwa mama kumtambua mtoto wake, vivo hivyo kwa baba. Kama mzazi ana pose threat kwa welfare ya mtoto, zipo restrain order kisheria.
Nachosema mie, baba na mtoto wapewe nao nafasi ya kuamua kama wanahitajiana ama lah.
Ndo kama hujui huna cha kudai,asiyekuwepo na lake halipo!Madhali kama mtu amesimama na kusema anazuia mawasiliano na ana sababu za msingi inabidi tuheshimu maamuzi yake kwasababu hatujui lolote kuhusu mahusiano yao mpaka wakafikia hapo!Unafikiri yeye hajui kama mtoto wake anatakiwa awe na father figure?Nadhani si rahisi kwa muhusika vilevile kupitia hayo.Na mpaka amepata guts za kusema ujue ni pride aloisimamia!Ukiwa na hint kuwa umezalisha mtu mahali ndo unaweza kudai, lakini kama huna hint kabisa utadaije?
Na akina mama hii ya kujua the dirty truth behind the scene inatupa kiburi sana. Kuna mdada alizaa na kijana kabla hawajafunga ndoa, kila wakigombana yule dada anamwambie mchumba wake, una hakika gani hata huyu mtoto ni wako?
Yule kijana akaona isiwe tabu, akamwambia, kama huyu mmoja tu na hatujaoana kila tukigombana ni hivi, je wakiwa watanona tumeoana? Alimwachia yule binti pete ya uchumba na kifunga uchumba na kwenda kuanza upya.
Sijui kwa wengine, ila hata mie mtu ku temper na partenity ya mtoto ni -100% wrong, regardless sie wazazi tumekwaruzana kiasi gani.
hili jina ni in memory na respect kwa my geography teacher "madam kilaza "
wanaume mara nyingi ndo wanakana mimba na single dads wapo ila wachache sana
hivi hapa wanapata picha daah!!
ukute maneno haya yanguu!!
Kongosho haya Bwana,kulea kazi jamani halafu wanangu wako 6,3 na 2yrs,nipe pole mwenzako.Ila maombi ni silahaSasa nimekuelewa, kuna mahali uliwahi komenti nikabaki :wacko:!!! Sikupi pole kwa kulea wala, maana sioni umepungukiwa, labda kwa kuondokewa na mwenza.
mi pia nimekuelewa sana
hao ndo baadhi ya me wako very selfish
nilikua na rafki yangu alikataliwa na baba ake
mama akamuonyesha mzazi wake ila baba anamkataa
siku moja tuko form three alikua anaenda shule yule binti wakakutana na baba ake ktuoni mzee kasalimiwa haitiki akamuuliza hivi "kwa nini unanikataa"?
akamjibu"sio mwanangu na mtafute baba ako"
alilia yule mdada na hakuja shule alirudi pale pale akaja kesho yake akatuambia yaliyomkuta
na mwenyewe anasema wanafanana kweli na yule mzee ila kamkataa
je jitu km hilo likiitwa mbwa ,pimbi,shenzi kuna ubaya?
Ndo kama hujui huna cha kudai,asiyekuwepo na lake halipo!Madhali kama mtu amesimama na kusema anazuia mawasiliano na ana sababu za msingi inabidi tuheshimu maamuzi yake kwasababu hatujui lolote kuhusu mahusiano yao mpaka wakafikia hapo!Unafikiri yeye hajui kama mtoto wake anatakiwa awe na father figure?Nadhani si rahisi kwa muhusika vilevile kupitia hayo.Na mpaka amepata guts za kusema ujue ni pride aloisimamia!
Ni kazi hasa,yaani ila ile kuwa watakua,hata mimi nilishawahi kuwa mtoto ndo huwa inanitia moyo sanaPole sana mumie,Mungu akupe nguvu za kulea wanao wawe watu wenye hekima na busara!Watu wengine hawaelewi kabisa ni uzito mkubwa kiasi gani alokuwa nao single parent.Wanachukulia rahisirahisi sana na inakera!
Akisoma hapa anajisemea hili langu hili,ila hatuingii mioyoni mwao.
Mkuu wangu hii kitu nimeishuhudia kwa macho yangu.Kipindi nafanyakazi shirika moja la umma kijana mmoja umri kama miaka kumi na nne / kumi na tano wakati huo kaagiziwa na Mama yake (kilimanjaro) sehemu Baba yake anapofanyakazi bahati mbaya siku hiyo (Baba mtuhumiwa aliaga anakwenda bank) tuna share ofisi moja walinzi walipopiga simu nikapokea wakanieleza kuna kijana anataka kuonana na fulani nikawaambia wamruhusu aje amsubiri ofisini kijana akaingi kanisalimia vizuri nikamkarisha kiti nikamweleza anayemtafuta kaenda bank atarejea baada ya dk 10.Kweli after 10 minutes jamaa kaingia ofisini nikamweleza ana mgeni wake wakasalimiana Kijana bila kupoteza muda akaanza kutiririka sababu zilizomleta Arusha duh Baba mtu akamtolea nje na kumweleza Mama yake ni mwongo yeye hausiki kabisa na akamwomba kijana aondoke wala asirudie tena kumfuata futa.Sitakaa katika maisha yangu nisahau huo mkasa basi kijana akanyanyuka kwa unyonge akaomba nauli ya kurejea Moshi Baba wa hiyari akakataa kutoa nauli ikabidi niingilie kati nikampatia nauli kijana akatokomea zake.
Baada ya kama miaka 8 - 9 kupita tangu tukio hilo litokee (shirika la umma lilikuja kufa kila mtu akashika hamsini zake) siku moja nipo mitaa ya Arusha City Parks napata moja moto moja baridi nashangaa natelewa bia 5 kwa mpigo nikashtuka nikamuuliza muhudumu kulikoni akaniambaia kuna jamaa kaniambia nikuletee hizi bia nikajisemea huyu lazima atakuwa katoka Merereni ndio wenye tabia hizo basi nikamwambia muudumu mwambie asante.Wakati naendelea kupambana na bia akajitokeza kijana aliyeninunulia na kujitambulisha kwangu na kunielezea lile tukio na jinsi nilivyomwokoa kwa kumpatia nauli kwani hakuwa anamjua mtu yoyote Arusha kipindi hicho.Si kwamba nilifurahi tu bali machozi ya furaha yalinitoka kwasababu kwanza kijana maisha yamemyookea haswa ni IT manager wa organisation ya kimataifa.Nikimtazama anafanana na Baba yake kila kitu nikajiuliza hivi sisi wababa tuna laana gani unawezaje kumkataa mtoto wako kisa unataka kulinda ndoa yako au usionekanane zamani ulikuwa mwingi wa habari.Unajua wengi hapa jamvini mmeshindwa kumwelewa Kilaza lakini ni bora usitie neno kama hujui machungu aliyokumbana nayo.
wanaume mara nyingi ndo wanakana mimba na single dads wapo ila wachache sana
Dhiki ndo inawatuma kwani we unaonaje?maana sasa tutatoka nje ya mada!!!Wanaotupa watoto wachanga ama kukana mimba hawajui kama si sawa? Kwa nini wanafanya sasa? Kuna justification?
Pride yake si lazima iwe pride ya baba/mtoto.
Ni kweli usemayo,yametokea tunapambana no way.
Sijaona sababu ya wewe kukasirika...
Kulea mtoto hakukupi haki ya kuwa baba yake..
Baba atabaki kuwa baba...mjomba atabaki kuwa mjomba...