Sinagogi hili la Siloam Ministries

Sinagogi hili la Siloam Ministries

Hiyo siku nimekaa mahali napiga bia zangu wakapita wanajadiliana eti mmoja anamwambia mwenzie Jana umeme ulikatika ile anaanza kusali, babaaa.... Umeme hapo hapo ukarudi..nilichke sana
Wewe nitakupiga aisee... nimecheka mbele ya watu wanaoniheshimu.
Nimeonekana kituko.
Sasa ndugu si kaomba nae kapewa hata hajamaliza kuomba.
 
Dini ni masrahi ya watu jamani. Iweje Mungu awe mmoja na sie tusiwe wa moja? Iweje Yesu mmoja lakini tuko wakristo tukitofautiana mambo ya hivyo tu?
 
kwao wiki inaanza alhamisi
Na wanadai hakuna mchana na usiku kuna majira ya mchana ambayo huanza kumi na mbili asubuhi mpaka kumi na mbili jioni na majira ya nuruni kuanzia saa moja usiku
 
Ila jama katika majipu naona na Viongozi wetu wangeanzia humu kwenye haya makanisa yaliyochipukia sasa ule uhuru wa kuabudu naona umevuka mipaka kuna mambo ya ajabu sana humu mtu tooka asubuhi mpaka jioni sijui mikesha mwanzo mwisho hizo kazi huwa wanafanya saa ngapi alafu useme maisha magumu
Ningekuwa Rais wa Tanzania, ningeyafunga na viongozi wangepelekwa nanii ili wa pone.

Wanachumia tumbo kwa kutumia ujanja wa viini macho.
Angalia mabango yao. Haya mtukuzi MUNGU, bali mapicha yao na majivuno eti Dr. Mtume. Asikofu rev. transfoma. Bulidoza....mzee wa upako...hii ni sawa na sifa na utukufu ni kwao????????wana boa
 
Wana bifu sababu ya hela.KANISA (Mke wa marehemu Eliya kizazi cha nne) anataka kuwapanda kichwani kina MIAKA 1000(Ambaye Eliya alimkabidhi huduma).Sasa WAKUU WA NJIA hawamkubali MIAKA 1000,wameenda kumchoma kwa KANISA.KANISA amepata kiburi akazira kusali hapo makao makuu mbezi.
Mbona sikuelewi ...WAKUU WA NJIA ni akina nani?

Kumbe ulisikia
 
Dini ya leo ni biashara inayolipa sana na kila mwenye uelewa kidogo wa theolojia hutaka kuanzisha kanisa lake
Kuna baadhi licha ya pesa Kuna mambo ya siri wanafanya au wana taratibu zao zenye kuacha maswali mengi
Hivi karibuni nilikutana na mwamimi aliyekimbia kanisa la Sialom mkoani pwani akanihadithia mengi ya kushangaza
-kwao majina si kama haya yetu bali majina yao ni kama haya..Siku yake!Ahadi!Agano! Kimbilio! Jaribu nk nk
-Chakula kwao wanaita karamu
-Maji yanaitwa damu yake
-wakipigiwa simu hawataji eneo husika bali wanasema wako mlima wa moto ili adui asijue uko wapi
-Wanaamini makombo ni tiba (makombo ya Chakula wanakula makuhani wao )
-viongozi wao wanajulikana kwa jina la makuhani
-ibada zao huanza saa sita alfajiri kwa kughani maneno ya kujirudiarudia tena kwa sauti ya juu (kupayuka)
-nguo zao ni suruari fupi nyeupe na kanzu
Maisha yao kwa sehemu kubwa wanategemea malipo kwa wale wanaokuja kuponywa kanisani
Hii ni imani lakini ni vema ukaamini kitu kisicho na ukakasi...muumini huyu amefanikiwa kukimbia na sasa yuko huru
Pia wanabadili jina la ubini mf. mshana kuhani badala ya mshana Jr:
 
Hamna lolote hili dhehebu ni tatizo Mimi nilishtuka na kuogopa waliponiambia kwamba shetani alishauwawa na huyo mwazilishi wao Elia. Bila maono ya Roho Mtakatifu wengi wataangamia.
Ndugu yangu ukisema hamna lolote unakosea. Kwa taarifa yako haya yote ni mpango wa Mungu. Mungu anao uwezo wa kufanya watu wote kuwa kitu kimoja lakini hakutaka iwe hivyo. Ndiyo maana Yesu alitamka bayana kwamba "sikuja kuleta amani bali mafarakano", akiwa na maana wapo watakao muamini na watakao mkataa na kutokana na hilo watu watafarakana. Siku ya pentekost Roho Mtakatifu aliwashukia wale tu waliokuwa wakisali pamoja na wanafunzi wa Yesu si kwa watu wote na ndio ulikuwa mwanzo wa kanisa. Ni vizuri kuamini katika Roho Mtakatifu lakini si vyema kusema wasio amini katika hilo ni hamna lolote. Ukifanya hivyo tofauti yako na wale wa IS (dola la kiislam) hamna tofauti, sema tu hujapata silaha. Nakushauri simamia imani yako. Waweza kuangalia bila kukashifu imani ya mwingine usije kuwa chanzo cha vita ya dini. Tumsifu Yesu Kristu!
 
5c59d71f254c8430e4e2a0a0fd2026fe.jpg

Mama yangu Amefika hatua hii
Kisahawaruhusiwi kwenda hospitali
 
Maombi yao kwa wagonjwa ni kuwafanyia jaribio waumini !! Wao wakiugua wanawahi hispitalini fasta!! Wanakwambia mtegemee Mungu kwa ulinzi wako, halafu wao wanalindwa na mabaunsa!! Duu hizi imani uchwara kazi kweli kweli !!
 
Ha ha ha mkuu mshana jr, shika neno.....

Watu wanaojiita wakristo ni wapumbavu sijawahi ona
Ishia hapohapo wewe usiye heshimu imani za watu. Imani tumeletewa na watu wa mataifa, sie tulikuwa tunaabudu mizimu. Heshimu imani ya mtu, hata kama mtu anaabudu shimo la choo elewa ndiko imani yake ilikolalia we heshimu tu hutapungukiwa na kitu
 
Gari wao wanaita farasi, kimbembe sasa ni kwny majina ya mikoa...... yani yote imebadilishwa majina wametunga ya kwao tu, halafu hawa jamaa c ndo kiongozi wao alikufaga kwa tetenus wao wanang'ang'aina kutuaminisha eti alipaa mbinguni
 
Kitanda wanaita madhabahu kuna jamaa tulikua tunakaa nae room moja anasali hilo kanisa,sasa one time akawa anaongea na demu wake kwenye simu akamwambia demu " mi niko madhabahuni" yaani kitandani.
Zanzibar wanaita kaanani, kuna siku jamaa akapata safari ya kwenda Zenji akawa anatuaga " jamani mi naenda kaanani" Dah! tulichoka.
Jina la jamaa sasa WISDOM GOD OF MERCY
 
Back
Top Bottom